Bado ngoma haijaanza, usianze mchezo!

Samahani

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
222
335
Unajua sio lazima kila saa uoneshe ni kwa kiasi gani unajua mambo fulani fulani kichwani mwako! Ndio maana niliwahi kuandika kuwa, maarifa ni sawa na uchi tu. Ni lazima kuwa nayo, lakini si busara kuyaweka hadharani muda wote!

Kuna wakati ni vema maarifa yakawekwa nyuma, kisha tukawaacha wenye ujuzi au maarifa makubwa zaidi watende kitu fulani. Hii iliwahi kumsaidia mama fulani msomi na mwenye maarifa makubwa, akafaidika sana na utulivu wake.

Unajua ilikuwaje? Ndio uketi sasa nikuhabarishe

Huyu mama aliyekuwa msomi wa elimu mbalimbali za dunia, alikuwa na mwanae pekee wa kike aliyekuwa anaumwa sana. Achana na kuumwa unakokujua wewe bwana. Eti unasingizia kuumwa kisha unameza panado kwa kusindikizia na Serengeti Lager, ukipona unatuambia ulikuwa unaumwa.

We endelea tu, Utakipata unachokitafuta

Binti alikuwa anaumwa kweli kweli! Sina hakika kama alikuwa amefikia hatua ya kuitwa mgonjwa mahututi, ila nnavyosikia alikuwa na homa ambayo ilimbadili mpaka rangi, akawa na rangi fulani katikati ya buluu, kijani na njano. Akawa hata kuzungumza hawezi, akavimba yote mapaja na kutetemeka mwili.

Mama yake akaona isiwe tabu. Asingeweza kuvumilia zaidi kumwona bintiye akitaabika. Akamwendea tabibu mmoja mashuhuri ambaye sifa zake na jina lake vilimtangulia kila alikokwenda. Mathalani alipotoka pahala fulani kwenda pahala pengine, upepo ungeweza kabisa kupelekea sifa zake upesi kule alikokuwa akielekea na alipofika, alikuta msururu wa wagonjwa, akawapa tembe kadhaa za dawa, wakapona ndani ya muda mfupi.

Naskia kuna wagonjwa walikuwa wanapona kwa kusikia tu sauti yake. Hili nimesikia tu.

Alikuwa tabibu bingwa huyu bwana!!

Sasa yule mama akamsaka huyu tabibu, akampata. Nakukumbusha tu kuwa huyu mama alikuwa ni mjuzi wa elimu nyingi tu, ingawa udaktari hakuwahi kuusomea. Akamsihi sana yule daktari akamsaidie binti yake.

Yule daktari 'akachomoa'!!

Hakuchomoa kwa kuwa alikuwa mchoyo wa elimu aliyokuwa nayo.. Bali alitoa sababu ya msingi kabisa. Alikuwa akiwahi sehemu fulani muhimu sana siku ile, sehemu ambako kulikuwa kuna wagonjwa mahututi kabisa waliokuwa kufani! Akamkatalia mama yule kistaarabu kabisa, lakini mama akazidi kubembeleza!

Ama..!! Bwana mkubwa yule akaona isiwe tabu.. Akamjibu kuwa, siku hiyo alikuwa na dawa za gharama na zenye nguvu mno, isingekuwa busara kutumia dawa zenye nguvu kubwa kwa kuwapa wagonjwa mahututi kama binti yake yule mgonjwa!! Aliamini kwa kujibu hivi, mama yule angejiondokea zake. Lakini mama yule, ambaye hakutaka kabisa kuonesha maarifa yake wakati ule kwa kuwa hayakuhitajika, akawa mpole na kuanza kujiondokea huku akijisemea mwenyewe kwa sauti hafifu..

“Sawa bwana daktari.. Ila kuna saa hata magonjwa mahututi hujikuta wakisalimika japo wakiuona tu uso wa daktari. Ikiwa ungeamua, binti yangu angepona..”

Haya aliyasema huku akijiondokea… Daktari yule akasimama mara moja. Akamwita mama yule na kumwomba radhi. Akampa vidonge kadhaa na kumpa maelekezo muhimu. Ndani ya siku mbili, binti yule alikuwa akicheza rede na kusutana na wenzake wakielekea kisimani.

Kuna saa unyenyekevu unalipa sana… Ni vile tu tumeumbiwa ubishi..

Enewei.. Hilo silo lililonileta leo… Hilo mi mwenyewe nilisimuliwa zamani kidogo.. Acha nikupe ambalo nina uhakika nalo.

Kuna saa tunajiwazia mambo ya kijinga sana.. Lakini wala tusilaumiane kwenye hili. Nilishasema juzi kuwa, mawazo huja kwa nasibu, haina haja kupambana kuyazuia. Ila kuna nyakati ambazo mawazo yetu yanawaza ujinga mara mbili zaidi.

