Baada ya wimbo wa "Wanatuona Manyani" kufungiwa, mwingine ajitoa muhanga na "Joka la Kijani"

Humo ndani msanii Chief Son anasema namnukuu kwa uchache, Tanzania sio maskini tatizo ni joka la kijani. Joka la kijani linazidi kutuvutia shimoni, joka la kijani linazidi kututia umaskini, joka la kijani tunapaswa kulitoa madarakani.
Hii itaanza kuwatafuna hao watoto walioshika mabango
 
Baada ya wimbo wakuitwa "Wanatuona Manyani" kufungiwa na mwimbaji kuwekwa ndani, sasa kuna msanii mwingine anaeitwa Chief Son kajitoa muhanga na wimbo wakuitwa "Joka la Kijani".

Humo ndani msanii Chief Son anasema namnukuu kwa uchache, Tanzania sio maskini tatizo ni joka la kijani. Joka la kijani linazidi kutuvutia shimoni, joka la kijani linazidi kututia umaskini, joka la kijani tunapaswa kulitoa madarakani.

Zaidi unaweza kutazama wimbo huo hapo chini.

Nice song
 
Joka la kijani... kichwa Kiko bandarini.... mkia uko magogoni!!!

Sijui tunaanzaje kuliua hili Joka!!!?
2025
images (13).jpeg
 
Huenda kuna kizazi kipya cha wasanii wenye akili kinakuja baada ya kile cha wenye kujikomba kwa watawala.
Waimba amapiano na singeli
Wavaa Heleni puani vikuku mguuni
Walamba lips

Ova
 
HIi imeenda.
Akitoa na mwingine na mwingine sijui watakamata wangapi
 
Huenda kuna kizazi kipya cha wasanii wenye akili kinakuja baada ya kile cha wenye kujikomba kwa watawala.
Kimeanza kuonekana Kwa mbali. Na hii ni 2023 mpaka 2025 tutakuwa na nyingi zinazohamasisha Uzalendo badala ya ngono zembe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom