Badala ya kusema VICOBA sio vizuri, tumieni muda huo kutoa Elimu ya nidhamu ya matumizi ya fedha

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Vijana wa kiume na wanaume wengi wakiwa wamejiajiri kwenye bodaboda, vijana wa kike na wamejikita kutafuta mitaji ya biashara kupitia VICOBA.

VICOBA mpaka sasa vimesaidia wengi sana kutokana na unafuu wa riba na upatikanaji wake kulinganisha na taasisi nyingine za kifedha na zimesaidia kuwakwamua sana wakina mama.

Tofauti na matarijio ya kuanzishwa kwa VICOBA sasa hivi vimechukuliwa kama njia ya kupata pesa ya haraka kwa kufanya matumizi ya anasa. Ushahidi ninao wa wanawake waliokopo kwenye VICOBA na pesa wakaenda kununulia simu za kisasa au kwenda kufanyia sherehe, hapa tuseme ukweli tu lengo la VICOBA limepotoshwa.

Mbaya zaidi kuna mwanasiasa ambaye anajua nidhamu mbaya ya pesa mahali popote inavuruga mipango na matumizi ya pesa ya VICOBA. Wakina mama hawa wanahitaji Elimu kubwa zaidi ya matumizi sahihi na nidhamu ya pesa. Ningewaona wa maana kama mngewashawishi kutumia VICOBA kuongeza mitaji na kukuza biashara zao.

Lema na CHADEMA ujumbe huu uwafikie popote
 
Back
Top Bottom