Baada ya kutoswa, Sumaye sasa ateta na viongozi wa CHADEMA

Hayo magamba sijui sumaye,el,chenge,mambe,sita ,siku wakitinga cdm tu kadi yangu ya cdm naipiga kibiriti na kachana na mambo ya siasa
 
Dah watu wanaitafuta IKULU kama LULU kunani IKULU Watu wenye tamaa za madaraka kama hawa hawahtajik ndani ya Chama makini CDM,Peopleeeeeeeeees
 
Mh Sumuaye katumwa kupunguza nguvu ya cdm, agombee kupunguza kasi ya dk slaa na pia ahusike kutengeneza migogoro ya ndani ya chama cdm. i would suggest asipewe hata kadi.
 
Mimi naungana na wengine kumtaka Sumaye ajiunge CDM sababu alikua PM hivyo ana watu walionyuma yake ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa kukiendeleza CDM ila hawezi kupewa agombee Urais sababu CDM hakina hulka ya kutoa hisani bali kwa mujibu wa kanuni na taratibu ila asipewe kugombea maana hatashinda na itakuwa mtaji mkubwa kwa CCM
 
Sumaye? Ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa, ikiwemo CDM, lakini kama mwanachama, na hakuna haja ya high profle discussions naye, hana impact. A spent force that was never useful anyway.....
 
Nimeshangaa kusoma eti Sumaye aihitaji CHADEMA bali CHADEMA ndiyo wanamuhitaji..... Mtu wa namna hii akishaanza kuonyesha dharau sidhani will do good for chama as taasisi. Yeye anaweza kuendeleza Masters yake ya Harvard sehemu zingine si lazima CHADEMA kama akiwa na hicho kiburi.

Kuna vyama kama SAU or CHAUMA wanahitaji viongozi wa kitaifa, bado hajachelewa ingawa sina hakika wanahitaji viongozi wenye viburi,.....he can still try.
 
sumaye ni chadema kitambo kila mtu anajua hilo,....by the way chadema= ccm remix
 
  • Thanks
Reactions: Ame


Thursday, 04 October 2012 21:23

NI KUHUSU MUSTAKABALI WAKE KISIASA

Mussa Juma, Arusha na Boniface Meena, Dar

SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648.

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa.

Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema. Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka.

Alisema mawasiliano ya Chadema na Sumaye yalianza mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Septemba 30, mwaka huu yaliyomwengua kigogo huyo kwenye kinyang'anyiro hicho.

"Ni kweli kuna watu wa CCM tumewasiliana nao baada ya uchaguzi ule (wa Nec) na Sumaye tunawasiliana naye pia lakini siwezi kusema tumefikia wapi," alisema mjumbe huyo na kuendelea: "Suala kwamba amekubaliwa kujiunga na Chadema au la, nadhani huu ni uamuzi wake. Ninachoweza kusema ni kwamba vikao vilikuwepo na vinaendelea kukaliwa."

Alisema baada ya matokeo ya Hanang' na hali ya kisiasa ndani ya CCM, Chadema kimekuwa kikiwasiliana na Sumaye na kikubwa ambacho kinajionyesha ni kada huyo wa CCM kutoridhishwa na hali ya mambo ndani ya chama chake.

Mjumbe huyo wa Chadema alisema chama hicho Wilaya ya Hanang' kinaandaa mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya wa CCM, wengi wao wakiwa baadhi ya walioanguka kwenye uchaguzi wa Nec wilayani humo.

Habari zaidi zimeeleza kuwa Chadema kimepanga siku yoyote juma lijalo, kuwapokea wanachama wapya kutoka CCM, baadhi wakiwa wale walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika wilayani Hanang'.

Mmoja wa watu wa karibu na Sumaye alisema anachojua ni kwamba Chadema wanamtaka Sumaye na siyo Sumaye kukitaka chama hicho cha upinzani.

"Wamekuwa wakimfuatafuata mara nyingi na mazungumzo ya aina hiyo si mageni baina ya Sumaye na Chadema. Ila ninachoweza kusema, safari hii chochote kinaweza kutokea kutokana na hasira alizonazo (Sumaye). Ngoja tusubiri, atafanya mkutano na waandishi Jumapili."

Sumaye, Mbowe wazungumza
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Sumaye alisisitiza kuwa atazungumzia masuala yote yanayohusiana na uchaguzi huo wa Hanang' atakapokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam.

"Nitakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kilichotokea naomba tu mwendelee kunipa muda," alisema Sumaye na kuongeza kuwa alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye si msemaji wa Sumaye... "Sitaki kumzungumzia Sumaye. Mimi si msemaji wake. Tumsubiri yeye azungumze kuhusu hilo."

Kada wa CCM Hanang' anena

Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Hanang', Goma Gwaltu amekionya chama hicho kuwa kisipodhibiti vitendo vya rushwa katika chaguzi zake, kitakufa.

Gwaltu alisema jana kwamba kwa mazingira yaliyopo sasa ndani ya CCM bila hatua kali kuchukuliwa, kiongozi asiye na fedha hawezi kushika uongozi na ndiyo sababu anaungana na wana-CCM wengine katika wilaya hiyo, ambao wanafikiria kukihama chama hicho.

"Kama wewe una nia ya kuendelea na siasa siyo rahisi kushinda hapa Hanang' ukiwa hukubaliani na watu fulani, sasa mimi naona ni bora tu kutafuta chama kingine kwani siyo dhambi," alisema Gwaltu bila kuwataja ambao wanataka kuhama CCM.

Hata hivyo, Gwaltu alisema kwa upande wake, hafikirii kuendelea na mambo ya siasa wala kulalamika makao makuu ya CCM kuhusiana na alichokiita hujuma alizofanyiwa.
 
Sumaye ni bora ahamie CDM kiakili lakini kimwili abaki ccm ili akibomoe vizuri chama chake.Ajitahidi awe pandikizi huku wafuasi wake wakihamia cdm, yeye awe mtoa siri kwa cdm za ccm atasaidia sana mabadiliko ya demokrasia

A very good advice to him....Silazima awe Rais lakini role yake ni kubwa kuuzamisha ufisadi bahari ya Sham...Awasaidie CDM kuchukua dola huku akiwa huko huko...Pension inamtosha asihangaike sana ila afanye whats good for this country kwa kuibomoa CCM kuanzia Hanang' etc mpaka ikulu kwani anajua njia nyingi za panya za hao magamba asaidie kwenye strategy ya kuziba hizo njia na hapo atakuwa kafanya zaidi kwa wa Tanzania kuliko just kuwa Rais...

Kuna njia nyingine ya yeye kwenda huko na kutishia ngome za watu kama atatulia na kusubiri...Nikatika kurudi na kutulia ndiyo busara hufanya kazi yake na Mungu huingia kati kupigana kwa niaba ya mhusika...
 
Viongozi wa CCM wanahamia CDM ili washike nafasi za uongozi, ukombozi utatoka wapi jamani? Mwisho wote watahama halafu CDM itachukua nchi lakini chini ya viongozi wa CCM. Hili ndio changa la macho.
 
Back
Top Bottom