Mwamba kama umeshawahi kupotelewa na boxer au soksi ujue umekwisha

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Mpaka mida ya saa nane adhuhuri binti haonekani, ikafika alsir around saa kumi na moja hakuna anayejua kapatwa na masahibu gani binti wa watu.

Aliondoka home majira ya saa sita tukajua ameenda dukani, kwakuwa ni mgeni maeneo haya na siku hiyo ilikuwa siku ya mnada huwa pamechangamka sana tukahisi huenda ameenda kuosha macho kidogo ukizingatia ametoka mkoani mda si mrefu.

Huyu ni binti wa kazi toka geita, si mgeni sana kwetu kwakuwa alishawahi kuishi na sisi, na tuliishi nae vizur tu, kwani kwetu dada wa kazi huchukuliwa kama ndugu kabisa na huenda usijue kama dada wa kazi mpaka labda uambiwe .

Kutokana na kuishi nae vizuri hata alipokwenda kwao bado mawasiliano yaliendelea kuwepo kama ndugu wanao juliana hali,, basi ikatokea uhitaji wa mdada wa kazi, basi kumbe alikuwa na mpango wa kuja dar es salaam, ishu naona ilikuwa nauli coz kutoka huko mpaka hapa ni kama kwenye elfu sabini hivi.

Alitumia nafasi ile kujifanya anataka kufanya tena kazi kwakuwa hakuwa na shughuli yoyote kwa mda ule, kwakuwa tuliishi nae vizur alikuwa mpiga kazi mzuri tukaafiki yeye atumiwe nauli kisha aje afanye kazi.

Alikaa Wiki moja tu kisha akapotea katika namna ile ya sintofahamu, kabla ya siku ya tukio alikuwa yupo bize sana na simu na mara nyingi alikuwa anatoka nje kuongea tofauti na siku za nyuma,nadhan ndio alikuwa anapanga mikakati yake namna ya kuelekea sehemu anayoijua yeye.

Mpaka inafika saa kumi na mbili bado hajarudi tukaona hapa kuna namna, tukamvutia waya laa haula simu haipatikani, mwamba nikaunganisha dotsi nikajua hapa tumepigwa,,,kwenda kucheki nguo zake zipo,na kingine kilicho tushangaza alikuja na nguo chache sana Kana kwamba si mkaaji,kwahiyo ukiunganisha dotsi unapata jibu kuwa alikuwa na mission maalum katika Safari yake.

Sasa ile kufungua nguo zake sasa zilizobaki laa salale, tukakuta kuna boxer ya mwamba chafu chafu hivi na kuna soksi, halafu kuna kibiriti, ukicheki vizur boxer hapa mbele ni kama ilikuwa inachomwa na moto wa njiti ya kiberiti huenda alikuwa anafanya manuizi flani hivi, kama haitoshi kuna hirizi mbili ambazo kama zimefungwa hivi, kwa elimu yangu ya Cuba nimegundua zile hirizi ni kama yake moja na huyo bwana moja kwakuwa zimetengenezwa kama umbile la mwanadamu, kwahiyo ni kama wamefunganishwa pamoja hakuna kuachana.

Nikajua hapa mwamba kaumia, hapa haendi popote wala hasemi chochote yaani kwisha habari yake, mkiona wanaume sometime wanakuwa mazezeta na hawana kauli kwa Madam zao basi NI KUWAOMBEA DUA TU.


Nawatakia mfungo mwema wa Ramadhani.

Ni hayo tu!
 
What I know is, good judgment comes from experience, and experience comes from bad judgment. So..... If you don't mind, it doesn't matter Mwa J takes whatever boxers...😊
 
Back
Top Bottom