Baba yangu ananikwaza!

Mama yangu alikutana na baba yangu wakiwa masomoni nje ya nchi, wakapendana, wakafunga ndoa - nikazaliwa. Baada ya muda mfupi wakashindwa kuelewana -wakatengana nikiwa na miezi kadhaa na hawakuwa na mawasiliano tena, mama akaolewa na baba aliyenilea na kupata wadogo zangu. Walipoona umri unafaa, wakaniambia juu ya hilo na nikapata hamu ya kumfahamu, nikafanikiwa kumpata kupitia ndugu zake.

Nilisafiri kutoka tulipokuwa tunaishi mpaka kwake, nikafikia kwa ndugu yake ambae ndio tulikuwa na mawasiliano nae. ilipita wiki toka niwasili ndio tukaonana maana alikuwa busy hakuwa na muda wa kuja kuniona pale nilipofikia. Hakuonyesha furaha niliyoitarajia, nikarudi kwetu na hatukuwa na mawasiliano tena.

Nikiwa chuo, nilipata barua kutoka kwake, akilalamika simjali na kwamba namthamini zaidi baba aliyenilea lakini nikae nikijua kuwa yeye ndio baba yangu na sitaweza kubadili hilo. Niliumia. Baadae akaanza kunipigia simu akinitaka nimsaidie kifedha, basically mawasiliano yetu yamejengwa katika utaratibu wa kumsaidia kiasi nikiona simu yake najua kinachofuata! Nimekuwa nikimsaidia kila ninapoweza na kwa uwezo nilio nao ingawa hathamini wala kujali hicho kidogo ninachoweza kumsaidia. Bado nasoma, so anataka tugawane pesa za ufadhili!

Kwa kweli nina wakati mgumu, nashindwa kumshirikisha mama yangu sababu nitakuwa nakumbusha kilio matangani - mpaka leo bado ana hasira nae. Nimekuwa nikimsaidia kwa huruma kutokana na hali aliyonayo, amestaafu na hakujiandaa - ana maisha magumu. Lakini ananikwaza kwa jinsi anavyonilazimisha kumsaidia, ni kama vile ananidai! hana lugha ya upendo, hana subira - ananikwaza!

Naomba mawazo yenu, nifanyeje maana naona tunakoelekea sio kuzuri.
Pole sana ndugu,ila mbona hapa si sehemu sahihi?Hapa mambo ya mahusiano tu.
 
Pole sana kwa masahibu hayo. Upendo unaojengwa kwa mmoja kutoa na mwingine kupokea hauwezi kuwa upendo wa kweli. Bahati mbaya wengi tunapatwa na mambo kama haya hasa pale unapokuwa na kitu. Watu wanamthamini mwenye nacho tu. Nina uhakika kama angekuona ukiwa huna kitu hata mawasiliano yasingekuwepo kabisa. Ushauri wangu ni kuwa unaweza kufanya unachoweza, lakini u shouldn't go out of ur way to help someone who doesn't appreciate the sacrifice others are making, let alone the fact that he doesn't even deserve it!
 
Nashukuru sana kwa maoni yenu, ni kweli inaniuma sana maana mahusiano yetu ni ya mimi kutoa na yeye kupokea. Hatufahamiani, nina wasiwasi kama anakumbuka nilizaliwa lini. Kuna wakati alipata ajali akavunjika mguu. Nikagharamia matibabu yake MOI na kwa Dr. Bake, huu ndio ulikuwa mwanzo wa mfululizo wa madai (kama Fidel alivyosema). Nlipokuwa likizo nikaenda kumuona (hii ilikuwa mara ya pili mimi na yeye kuonana). Mke wake alinishukuru sana, yeye aliniambia nimnunulie suti kali kama anazovaa baba yangu ili na yeye awe kama akina Lowassa! Nilidhani anatania, baada ya hapo ikawa ni simu za kudai suti - nikamtumia 2, sasa anataka kila mwezi niwe namtumia pesa za matumizi -ukweli ananitia majaribuni maana sitaki kumuingiza mama na baba yangu kwenye tatizo ambalo walishaliepuka lakini pia naogopa hali hii ikiendelea naweza kumkosea Mungu.

