SoC03 Baada ya miaka 19 nje haya sijayapenda Tanzania tuchukue hatua

Stories of Change - 2023 Competition

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,507
Niliondoka miaka ya 2004 Tanzania kwenda kutafuta Maisha huko Ulaya, Marekani na Asia ambako nimekaa kwa kipindi hicho chote. Niliondoka Tanzania nikiwa naishi Arusha.

Niliacha nchi ikiwa isha anza kupiga hatua kadhaa za kimaendeleo, ingawa sio kama ilivyo sasa hasa ukitilia maanani sayansi inavyo kuwa kwa kasi ya kutisha sana Ulimwenguni kote. Sitapenda kuongelea maendeleo kwa sababu maendeleo yapo ila nitaongelea mapungufu yote ninayo yaona na yanayo hitaji jitihada za dharura kalba hali haijawa mbaya sana;

Nilirudi Tanzania kupitia Uwanja wa KIA kwa shirila la ndege La KLM na tuliingia mida ya saa 2 usiku, wakati ndege inatafuta uelekea tylipita jiji la Arusha kwa kweli zile taa usiku zilinihamasisha na kuiona ule mji kama miji mingie tu huko Duniani,.

Baada ya mapumziko Arusha nilitembelea maeneo yafuatayo Kilimanjaro, Tanga, Bagamoyo, Dar es salaam, Manyara, Mara, Mwanza, Kigoma, Tabora na Singida. Huko kote haya ndio mambo nayaona ya hatari kwa Taifa hili pendwa;

Kasi ya kutisha ya kuharibu mazingira; Kiwango nilicho kishuhudia kote huko cha kuharibu mazingira kinatisha sana,mazingira yanaharibiwa sana na ni kama hakuna wa kusikitika au kulia,nilianza kuona Arusha jinsi mazingira ya awali yalivyo haribiwa, Migomba haipo tena Arusha, Kahawa hazipo tena Arusha,hali niliikuta pia Kilimanjaro,Moshi, Mlima Kilimanjaro barafu imekata kabisa,nimeona hali Tanga, Bagamoyo ilikuwa pori zuri ila kila mtu anafyeka na kujenga au kulima,hali iko hivyo Mwanza, Mara, Kigoma na kwingineko, Mikaa na kuni ni biashara kubwa sana, nilimtembelea rafiki yangu anaye fanya kazi Idara za mazingira nikakuta nyumbani kwake amejaza mikaa na kuni za kupikia huyo ni mlinzi wa mazingira, nilikutana na gari za Serikali zimebeba mikaa juu ya keria, Serikali ndio mtunza mazingira mkuu ila anapo geuka kuwa wakala wa kuharibu mazingira inasikitisha sana.Wanasiasa kitu ambacho hawana muda wa kukizungumzia ni mazingira.

Nilishindwa kupata eneo maalumu la makazi kote niliko fika; Nilifikia eneo la Sakina mwenyeji wangu akanimbia huku ni makazi, ila sikulala vizuri usiku huo kwa sababu kuna kiwanda mita kama 70 kutoka nilipo fikia wanafyatua tofali usiku na mchana na nazania pia walikuwa wana fidia mgao wa umeme, Kesho yake nikaenda kwa rafiki yangu mwingine eneo la njiro nako panaitwa eneo la makazi ila nikakutana na night club hatua chache na anapo kaa rafi yangu, nilochoka sana, nika tembelea eneo la Uzunguni zamani zile ilikuwa ni eneo tulivu sana ila nilishangaa kukuta kwa sasa kuna mahoteli eneo lile, Dar salaam hali ni ile ile, Moshi kote kule shant town, Mwanza, Kwa kuhitimisha kote niliko pita sikukutana na eneo maalumu la mkazi kote huko ni mchanganyiko wa Makazi, Baa, Maduka, Viwanda, Night club, Makanisana na misikiti, Je watwala wapo kweli haya yakitokea?

Sikuiona Tanzania ya Viwannda inayo hubiriwa; Eneo la kuiona Tanzania ya viwanda ni Kariakoo nimefika nikakuta asilimia 99 ya bidhaa zinazo uzwa pale ni kutoka nje hasa China, India, Uturuki, na Ulaya, Kariakoo ndio kioa cha Tanzania ya viwanda kama tulikuwa hatujui, sasa pata picha ya pale, Ukienda Mumbai India utakutana na picha ya India ya Viwanda, Ukifika Instambul Uturuki utapata picha, Bangkok Thailand kule ndio kioo cha Thailand ya Viwanda, sasa kama kuna eneo jingine labda sikufika ambalo ukifika unaiona Tanzania ya Viwanda naomba nijulishwe, ila niliko fika kote sikuiona Tanzania ya Viwanda, Je watawala wana tuhadaa?

