Meaning?
Mkuu Mbase, nimeguswa sana na michango yako, haswa kwa objectivity yako kutanguliza mbele maslahi ya taifa na sio maslahi ya vyama.Nimekuelewa mtani wangu, ndicho hua nakisema hapa kila siku,unakumbuka mwaka ule tulipokuwa na mkutano pale Diamond Jubilee? kama ulikuwepo lengo la kikao kile kilikuwa kuandaa jukwaa la kudai katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa vyama vingi, na pia kuomba serikali ya mpito kuelekea katika mfumo wa vyama vingi wakati tunaandikia katiba mpya na ndipo NCCR ikaanzishwa. Lakini jamaa tuliowaamini wakaibadilisha NCCR kutoka jukwaa la kudai katiba mpya mpaka chama cha siasa. Hapo ndiyo hasira yangu inapokuja kwa hawa wapinzani maana walichokifanya ni kukimbilia Ikulu. Waliponikatisha tamaa NCCR nikaanza kuwa mfuasi wa Mtikilia nikiamini kama ataungwa mkono na wanasiasa wenzake wa upinzani katika kesi alizozifungua za kikatiba. Lakini leo siamini macho yangu hawa wapinzani wanaposema wameibiwa kura najiuliza nani kawaibia? Tangu lini Tanzania iliachana na chama kimoja? hawakujua kama katiba iliyopo ilikua ya chama kimoja na hivyo tume ya uchaguzi haiwezekani kuwa huru??? Hapa JF nilitegemea kua kuna ma GT kama tunavyotaka kuaminishwa lakini naona kuna wengi ama ni mbumbumbu kwa maana hawajui mageuzi yalianzaje ama vichwani ni weupe kwa maana hawatumii akili zao walizopewa na Mungu.
Watu kama kina Sumaye, Lowasa, Ulimwengu, Kingunge, Seif, Duni hawa wote ni mazao ya chuo cha siasa kivukoni. Hiki chuo kazi yake moja ilikua kuwaandaa makada wa CCM, Leo hii hawa makada ndiyo wanaitwa makamanda wa UKAWA. Hawa makada wa CCM wanasema tumerudi nyuma miaka 50, halafu hatuwaulizi nani ameturudisha huko nyuma na walikua wapi kuona hizo juhudi za kuturudisha nyuma??
Vijana wa kizazi kipya ndiyo kina Sugu, Nape, Lissu, Zitto, Kibajaji, na wengine wengi je Mayalla unaona kama kuna yeyote hapo ana hata 50% ya uwezo wa Mapalala ama Fundikira walioshindana na mtu muelevu kuliko hawa tulionao leo Mwl Nyerere?? Hawa vijana wamejawa na unafiki na mambo yale yale yaliyotufikisha hapa tulipo ya ZIDUMU FIKRA AMA ZA MAGUFULI, SEIF, LIPUMBA AU MBOWE. Safari ni ndefu sana kama wananchi tuna akili hizi ninazozisoma humu JF. Nilijiunga kwa mara ya kwanza na JF ilipoanzishwa lakini nikachana nayo maana majadiliano yetu huwa partisan zaidi badala ya kuwa bipartisan.
Partisan ni kama hawa wanaoitana nyumbu na book saba, hili ni kundi ambalo linajadili maswali ki itikadi zaidi hata kama hayana maslahi kwa Taifa, Sera za bipartisan ni pale watu wanapoondoa uchama na kuchangia kwa maslahi ya Taifa. nadhani nimeeleweka hapo mkuu Mayalla Maana rahisi kabisa ni kuungana ama kukubaliana katika sera kwa vyama ambavyo hutofautiana kisera. Mfano CHADEMA walikuja na sera za kupinga ufisadi kabla ya uchaguzi mkuu hivyo sera kama hii CCM walitakiwa kukubaliana na CHADEMA hii ndiyo bipartisan.. nadhani nimeeleweka mkuu PaskalMkuu Mbase, nimeguswa sana na michango yako, haswa kwa objectivity yako kutanguliza mbele maslahi ya taifa na sio maslahi ya vyama.
By neno bipartisan unamaanisha nini? .
Thanks
Paskali
NI ZAMU YA RAISI MUISLAMU; PUNGUZA MAPENZI PASCO
Utaratibu wetu ni kupokezana
Najua itakuwa zamu ya waislamu
Labda mumshauri abadili dini
View attachment 476Anatufaa Kivipii kwamfano