..kwa maelezo haya ni kama vile namfahamu huyu mtu kwa karibu sana.
 
''Phil is my father cause the biological didn't bother'' Shaquille O'neal

Pole Annina. Nakupelekea huo mstari kutoka kwenye wimbo mmoja wa huyo mcheza basketball, na yeye baba yake mzazi alimtelekeza baadaye shaquille akaja kuwa mtu mashuhuri, baba yake mzazi akataka kujitia kimbelembele, ndiyo hapo shaquille alipoamua kutunga huo wimbo.

by the way baba yake wa kumlea anaitwa Phil ( nasema hivi ili isije ikaeleweka kuwa Shaq anamuimba kocha wake wa zamani)
 
Baba wa namna hii hata kama angekuwa biological father ni noma.Ndiyo maana unakutana na mitoto ya kinyamwezi michizi inawalipukia na "I didn't ask to be in this world"

Baba kachemsha kwa kutokuwa na contact muda wote huo, anaendelea kuchemsha kwa kudai privilege ya ubaba wakati kazi ya ubaba hajaifanya.Biological my foot, mie naona huyo baba aliyekulea ndiye baba na kama kuna mtu ana haki ya kukupiga mizinga ni yeye, kwani kadiri ulivyotueleza baba yako wa kibaiolojia alikuacha ukiwa na miezi michache.

I can hear Robert Byrd saying "Shame.....Shame..."

Hauko peke yako mazee, next time akitaka vizawadi zawadi mpelekee CD ya Shaquille O'Neal na lyrics za "Biological Didn't Bother"

Nimesoma hizi lyrics machozi yananilenga, ona Shaq aliyopitia na alipo sasa, ona baba yake alivyochemsha.

Moral of the story, vijana msiache damu zenu.



Title: Shaquille O' Neal - Biological Didn't Bother

Yo, Yo
I want to dedicated this song to Philip Arthur Harrison
Word up
cause he was the one who took me from a boy to a man
So as far as I'm concerned, he's my father cause my biological didn't bother

[Verse 1]
Biological father, left me in the cold, when a few months old
Aa father's child was greater than gold but I guess not
You brought me into the world but your not my dad
Mess around with those drugs makes my moms mad
So we left you with no remorsal pity
Took the first bus from York to Jersey City
Women and child alone now thats pressure
Moms got to go to work, drop me off by Obesa
Momma, Aunt DeDe, whoever
Aunt Falma, Uncle Roy we stuck together
A year went by and I could walk y'all
Moms got that good ol job at city hall
She probably didn't trust men anymore
Until Philip Harrison walk though the door
Went out a few times but what about Shaquille
Moms offered him a million dollar package deal
She said you want me you gotta take my son
or else its like a hot dog but without the bun
Guess what he accepted, responsibility he never left it
He kept it, he kept it
He took me from a boy to a man so Phil is my father
cause my biological didn't bother

[chorus] He took me from a boy to a man so Phil is my father
cause my biological didn't bother. (4x)

[Verse 2]
January 5th Phil made a promise (what's that)
He joined the army we moved to fort mamth
He disciplined me right from the get go
Age 2 bottle and my Mom shaquille let go
Actin spoiled, rotten, trippin
Got a butt whippin because I didn't listen
Back then you see privates made no bucks
Had to get another job driven trucks
Workin hard as hell didn't satisfy him
Had to another job working at the gym
He wasn't "Gone with the Wind" like Clark Gable
Work all them jobs to put food on the table
Phil's my father, daddy and thats the scoop
Can I go to the gym with you and shoot some hoops
Come on he put me under his wing
Was the ball boy for his little Arthur team
Sometimes he even made me mad
But it didn't matter cause I still wanted to be like dad
but a little bit better
Encouraged me to stay in school and to get then good letters
I wasn't a brainiac but I tried hard
Got to watch the Knicks play if I had a good report card
All types, all sorts
Disobeyed my dad and I couldn't play sports
I learned to dribble from right to left
I couldn't do a damn thang with all them F's
Age 15 father and son confrontation that's nothin
but father and son trials and tribulation
Back then I could under stand but I'm glad you did it
cause now I'm a man
He took me from a boy to a man so Phil is my father
cause my biological didn't bother

