Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Kama wewe si mshabiki wa upinzani basi ni shabiki wa CCM, na kama ni hivyo basi ingeshangaza sana kama na wewe ungeona kwamba upinzani unafaa kutoa Rais iwe 2020 ama hiyo 2025. Mbali na U-CCM wako lakini pia kwa Makonda na Magufuli umepata sababu za ziada za kuwashabikia na siku hizi huoni haya kwa hilo!

Kama mpaka mwaka 2025 unaona ni CCM tu ndiyo inafaa kutoa Rais basi kuna tatizo, na tatizo la ziada ni pale unapoona anayefaa kugombea huo urais wenyewe. Hili na upinzani kuwa bado sana kwenye nafasi ya Urais ni kwa vigezo vya sayansi ya siasa ama ni kwa mtindo wenu wa kutumia kila zana haramu kuhalalisha ushindi wenu?

Toa sababu ni kwa nini Upinzani haujawa tayari kutoa Rais?
Sioni mtu wa kuongoza nchi kwenye upinzani , Mbowe ? Lissu ? Sugu ? Halima Mdee , Msigwa ? Waliomo Ukawa hata kiganja hawajai , mawaziri utachagua wapi ,
 
Lowasa hagombei tena 2020?Na je bado ana nguvu kisiasa?Jibu ni fupi-Hapana hana nguvu tena za kuua Simba.Simba ni mkali...eeh eeh aliua baba eh eh eh akaua mama...eh eeh eeh.
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Leo nimemsikiliza huyu jamaa kwa makini, jamani uwongo tuweke Pembeni, ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza, kama hatutabadili kumuongezea Magufuli miaka 10 mingine baada ya 2025, then huyu jamaa atatufaa sana.

Sitanii.

Paskali
 
Tanzania mara ya kwanza huenda tukawa na rais huyu kwa muhula mmoja tu - jinsi wakulima wanavyoisoma namba, jinsi watumishi wa umma wanavyoandamwa, jinsi madereva (Magari na pikipiki) wanavyonyanyaswa - napata shida kidogo kufahamu future ya CCM yetu.

Takwimu: Mwaka 2015 CCM kura 8milioni , CDM kura 6milioni - lkn uchaguzi wa mwaka 2020 tuna ongezeko la vijana takribani 5,550,497 watakaokuwa na sifa ya kupiga kura.

Sasa jiulize vijana hao ni rahisi wakawa upande wetu???
 
Leo nimemsikiliza huyu jamaa kwa makini, jamani uwongo tuweke Pembeni, ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza, kama hatutabadili kumuongezea Magufuli miaka 10 mingine baada ya 2025, then huyu jamaa atatufaa sana.

Sitanii.

Paskali
Paskali kwani kwa kipindi hicho kijacho after Jpm taifa litakua linamhitaji mtu anayejua 'kujieleza' kulikotukuka kama unavyomnadi jamaa Bashite??
 
Leo nimemsikiliza huyu jamaa kwa makini, jamani uwongo tuweke Pembeni, ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza, kama hatutabadili kumuongezea Magufuli miaka 10 mingine baada ya 2025, then huyu jamaa atatufaa sana.

Sitanii.

Paskali
Mkuu umepima akili zetu na kutuona hamnazo sawa na Bashite na Sizonje?
 
Haaa haaaa Uwiiiiiii t-e-e te-e-e Paskali Mayali huyu huyu au? ha ha ha . Hivi, how dare you!! Mwanataaluma kama wewe eti
"Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, ------- bla bla blaaaaaaa"
..ck da-ya sss
:oops::oops:
 
Paskali kwa nyuzi hizi iko namna kuna mtu unamkwepa kiaina baada ya kumtupia bomu la mkono kwenye mkutano pale nyumba nyeupe. Pamoja na hayo bado anakunyatia kimya kimya hivyo kila hatua moja mbele geuka nyuma mara mbili..!!
anachofanya mayala ni kuomba msamaha indirect hahahahaha au la alishaitwa baada ya ule mkutano akaminywa sehemu akaambiwa chunga sana !!!!!!!!!!!!!huko nyuma hakuwa hivi paskali
 
Back
Top Bottom