Baba kanikataa kisa alitaka nisome Clinical, mimi nimeamua kusoma Computer Engineering

coockie monster

JF-Expert Member
May 2, 2015
357
669
Habari zenu wakuu?

Mimi kijana wa miaka 23,ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wa 8 baba mmoja(two wifez). Nimelelewa katika familia ya kidini sana na huku baba yangu akiwa mtu strickly, mkali, Kr perfect na no one can tell him anything.

Tangu nilipokua mdogo nilikua namuogopa sababu alikua mkali sana,anachapa sana hata kwa vitu vidogo alikua nataka tusikosee kitu chochote ukifanya ana critisize..

Sasa masaibu yameenza baada ya kufeli form 6 kutokana na uzembe wangu mwenyewe nilimdissappoint sana nikawa mtu wa mishe nyingi, bangi na sigara kwa sana(hapo alikua hajui) akawa hanipendi kwa kweli sasa baada ya kukaa mwaka mzima home nikapata chuo cha afya na yeye akawa anataka nisome hiyo afya japo mm sikuipenda sababu hobby yangu kubwa ilikua ni computer engineering .

Nilikuwa natumia vilevi hivo still nilikjifunza mambo mengi mwenyewe kuhusu computer nikanunua my own laptop nikajua baadhi ya programming language kwa juu juu (python)inshort najua mambo mengi kuhusu pc na ndo my dream carrier .

Sasa mimi kuchaguliwa course ile sikuipenda japo niliapply pia kwenye computer engineering DIT, lakini bahati mbaya baada ya deadline waliniambia nimekosea kuapply kwahiyo nikakosa(nilapply diploma form 4 marks zangu ni nzuri) nilihuzunika sana japo yeye alifurahi akijua mwanae nimepata Clinical Officer.

Kabla ya kuanza chuo nilikua na kibiashara chetu mimi na mshkaji wangu ambacho kilikua kinanipatia pesa basi baada ya kupata chuo cha afya hicho nikawa siko mortivated kabisa na kusoma hiyo coz japo najua ilikua ina heshima.

Kazi uhakika na inalipa ila it was not my dream,not the thing i wanted to do in my life nikafeli pepa za mwanzo basi ndo kabisa nikagive up na ku drop out chuo ili niapply again engineering this year bila wazee kujua.

Sasa mitihani ikaanza kunivaa baada ya mzee kujua kua mimi sipendi ile course akanimind sana akaforce mimi nimalize mwaka ndo niache kumbe maskini nishaacha kitambo na alivyokuja kujua kuwa nimeacha ndo kabisaaa akatamani kuniua .

Akaniambia i am not his son and hatokua radhi na kitu nitachosoma.

Nimejaribu kumomba msamaha lakini kakataaa na huku nimeshapata course yangu nayotaka ambayo ningejilipia ada.

Kakataa kunisamehe na anataka nisepe hapa kwa sasa michakato yangu ya pesa imefreeze,bado naishi home.

Nina stress na madeni, mambo yangu yote yamekwama,i am a loser now kilakitu changu kibaya kinaanza kureveal na anaanza kujua na inazidi kumfanya awe bitter(japo nimeacha vilevyi vyote) sina raha na maisha yangu.

Yes najua nimefuck up my life, dissapoint my family and friends nimeharibu everything, nobody trust me, suicidal thoughts zimenijaa but i cant do it i want to move very far nianze upya kwa hapa naona siwezi kuanza upya, sababu my bad past is still around here on my family hawatoniamini tena.

Mi nataka nihame mkoa niende hata mkoa mwingine(nipo dar now) ambao sijulikani nistart again maisha yangu na kuwa mpya, mchamungu na mchapa kazi.

Mimi na upeo mzuri tu na najua vitu vingi tu sababu ya exposure yangu, but now i lost everything am just me i need a new life very far.

Wakuu nilikua naomba tu ushauri wenu na experience zenu i really need it.

Please najua mi mzembe, mjinga, mpumbavu, sijielewi yote hayo nishaambiwa haina haja ya kuniambia tena utazidisha machungu.
 
Pole........

Ila wazee wa kiafrika kwa kupangia watoto kazi na watoto wwngine kwa ujeuri...

Kuteleza si kuanguka jipange uanze upya
 
Mama yako anasemaje, UPI ni msimamo wake?

Ingekuwa Mimi ningeondoka tu home, kwa sababu hata nikiishi hapo nitakuwa stressed mara dufu.

Usiogope laana kwa sababu hata sasa baba yako ameshakukana, hakuna balaa utakalopata maadam dhamira yako ni safi.

Ondoka home, tafuta maisha, kama shule utarudi tu. Wakiona umekaa sawa watajirudi tu.

Good luck
 
I have been in shit too.umenikumbusha mbali sana..just move on man
 
Watu wenye exposure hawako hivo dogo, unawaza kujitundika umekua mhehe wewe?
 
Mama yako anasemaje, UPI ni msimamo wake?

Ingekuwa Mimi ningeondoka tu home, kwa sababu hata nikiishi hapo nitakuwa stressed mara dufu.

Usiogope laana kwa sababu hata sasa baba yako ameshakukana, hakuna balaa utakalopata maadam dhamira yako ni safi.