(chorus)

[Verse 3]
Look at me now successful for sure
Phil raised me well, to be an entrepeneur
and if your making big dope be materialistic
cause you'll end up another statistic
everything's going well following my dreams
I dunked on Patrick Ewing
I won the ring like hakeem
Uh oh what do you know
Biological ones on the Ricky Lake show
What does he want, does he want money
What people do for money!!!
It's kinda funny to me
He aint gettin no check from me (check it)
He can go on all the talk shows he want
Phil is my dad so dont even front
He took me from a boy to a man so Phil is my father
cause my biological didn't bother

(Chorus)
 
damu nzito kuliko maji my dia, fanya kile unachojisikia kufanya wewe na sio kulazimishwa!!!!
 
Hata hivyo una moyo shost mimi ningempiga chini sicheki na kima,how come alikuacha ulelewe na mama pekee?ulivomtembelea mara ya kwanza kwa nini hukufikia kwake?ukafikia kwa rafiki/ndugu yake ?achana naye hakuna laana hapo.
 
Hata hivyo una moyo shost mimi ningempiga chini sicheki na kima,how come alikuacha ulelewe na mama pekee?ulivomtembelea mara ya kwanza kwa nini hukufikia kwake?ukafikia kwa rafiki/ndugu yake ?achana naye hakuna laana hapo.

Asante Natasha, sikuweza kufikia kwake sababu sikujua atalipokeaje jambo hili yeye na familia yake. Kumbuka hatukuwahi kuwa na mawasiliano yeyote kabla, nisingeweza kwenda kwake moja kwa moja. Hata sasa siwezi, nilipoenda mara ya pili nilifikia tena kwa yule ndugu yake na kwake nilikuwa naenda na kurudi - ni ngumu sana, hata kumuita baba siwezi maana nina baba mwingine. Tatizo jingine ni kwamba haonyeshi kujutia aliyoyafanya kwangu, badala yake ananilazimisha tusahau yaliyopita na tugange yajayo ambayo ni kumsaidia yeye!
 
Annina Vipi hali ya kiuchumi ya mama na baba mlezi, ninahofu unaweza kuwasahau waliokuwesha kufika hapo ulipo na ukamjali zaidi huyo baba who has contributed nothing to your achievement.
Kimsingi unapaswa tu kumheshimu kama baba na si kama navyotaka kukutumia. Huyu baba hana upendo wadhati na wewe ndiyo maana katika wamasiliano yenu anatanguliza zaidi lawama kukutia hofu, ujione mkosefu. Ebu siku moja mulize kwa nini hakujishughulisha kukutafuta hadi baba mlezi akufahamishe? Then you will know the truth.
 
Asante Mpangwa, umesema sawa kabisa. Kiuchumi, baba na mama yangu wanaweza kujipatia mahitaji yao muhimu ikiwemo kusomesha watoto wao. Mimi bado nasoma, kimsingi bado nawategemea na sijatoka mikononi mwao. Ni kwamba nimepata ufadhili wa hii kozi, kwa kiasi fulani nikijibana naweza kubaki na balance kidogo - ndio huyu mzee anataka nijibane zaidi na zaidi na hiyo balance iwe yake!
 
Bluray,
Asante sana kwa lyrics za "Biological Didn't Bother" kutoka kwa Shaquille O'Neal - nimelia. Ameeleza yote, ingawa ni story yake binafsi lakini facts zinatugusa wengi. Ni kama vile anataka nilipie yeye kuwa biological father - shame!
 
Thanks for the lyrics Bluray. The song is very emotional, I do not know why some men forget to care for heir children, they pass on the hate and misunderstanding that they had with x-wives, or girlfriends to these innocent kids.

We should also encourage the culture of counseling. Some of these emotional wounds can be relieved by proper talking and expressing anger and pain, it may give the baba a chance to explain his stupidity.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom