Kikongwe wa miaka 110 aua mke kisa kunyimwa unyumba

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,464
17,292
Babu, kikongwe wa miaka 110 amekamatwa kwa kosa la kuua mke baada ya mke wake kumnyima unyumba.

====
Polisi huko katika wilaya ya Ntungamo nchini Uganda, wanamshikilia mzee mmoja mwenye umri wa miaka 110 kwa tuhuma za kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 109 kwa kosa la kumnyima unyumba.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa mkoa wa Rwizi Samson Kasasira, Mzee Dominic Babiiha anatuhumiwa kumuua mkewe Costansio Bakasisa akitumia mundu majira ya saa 1 asubuhi jumamosi huko nyumbani kwao eneo la Kahunga.

Taarifa Zaidi zinatanabaisha kwamba wazee hao ambao ni wakulima wamekua wakiishi vyuumba tofauti tangu walipooana.

Polisi wamesema mkewe alikataa kumpa tendo la ndoa sababu alikua akijisikia vibaya, ambapo licha ya hayo bibi huyo aliendelea kulazimishwa tendo hilo ambapo aliamu kwenda kulala chumba cha wajukuu zake.

Mzee huyo aliamua kuchukua mundu na kumuamuru atoke nje ya chumba, ambapo aliingia kwenye chumba hicho na kumshambulia na mundu mfululizo huku wajukuu wakikimbia nje kuomba msaada
 
Duh,
Sasa kwa miaka hiyo ya OneTen,akifungwa kifungo cha maisha atazidisha hata miaka 2 mbele ?
 
Back
Top Bottom