Fikiri tu uwapo na njaa, au kukosa pesa, au kuandamwa na madeni, kuwa mgonjwa na katikati ya tabu nyingine kadha wa kadha. Binafsi naamini kuwa, hizi ndizo nyakati ambazo huwa tunajikuta tukiwaza ujinga mara mbili zaidi. Sasa haya yaliwahi kumkuta mzee mwenzangu siku za nyuma.

Ndio utulie sasa nikuhadithie kwa kina.

Huyu jamaa alijaliwa kuzaliwa kijijini hasa, pahala ambapo, kila kitu kilimlazimu kutumia nguvu nyingi kukipata (isipokuwa mke ambaye alimpata kwa kumkwatua ngwala tu, habari ikaishia hapo). Ilimlazimu huyu bwana atumie jasho lake ipaswavyo kila siku akifanya kazi kwa juhudi kubwa. Kuna wakati ilimlazimu alime mchana wa jua kali ili jasho lake litumike kuyamwagilia mazao yake.

Jamaa alipambana kwelikweli.

Lakini matunda ya jasho lake hayakulingana na nguvu aliyoitumia kulizalisha jasho lile. Alizalisha jasho la kutosha lakini mavuno hayakufidia kabisa jasho alilomwaga. Yeye na familia yake wakazidi kunyong’onyea. Alitamani kuiba, lakini akakumbushwa kuwa, wizi ni dhambi kama tu mauaji. Akatamani vya wenzake, lakini akakumbushwa katika ibada kuwa, kutamani nako ni dhambi kama tu kuzini na mke asiye wako.

Akalazimika kulikamata jembe lake kwa umakini zaidi. Yeye na mkewe na watoto wao, wote wakaiangukia Ardhi. Msimu mmoja wangevuna vizuri, halafu msimu mwingine wakavuna vichache kupita maelezo. Njaa ikawa rafiki yao. Siku moja, yeye na mkewe wakawa wakijisomea kitabu kitakatifu cha Mungu kwa tafakari kubwa. Huko, wakaisoma tena ile habari ya Adamu na mkewe Hawa.

Katika tafakuri yao, wakagundua kuwa, hawa wapenzi wawili wa mwanzo waliishi katika bustani safi iliyokuwa na maziwa na asali. Wakajaribu kukumbuka wao mara ya mwisho walikunywa maziwa lini..

Matumbo yakawavuruga kwa kule kuwaza kwao chakula wakati hawakuwa wamekula kwa siku nzima

Wakatazamana, kisha wakaendelea kutafakari.

“Wanawake watu wa ovyo kabisa.. Bora Hawa asingezungumza na nyoka.. Kwani angemchunia tu ingekuwaje? Tusingekuwa tunasota hivi kwa shida”. Alianza mwanaume kwa hasira.

Mwanamke akainamisha kichwa chini na kuchora chora mchangani.. Kisha akainuka naye akajisemea peke yake.

“Wanaume watu wa ajabu sana.. Bora Adamu asingekubali kupokea tunda kutoka kwa Hawa. Labda Mungu angemuadhibu tu Hawa kwa kumuua.. Kisha akaumbwa mwingine. Tusingekuwa tunasota hivi kwa shida.

Bwana wee…

Walibishana hao mpaka kigiza kikaanza kubisha hodi. Wakaenda kulala huku wakibishana kwa nguvu. Wakati wanakaribia kulala, wote wakakubaliana kuwa, waliokuwa na makosa walikuwa wale wazazi wa mwanzo kwa kule kukosa kwao umakini wa kuzingatia kanuni rahisi tu waliyopewa na Bwana Mkubwa, Muumba wa vinavyoonekana na visivyoonekana..

Wakalala wakiwa na hasira kupita maelezo!

Asubuhi si ikafika bwana?

Wakashangaa sana kugongewa mlango wao. Hawakuwahi kutembelewa na majirani kwa ule ufukara wao. Nani angewafuata? Awafuate akachukue kitu gani kwao? Mume akakurupuka upesi. Sio kwa shauku ya kumwona mgeni, bali kuwahi kuuzuia mlango usije ukavunjika kwa kule kugongwa gongwa. Mlango wenyewe ulikuwa mlango basi?

Nyumba ya tabu hata kuta zake ni tabu tu.

Alipofungua kile kinachofanana na mlango, akakutana na kikongwe mmoja aliyekuwa na haraka kwelikweli. Wala hakungoja salamu zikamilike. Akatoa kifuko kilichofungwa vema na kumkabidhi bwana yule…

“Samahani mwanangu.. Nna safari ya mbali nakwenda, naomba unitunzie kifuko hiki. Kuna kijana atafika hapa baadae kukichukua. Ana nywele ndefu na ndevu ndefu pia. Nilimngoja pahala nimkabidhi lakini nimesubiri sana. Naomba sana usikifungue tafadhali. Chondechonde, usije ukathubutu kukifungua.” Alimaliza kikongwe yule na hata kabla ya kungoja jibu akanza kujikongoja kutokomea katika kigiza ambacho kilikuwa kinaanza kufukuzwa na nuru ya jua.

