Babu wa samunge na kikombe chake!!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Mwaka jana kipindi kama hiki mjadala juu ya kikombe cha babu wa samunge ulitawala katika vyombo mbalimbali vya habari na maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi walifurika katika kijiji cha Samunge kupata kikombe. Hapa nchini watu wengi maarufu wakiwemo wanasiasa na watendaji wa serikali nao walipata kikombe. Ikiwa takriban mwaka mmoja umepita tangu kikombe cha babu kianze kutolewa tujadili success and failures za kikombe. Je kikombe bado kinapatikana kule samunge!??????
 
Nawafahamu wawili waliopata kikombe wameshatangulia mbele ya haki.
 
Babu yule mimi namsifu sana, Rais wetu angekuwa na uwezo ule wa kukusanya mapato, fikra za watu na attention ya wagonjwa Tanzania ingesonga mbele.
 
Nipo mitaa ya Samunge huku katika boma la mbwa mwitu (wild dog sanctuary)
Naona kuko kimya kabisa hatupishani hata na magari yanayoenda kwa babu.
 
Jamani kipindi kile hamkumbuki kuwa ndo mjadala wa kuilipa Dowans ulikuwa umeshika kasi? Yani magamba walikuja na plan ya hali ya juu wakatupotezea kwa babu loliondo. Mh hata wale viongozi wa KKKT wa kaskazini walimpamba kweli huyu mzee. siku hizi siwasikii Kazi kweeli kweeli
 
da ila safari ile niliipenda sana ya kwenda samunge! mandhari ya Oldonyo lengai, Lake Natron, wasonyo, ilikuwa adventure moja tosha kabisa
 
Nipo mitaa ya Samunge huku katika boma la mbwa mwitu (wild dog sanctuary)
Naona kuko kimya kabisa hatupishani hata na magari yanayoenda kwa babu.
Tupo Samunge hapa washkaji wanasubiri kugonga kikombe kwa Babu,hawaruhusu kupiga picha,na kuna walinzi hapa.
 
Mwaka jana kipindi kama hiki mjadala juu ya kikombe cha babu wa samunge ulitawala katika vyombo mbalimbali vya habari na maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi walifurika katika kijiji cha Samunge kupata kikombe. Hapa nchini watu wengi maarufu wakiwemo wanasiasa na watendaji wa serikali nao walipata kikombe. Ikiwa takriban mwaka mmoja umepita tangu kikombe cha babu kianze kutolewa tujadili success and failures za kikombe. Je kikombe bado kinapatikana kule samunge!??????
mwenzenu Babu aliona staili pekee ya kutoka ni kuhusisha utapeli wake na imani ya kidini na hapo ndipo alipopiga bao,mimi namsapoti babu kwa kuweza kuwadanganya watanzania wenye elimu zao kurudi kwenye zama za stone age
 
hili mjadili na magamba maana ndo waliongoza misafara kwenda kwenye kikombe
 
Back
Top Bottom