Kukutana na Mikusanyiko ya watu wasio kuwa na kazi za kufanya saa 2 asubuhi;Nikiwa Dar es salaam ilitokea ajari la lori liliingia mtaraoni na kupinduka, nilishangaa kukuta umati mkubwa kabisa wa watu nikataka kujua kama ni kikosi cha uokoaji, ila nikaambiwa hao ni watazamaji, nikuliza mbona ni saa 2 asubuhi au hawa wametoka shift ya usiku? Nikaambiwa hapana bali hali ndio iko hivyo, nilikuja kuamini baada tena ya kuja kukutana na ajari mwanza mida ya saa 6 na umati pia ukiwa mkubwa kuliko hata ule wa Dar. Watanzania wenzangu mambo mengine Serikali inatwishiwa lawama bure kwamba kweli hatuna kabisa kabisa cha kufanya tukiamka? Hata kama ajira ni ngumu ndio iwe hivyo sasa? Hatuna namna ya kuupatia muda wetu thamani?

Maongezi ya Vijana asilimia kubwa ni mpira wa Yanga na Simba, ligi za Ulaya, kidogo story za habari za matajiri wa Tanzania, siasa na habari za wasanii, mpaka naondoka sikikuta sehemu watu wakijadili Maisha yao, hali ya Uchumi wan chi, haki zao kama raia. Habri zote ni zile zisizo kuwa na thamani kwao na kwa nchi yenyewe.Sio bure Watanzania wenzangu wanapandishwa basi wakikaa sit za nyuma basi ikifikakwenye mizani wnaambiwa watoke nyuma waende kuchuchumaa katikati ya basin a wao kweli wanatii, kwa maonegezi kama yale ya vijiweni ni lazima watii makondakita wa mabasi.

Kasi ya kubadili aridhi ya Kilimo kuwa makazi; Hili nililiona Arusha, Mashamba ya kahawa kwa sasa ni nyumba, Migomba imefykwa zimejengwa nyumba, Karatu mashamba ya ngano kwa sasa ni nyumba za watu kuishi, Babati kote huko, Bagamoyo ile baada ya muda itakuwa ni nyumba tupu, Mwnaza kasi ya kubadili majaruba kuwa viwanja ni kasi ya kutisha kabisa. Ndugu zangu New York ina miaka si chini ya 500 tangu ianzishwe, Ila ina mashamba. Tusicheze na food security, hii itakuja kutugharimu sana, lazima tuchore mistari kati ya maeneo ya mashamba na makazi. Mashamba yalindwe kwa gharama zozote zile.

Tatizo la ajira bado watawala wanalichukulia kawaida sana; nilikutana na ndugu zangu wengi walio maliza vyuo vikuu wakiwa mtaani bila kazi, na wote hao nikiongea nao lawama ni kwa Serikali, na ni kweli lazima Serikali ibebe lawama kwa sababu ndio jukumu lao kuhakikisha raia wana ajira, Serikali haina majibu ya uhakikia, haina mikakati, hili swala la ajira baadae litafikia kiwango ambacho hakiwezi dhibitiwa tena na hapa ndio Serikali itajilaumu sana na muda hautakuwa upande wao tena . Ukosefu wa jaira unapaswa kuwakosesha usingizi viongozi, ila sina uhakika kwa Tanzania kama viongozi wanakosa usingizi kiasa vijana hawana ajira.

Slums zinakuwa kwa kasi sana Tanzania; Nilifika Arusha eneo la kwa mrombo kule ni eneo jipa la Slums yaani Modern Slums, Mwaza hali ndio mbaya kabisa, Unakutana na wauza kiwanja wanapima kiwanja cha 10x15 hii ni slums.

Haya na mengine mengi ni maswala ambayo kama Taifa lazima tuyafanyie kazi, tyupunguze siasa, kuna siasa sana nchi hi kwa kila jambo, Mmabo ya Mazingira siasa, Ajira siasa, Mpiango miji siasa, Kilimo siasa.
 
Back
Top Bottom