Basi bwana…

Siku ile ilipita, na iliyofuata, na nyingine tena.. Mwaka wa kwanza, na wa tatu, na wa tano, kisha kumi ikatimia!! Halafu wa kumi na moja na wa kumi na mbili.. Hakuja kikongwe wala kijukuu wake kuchukua kidubwasha kile. Walingoja na kungoja, lakini hakutokea yeyote kati ya walioyemtegemea.

Mwisho walichoka!!

Wakaona huu sasa ni ujuha!! Iweje waendelee kungoja mtu asiyefika? Wakaketi, bwana upande huu, na bibi upande ule. Wakashirikiana kwa uangalifu mkubwa, wakakifungua kifuko kile.

Lahaula!!!

Kulikuwa na sarafu nyingi sana za dhahabu, jozi kadhaa za lulu, vipande vya almasi, na tunu nyingine nyingi sana. Walijikuta wakikenua na kumshukuru Mungu kwa zawadi ile. Upesi wakawaendea wanunuao tunu zile, wakauza kiasi kidogo sana kisichofika hata moja ya kumi ya hazina ile. Kiasi hicho tu kikawashangaza kwa namna kilivyowajaza mapesa.

Upesi wakayabadili kabisa maisha yao. Sasa hata rangi za ngozi zao zikarudia kuwa zenye rangi ya kueleweka.
Wakaingia katika kundi la watu wa kuheshimika katika mabaraza ya mji! Wakajijengea na jumba kubwa pale kilipokuwa kile kichuguu walichokitumia miaka nenda miaka rudi wakikiita nyumba. Loh!! Waliheshimika, na bado walikuwa na hazina kubwa mno katika ghala yao!!

Miezi kadhaa baadae, hamadi!! Wakapata mgeni.

Kizee yule alifika akiwa amekongoroka zaidi. Alikuwa na haraka kama kawaida yake. Akawasalimu na kuwakumbusha kuwa, alikuwa amefuata kifuko chake!!

Salaaaale!

Walitafutana!! Walihangaika wakiigiza igizo bovu la kukisaka huku na kule kitu ambacho walijua wazi kuwa hakikuwepo. Kikongwe alibaki kuwatazama tu kwa makini. Wakiwa wanajiweka tayari kuigiza igizo la mwisho kwa kuchukua ile hazina iliyobaki ili kuifungasha tena na kuirudisha kwa mwenye nayo, kikongwe akawaambia kwa upole..

“Si vema sana kuanza kutengeneza mitindo ya machezo kabla ya ngoma.. Usilolipitia si vema kulijadili. Nilikuwa mpita njia tu siku ile mlipokuwa mkilalamika na kuwalaumu hao ambao hamjawahi hata kuwajua. Nilifikiri nilipaswa kuwapa somo fulani.. Huenda sasa mmejifunza”.

Akajiondokea akiwaacha wametumbua macho.

Kuna wakati tunajikuta tunahangaika na mambo ambayo hatuyafahamu!! Kuna wakati tunaanza kuwalaumu watu ambao, hali wanazopitia, kama tungelikuwa ni sisi, huenda tungechukua maamuzi mabaya zaidi ya wanayochukua wao. Hebu fikiri.. Mtu unaweka soda kwenye jokofu ukijiapiza kuwa utainywa kesho!! Ila unalala ukiwa unaiota usiku kucha. Uzalendo unakushinda usiku wa manane kwa kuwa, kuna aina fulani ya kiu hujawahi kuipata tangu uzaliwe.

Unaamka tena kwa kunyata na kuishambulia kama vile si wewe uliyeinunua!! Ni wewe unayemlaumu mchungaji wa kanisa unaloabudu au kadhi wa msikiti unaoswalia kwa kubadili matumizi ya mifuko ya saruji iliyonunuliwa Ili kuziba ufa katika kiambaza cha kanisa au msikiti, badala yake akaitumia kurekebisha msingi wa nyumba yake?

Usiku na mchana unawalaumu viongozi wa dini na serikali kwa kutokutimiza wajibu wao kikamilifu. Tena kuna saa unaongea mpaka unatulowesha kwa mate tunaokuzunguka!! Ila kila siku asubuhi unapotoka kwako, unaahidi utaletea watoto wako pipi, lakini badala yake, unarudi ukiwa umelewa na badala yake unaanza kuwalazimisha wakuvue soksi zako ambazo kutokana na utoro wako nyumbani hata mkeo hapati nafasi ya kuzifua!! We bwana we, uko makini kweli na ujuha wako?? Maana majuha wenzako pia tunakushangaa!!!

Unailalamikia ofisi yako kwa kutokukuongezea mshahara. Yani kwako ni jambo dogo tu, kwamba mwajiri ameshindwa kutambua thamani yako na kukuongezea njuluku kidogo. Lakini kila ukiingia ofisini wewe ndio wa kwanza kutumia muda wa maongezi uliopewa na ofisi kuongea na kimada, na kuna wakati kwa umaluhuni wako unajikuta unatumia mitandao ya ofisi kutazama picha za "hovyo hovyo". Binti wa kazi nyumbani kwako ana mwezi wa pili sasa hata nguo ya ndani hujamnunulia, fedha yake unasingizia unamuhifadhia!!

Hivi we ndio tawi gani la benki vile?? Unakwama wapi mpaka unashindwa kuwa mwaminifu kwenye madogo huku ukipuyanga kulalamikia makubwa?? Unayaweza kweli wewe?

Una mali kidogo tu, lakini kila ukienda mjini, huwezi hata kutoa sarafu moja ukampa ombaomba. Halafu unaomba kazi kwenye kampuni kubwa, unanyimwa, kisha unaanza kutoa milio ya ajabu ajabu!! Usipokuwa mwaminifu kwenye madogo, huwezi kuaminika kwenye makubwa.

Unashindwa kuwa mwaminifu kwa mkeo uliyemuoa kwa miaka kumi sasa.. Halafu leo unamlalamikia raisi wa taifa fulani ambaye ameshindwa kuwa mwaminifu kwa wananchi wake? Rafiki yangu… Acha kucheza ngoma ambayo bado haijaanza kutoa mvumo. Huenda wewe ungepewa nchi hiyo uitawale, ungeshaiuza siku nyingi na pesa yake ungewahonga wanawake wa babeli ya kisasa!

Tumia ngoma ipitayo masikioni mwako kutunga mtindo, tutakuelewa. Fikiria ukubwa wa tatizo lako kisha ulitatue, utakuwa mshindi! Si busara kuwatupia lawama watu wanaokosea katika nafasi zao kubwa huku wewe ukipuyanga vibaya katika nafasi yako ndogo tu.

Huenda tukikosea na kukupa nafasi zao, hata yule aliyezungumza na Hawa kule bustanini atakukana na kusema, “Ondoka kwangu haraka mwanaizaya we, sikujui kamwe mimi!!”.

Shauri yako...
 
Huyu mama aliyekuwa msomi wa elimu mbalimbali za dunia, alikuwa na mwanae pekee wa kike aliyekuwa anaumwa sana. Achana na kuumwa unakokujua wewe bwana. Eti unasingizia kuumwa kisha unameza panado kwa kusingizia na serengeti, ukipona unatuambia ulikuwa unaumwa.

Sasa yule mama akamsaka huyu tabibu, akampata. Nakukumbusha tu kuwa huyu mama alikuwa ni mjuzi wa elimu nyingi tu, ingawa udaktari hakuwahi kuusomea. Akamsihi sana yule daktari akamsaidie binti yake. Yule daktari akachomoa!!

Akalazimika kulikamata jembe lake kwa umakini zaidi. Yeye na mkewe na watoto wao, wote wakaiangulia Ardhi. Msimu mmoja wangevuna vizuri, halafu msimu mwingine wakavuna vichache kupita maelezo. Njaa ikawa rafiki yao. Siku moja, yeye na mkewe wakawa wakijisomea kitabu kitakatifu cha Mungu kwa tafakari kubwa. Huko, wakaisoma tena ile habari ya Adamu na mkewe Hawa.

Unaamka tena kwa kunyata na kuishambulia kama vile si wewe uliyeinunua!! Ni wewe unayemlaumu mchungaji wa kanisa unaloabudu au kadhi wa msikiti unaoswalia kwa kubadili matumizi ya mifuko ya saruji na kurekebisha msingi wa nyumba yake?

Nigga uandishi wako umenikumbusha vitabu vya Shaaban Robert. Dah vile vitabu ulikuwa unavisoma huku unatabasamu. By the way somo zuri.
 
Aliyesoma yote asamarise tafadhali ....
 
unatumia mitandao ya ofisi kutazama picha za "hovyo hovyo". Binti wa kazi nyumbani kwako ana mwezi wa pili sasa hata nguo ya ndani hujamnunulia, fedha yake unasingizia unamuhifadhia!!
 
Huenda wewe ungepewa nchi hiyo uitawale, ungeshaiuza siku nyingi na pesa yake ungewahonga wanawake wa babeli ya kisasa!
 
Mkono wako umeeleweka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom