Amuua mkewe ili aishi na mwanafunzi wake wa miaka 16 kama mke wake

Mbaga Lazaro

Senior Member
Aug 9, 2020
132
107
Kesi hiyo haikutatuliwa kwa zaidi ya miaka 40.

Hadi Jumanne iliyopita, jaji wa Mahakama Kuu ya New South Wales nchini Australia alipomkuta Chris Dawson, 74, na hatia ya kumuua mkewe, Lynette.

Chris, mchezaji wa zamani wa raga, aliishi na mke wake pamoja na na watoto wao wawili huko Sydney.

Walikuwa familia iliyoonekana kuwa ya kawaida hadi mke wake alipotoweka bila maelezo mnamo Januari 1982. Alikuwa na umri wa miaka 33.

Chris alikuwa ameachana na mchezo wa raga mwishoni mwa miaka ya 1970 na alikuwa akifundisha elimu ya viungo katika shule ya umma kwenye Fukwe za Kaskazini za Sydney.

Akiwa huko alipendana na mmoja wa wanafunzi wake kijana, Joanne Curtis, aliyejulikana kama JC wakati wa kesi ambapo uamuzi tayari umefikiwa katika kesi hii ya kushangaza.

Kukosa Uaminifu

JC alikuwa na umri wa miaka 16 tu wakati Chris alipovutiwa naye, kwa mujibu wa maelezo yaliyofichuliwa katika kesi na katika kipindi cha podikasti ya uchunguzi ya 2018 iliyoibua kesi hiyo, The Teacher's Pet.

Joanne alikuwa anatoka katika familia iliyovurugika, ambapo vurugu na pombe vilikuwa sehemu ya utaratibu wa kila siku.

Licha ya ukweli kwamba msichana huyo alikuwa mdogo, Mara mbili ya umri wake na alikuwa ameoa, profesa huyo alianzisha uhusiano wa karibu naye.

Chris alimuajiri kijana huyo kama mfanyakazi wa ndani nyumbani kwake na kuanzisha uhusiano wa siri na yeye.

Kulingana na ushahidi wa JC wakati wa kesi, wote wawili walikuta kimwili kwa siri wakati Lynette alipokuwa amelala au anaoga.

Chris Dawson alikuwa amechanganyikiwa kabisa kwa binti huyo, ambaye alitaka awe kama "mbadala" wa mke wake, kulingana na Jaji Ian Harrison.

Kwa kweli, siku tatu tu baada ya Lynette kutoweka, mwanafunzi huyo

alihamia kwa Dawsons.

Chris alidai kuwa mkewe alimpigia simu siku chache baada ya kutoweka na kumweleza kuwa anahitaji mapumziko kwenye uhusiano wao.

Aliwahakikishia kuwa Simu hiyo ya kwanza, ilifuatiwa na nyingine, lakini hii haijathibitishwa pia na hakimu anaamini kuwa ni uwongo.

Utetezi wa mume huyo pia ulidai kwamba angalau watu watano walimuona mwanamke haliyepotea akiwa hai baada ya Januari 1982.

Hili pia halikumshawishi hakimu, ambaye alchukulia kuonekana huko kama makosa ya utambuzi wa mashahidi wanaodaiwa.

Miaka miwili baada ya Lynette kutoweka, mnamo 1984, Chris Dawson na Joanne Curtis walifunga ndoa na kupata mtoto wa kike.

Wenzi hao walitengana mwaka1993.

Podcast

Uchunguzi kuhusu kutoweka kwa Lynette wa mwaka 2001 na 2003 ulihitimisha kuwa alikuwa amefariki na aliuawa na "mtu anayejulikana".

Lakini waendesha mashitaka hawakuona ushahidi wa kutosha wa kushinikiza mashtaka, hadi mwandishi wa habari Hedley Thomas alipochunguza kesi hiyo kwenye podikasti yake.

Podcast imeshiriki nafasi kubwa muhimu katika kukamatwa kwa Chris mwaka 2018 na mashtaka yalifuatia.

Jaji Harrison alimkosoa mwandishi huyo kwa “mtazamo wake usio na usawa” wa kesi hiyo na kusema kwamba ameathiri ushahidi uliotolewa na baadhi ya mashahidi.

Kwa kweli, uchunguzi uliotokana na podikasti ulisababisha kesi kuanza kwa kuchelewa.

Upande wa utetezi ulijaribu hata kusimamisha kesi hiyo kwa kusema kuwa matokeo yake yalimnyima mshtakiwa fursa ya kusikilizwa kwa haki.

Hatimaye, iliamuliwa kufanya kesi na jaji badala ya baraza la waamuzi maarufu, wakiamini kwamba mahakama hiyo ingeathiriwa zaidi na maoni ya umma.

Hukumu

Jaji Harrison alitoa uamuzi wake Jumanne baada ya kesi ya miezi mitatu iliyojumuisha ushahidi kutoka kwa mashahidi wengi.

Ijapokuwa hakuna ushahidi wowote uliokuwa na hitimisho ndani yake, baada ya kuutathmini kwa ujumla wake, hakimu aliamua kwamba Chris Dawson alikuwa na hatia.

Alitupilia mbali maelezo ya mshtakiwa kwamba Lynette Dawson aliondoka nyumbani kwake kwa hiari.

Ilikadiria kwamba mwathiriwa "aliwapenda sana watoto wake na mumewe" na kwamba vitu vyake vyote vilibaki katika nyumba ya wanandoa hao baada ya kutoweka kwake.

"Hata lenzi zake zilikutwa kwenye kontena la buluu, Dawson alipopeleka vitu vyake," alidai.

Pia, tangu Lynette alipotoweka, hakuna hata mmoja wa marafiki na familia yake aliyekuwa na habari au dalili yoyote kwamba huenda akawa hai popote.

Akichukua ushahidi wa kimazingira kwa ujumla, hakimu alisema kuwa "bila shaka" Chris alimuua mkewe na kuutupa mwili wake.

Baada ya hukumu hiyo, mhalifu alifungwa pingu na kutoka katika chumba cha mahakama huku akitikisa kichwa kwa kutoridhishwa.

Familia

Wanafamilia wa Lynette Dawson waliokuwepo mahakamani walipokea hukumu hiyo wakibubujikwa kwa machozi.

Kaka yake, Greg Simms, alisema kuwa uamuzi wa mahakama ulithibitisha tu kile walichokuwa wakijua kwa miaka.

Aliipenda familia yake na kamwe hasingeweza kuwaacha kwa hiari yake mwenyewe. Imani yake, hata hivyo, ilisalitiwa na mwanamume aliyempenda," Simms alielezea kwa waandishi wa habari, akionekana kuguswa.

Pia alimtaja Chris Dawson, ambaye alimwomba "sasa afanye kilicho sawa" na "kuturuhusu kumleta Lynette nyumbani ili apumzike kwa amani, hatimaye kumpa hadhi anayostahili."

Adhabu kamili ya mtuhumiwa huyo itajulikana hivi karibuni, katika tarehe ambayo bado haijaamuliwa.

Wakili wa Chris Dawson amedokeza kuwa kuna uwezekano atakata rufaa.
#BBC.
 
Kwenye ndoa nyingi watu wanaombea wenzi wao wafe ili waweze kuwa na watu wengine

Kwenye tendo la kuingiliana kimwili shetani ana nguvu sana na kuna muda akili huwa haifanyi kazi kabisa
 
Nimejikuta natafuta hii HABARI via Google kimshuhudia uyo Dawson na former wife wake versus current wife Joanne ....
 
Back
Top Bottom