NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Kuna huu utaratibu mtu anakuja kukuomba ajishikize site kwenye kiwanja chako na wengi wao huwa wanapewa ulinzi wa kumuangaliza mwenye nyumba pale inapojengwa ama kumlindia kabla hajahamia.
Kisa cha kwanza: Kuna sehemu walipewa nyumba watu wamekaa mpaka wamezaa watoto wakubwa kabisa wa kwanza kamaliza anaingia darasa la saba mwakani, mwenye nyumba hakuwahi kuja kama miaka mingi mpaka watu walizani nyumba ni ya kwao hao waliopewa waiangalie, juzi juzi yule mwenye nyumba kaja na mjomba wake ambae kasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatoa hadi watu wakashangaa aliejenga alikuwa wapi miaka yote.
Kisa cha pili: Kuna jamaa alihamia kwenye nyumba yake haina choo ila Kuna jirani yake alikuwa kajenga nyumba ina choo ila bado hakuhamia, jamaa yule asie na choo alimuomba jirani ambae hakuhamia atumie choo chake na akaruhusiwa bila kinyongo, Ila sasa baada ya muda yule jirani alihamia kwake, yule jamaa bado hajajenga choo kwahio wanatumia choo wote, Sasa jirani akapata pesa akajenga fensi, yaani yule jamaa alimnunia sana mwenzake, yaani Kuna visa vingi vilipita, nilijifunza kitu.