Ondoka home, tafuta maisha, kama shule utarudi tu. Wakiona umekaa sawa watajirudi tu.

Good luck

naishi kwa stress sana,usikua silali,mchana sishindi home na kaasababu bado nataka kusoma naamini ntasoma
 
Kwanza punguza ujuaji kijana, pili badilisha heading ya uzi na uiweke kwa lugha ya kiswahili sababu umeanza kwa kutumia lugha iliyo letwa na majahazi, na bila shaka washauri wazuri wanapita pasipo kuingia na wasome yanayo kusibu (peginene ukapata msaada).
 
yah im moving on,niambie ulisurvive vp?

Niliamua kwenda kahama nikapanga chumba kwa elfu 10 kwa mwezi hakikuwa na umeme wala maji na sikuwa na pesa kabisa,kula na bangaiza nikikosa nalala njaa.. but mungu alinisaidia baada ya kuteseka kwa muda mrefu nikapata kazi mgodi wa buzwagi maisha yakaendelea.dont give up nilipitia maisha magumu sana trust me niki move on nw naishi kwangu na nina familia
 
Kama mzee pamoja na jamii ilio kuzunguka haina imani na wewe, unadhani huko mbali utaaminiwa na nani?
Nakushauri uanze na kurudisha imani hapo nyumbani, kwa baba, pamoja na jamii ilio kuzunguka. Hii itawafanya mzee arudishe moyo kama baba na hasa atakapo ona umebadilika kitabia na ukimcha mungu.
Tafuta kibarua chochote halali kinacho weza kukupatia kipato, na usitishwe na maneno ya mzee, kwani yeye anapatwa jazba kwa maumivu ya kutumia pesazake nyingi kwaajili ya kukutengeneza maisha alafu ukaharibu. Pia anauchungu kama mzazi ndiomaana anafikia hatua ya kukusemea maneno makali, ingawa bado naamini anayo mapenzi na wewe ndiomaana anakarisika.
 
i have been through hell myself Young man.. so i know exactly how you feel. kukimbia home ndio matatizo yataongezeka kama huna pa kwenda. just chill, ila nataka nikupe moyo tu kwamba TIME HEALS EVERYTHING hayo matatizo yako yape muda kidogo tu, Mungu atafungua njia.
 
usione umepitia dogo kila mtu akiandika yake hapa mbona utajiona una nafuu kubwa tu tafuta ada urudie form 6 mbali na home kwa mwaka mmoja as qt maana uwez fanya tena mtian kwa umri huo necta hawatak labda ufanya
as private ukifaulu ukapata kulipiwa eng chuo ucrud home tena had upate kazi
 
Kama mzee pamoja na jamii ilio kuzunguka haina imani na wewe, unadhani huko mbali utaaminiwa na nani?
Nakushauri uanze na kurudisha imani hapo nyumbani, kwa baba, pamoja na jamii ilio kuzunguka. Hii itawafanya mzee arudishe moyo kama baba na hasa atakapo ona umebadilika kitabia na ukimcha mungu.
Tafuta kibarua chochote halali kinacho weza kukupatia kipato, na usitishwe na maneno ya mzee, kwani yeye anapatwa jazba kwa maumivu ya kutumia pesazake nyingi kwaajili ya kukutengeneza maisha alafu ukaharibu. Pia anauchungu kama mzazi ndiomaana anafikia hatua ya kukusemea maneno makali, ingawa bado naamini anayo mapenzi na wewe ndiomaana anakarisika.

asante sana kwa ushauri,ila mbona nishabadilika ila anaona kama namuektia pia..
 
Niliamua kwenda kahama nikapanga chumba kwa elfu 10 kwa mwezi hakikuwa na umeme wala maji na sikuwa na pesa kabisa,kula na bangaiza nikikosa nalala njaa.. but mungu alinisaidia baada ya kuteseka kwa muda mrefu nikapata kazi mgodi wa buzwagi maisha yakaendelea.dont give up nilipitia maisha magumu sana trust me niki move on nw naishi kwangu na nina familia

duh im ready for life consequencess,najua ni ngumu ila its my only choice
 
Kwanza punguza ujuaji kijana, pili badilisha heading ya uzi na uiweke kwa lugha ya kiswahili sababu umeanza kwa kutumia lugha iliyo letwa na majahazi, na bila shaka washauri wazuri wanapita pasipo kuingia na wasome yanayo kusibu (peginene ukapata msaada).

sawa mkuu,sio ujuaji nimefunguka kila kitu ila wewe ndio umetafsiri ujuaji
 
i have been through hell myself Young man.. so i know exactly how you feel. kukimbia home ndio matatizo yataongezeka kama huna pa kwenda. just chill, ila nataka nikupe moyo tu kwamba TIME HEALS EVERYTHING hayo matatizo yako yape muda kidogo tu, Mungu atafungua njia.

ni kweli,ila kama sasa iv naishi kama paka na panya na wazee,nazidi kupata stress,ndugu wote wananiona nimewadisappoint washaniona loser,wadogo zangu washanidharau hivi unaweza ukaishi eneo hilo kwa mda tena hata ukibadilika?its very hard ila let see
 
Back
Top Bottom