Tetesi: Baadhi ya viongozi kuwekewa vikwazo vya kusafiri kwenda Ulaya na Marekani

Aisee wakuu hali ni mbaya,

Nimeona habari katika chanzo kimoja cha kimataifa, ni kuwa kuna hatari ya kuwekewa vikwazo vya kusafiri kwenda ulaya na marekani kwa viongozi fulani kutoka Tanzania.

Inasemekana vikwazo vinaweza kuwakumba, Paul Makonda, msajili wa vyama vya siasa, na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali.

Aisee hali ni mbaya

Source. Fox news.
Mbona mnakuza mambo wakati hayako hivyo
 
Aisee wakuu hali ni mbaya,

Nimeona habari katika chanzo kimoja cha kimataifa, ni kuwa kuna hatari ya kuwekewa vikwazo vya kusafiri kwenda ulaya na marekani kwa viongozi fulani kutoka Tanzania.

Inasemekana vikwazo vinaweza kuwakumba, Paul Makonda, msajili wa vyama vya siasa, na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali.

Aisee hali ni mbaya

Source. Fox news.
Kwani nani anataka kwenda marekani makonda afate nn marekani? Jpm mwenyewe hajawahi kwenda hata kwa mwaliko wao huwa haendi.
 
Nimeona habari katika chanzo kimoja cha kimataifa, ni kuwa kuna hatari ya kuwekewa vikwazo vya kusafiri kwenda ulaya na marekani kwa viongozi fulani kutoka Tanzania.
Kwani ni kiongozi gani wa awamu ya tano aliekwenda huko zaidi ya Mahiga?
waweke tu vikwazo,hatuna shida ya kwenda huko
 
Aisee wakuu hali ni mbaya,

Nimeona habari katika chanzo kimoja cha kimataifa, ni kuwa kuna hatari ya kuwekewa vikwazo vya kusafiri kwenda ulaya na marekani kwa viongozi fulani kutoka Tanzania.

Inasemekana vikwazo vinaweza kuwakumba, Paul Makonda, msajili wa vyama vya siasa, na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali.

Aisee hali ni mbaya

Source. Fox news.
Jwa hao, hata kama US/EU wakiazimia wakamatwe au watekwe na kwenda kuhukumiwa kwenye mahakama za Marekani kama alivyofanyiwa yule Rais mfanyabiashara ya madawa ya kulevya, Noriega, litakuwa ni jambo jema sana.

Wasituwekee vikwazo vya kibiashara, ambavyo kwa vyovyote vitawaumiza wanaodhani wanataka kuwatetea.

Kuna mpango wa US wa siku za nyuma wa kutaka US iwe na uwezo wa kumwua kiongozi yeyote muuaji Duniani bila ya kuleta madhara kwa wananchi, sijui uliishia wapi. Mpango ule ungefanikiwa, na utekelezaji wake ungekuwa unafanyiwa tathmini ya haki, ukipunguza au hata kufuta kabisa udikteta.

Haya maneno ya kusema nchi huru isiingiliwe, wakati watu wanauawa au kugandamizwa na watawala, siyo haki.

Umoja wa Mataifa ni vema ungekuwa na azimio la kuwa na utaratibu wa kuwaondoa watawala madikteta Duniani pale inapothibitika bila shaka kuwa mtawala ni dikteta.

Hii ya kusema kuwa hata ukimwona jirani yako anawaua wanawe, halafu unasema siwezi kuingilia kwa sababu wale ni wanawe au kwa sababu anawaulia nyumbani kwake, ni kuepuka kuwajibika kwa Dunia dhidi ya dhuluma ya nafsi za binadamu.
 
Kama umefuatilia news za wenzetu siku mbili hizi utakuwa umekutana na news kuwa Marekani inaanza kupambana rasmi na ukuwaji wa uchumi na influence wa nchi ya China na Russia Africa.

Kwa hiyo, hawa jamaa wakiweka vikwazo Tanzania, wala siyo kwa faida yetu au kwa kutusaidia. Lengo lao kubwa ni kuibana China na Russia kwenye nchi za Africa.

Sisi huku tutapiga makofi na kuwashukuru wakati mzee Trump hana time na wewe kabisaa, lengo ni kuiangusha China na Russia.

Wapiganapo fahari wawili... Ziumiazo nyasi... Endeleeni kuwapigia wazungu makofi.

Chanzo cha habari ni BBC, Aljazeera na Reuters

U.S. to counter China, Russia influence in Africa: Bolton | Reuters
Wewe unauwezo mkubwa sana wa kuona. Hiyo issue ndio ina trend huko kwa sasa. Na sio kuhusu Tanzania tu. Sababu sisi huku tunapelekwa na lundo la ujinga tunadhani Wamarekani wanakaa vikao kujadili visa za akina Makonda. Ukisoma hapo juu, utaona huruma sana.
 
Democrasia umekuwa nayo miaka mingi na hujaeta maendeleo.. bado masikini.. Leo tunainua uchumi wetu na kukemea vitendo vya wizi .. wewe unakaa tu kusemea wanaume wa ulaya .. Eti Domokorosia... Mtu ushinde unapiga porojo bila kufanya kazi kisa democrasia..
Magufuli akiacha kusigina katiba eventually mambo yatakaa vizuri tu, lakini kwa njia aliyoichagua atapata tabu sana.

Pressure is slowly building up on him, diesel imemwagwa shimoni taratibu nyoka na kenge wataanza kutafuta pa kutokea. something will happen. Hata kama si leo au kesho.
 
Umasikini unakusumbua. Umekosa michongo ya hela unaona bora umwage ugali wote wakose ikiwemo vita.

Nimefanya kazi na makampuni binafsi ambapo nimeweza kusafiri kwenye nchi kama Sudan na Somalia.

Ombea vitu vyote, kasoro vita aisee. Hiyo kitu acha kabisaa.

Hata mimi nilikuwa naogopa vita sana, ila kwa tulikofikia hapana aisee, waje tu wakinukishe jiwe litoke, hivi huoni jinsi lilivyoharibu nchi yetu pendwa?
 
Wazungu wakati mwengine kama matahira flani ivi. Wanaona kwenda ulaya ni deal. Walitaka nchi hii iwe na kiongozi mkuu mtembeza bakuli ulaya. Eti kuwekewa vikwazo kwenda ulaya!!! Kicheko .com

Mpaka na watu kama nyie mpate akili na usukule uwatoke
 
Hata mimi nilikuwa naogopa vita sana, ila kwa tulikofikia hapana aisee, waje tu wakinukishe jiwe litoke, hivi huoni jinsi lilivyoharibu nchi yetu pendwa?
Walitaka Assad atoke, mpaka leo anadunda na matokeo yake wana crisis ya wakimbizi waliowasababishia wao.
 
Back
Top Bottom