Baada ya kura za maoni, 95%hawataitaji katiba mpya

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Najaribu kujiuliza hivi mchakato wa kupata katiba mpya si lazima utaanza kwa kupata maoni ya watanzania ili kujua kama kweli wanahitaji katiba mpya?

Kama kutatakiwa kupata maoni ya watanzania ni tume gani itasimamia hizo kura za maoni, ninaamini kama tume itakayosimamia kura za maoni itatokana na uteuzi wa baba Ridhiwani kuna uwezekano wa kusikia 95% ya watanzania hawataki katiba mpya. Subirini:drum:
 
Kuomba maoni ya wanachi kama wanataka katiba mpya ni kuwatukana kwani hata hiyo ya zamani hatuijui.
 
matokeo ya uchaguzi au ripoti ya wananchi watakayo taka katiba mpya itawekwa wazi na usimamizi utachanganya watu mbali mbali wa dini zote wasomi na wanasiasa pia
 
Uwezekano huo ni mkubwa ikizingatiwa inatarajiwa kupunguza mamlaka makubwa ya raisi na ukiritimba wa viongozi wajao!
 
Najaribu kujiuliza hivi mchakato wa kupata katiba mpya si lazima utaanza kwa kupata maoni ya watanzania ili kujua kama kweli wanahitaji katiba mpya?

Kama kutatakiwa kupata maoni ya watanzania ni tume gani itasimamia hizo kura za maoni, ninaamini kama tume itakayosimamia kura za maoni itatokana na uteuzi wa baba Ridhiwani kuna uwezekano wa kusikia 95% ya watanzania hawataki katiba mpya. Subirini:drum:
Kitu chochote ambacho mtu hakijui..........ukimuuliza kuhusu hicho.tegemea jibu la kubuni
 
KATIBA MPYA LAZIMA

Mchakato wa katiba mpya lazima ufanyike. Asijitokeze mtu akafikiri yupo juu ya sheria. katiba ni ya wananchi. Ninatumai kwamba katiba mpya itakuwa mwanzo wa maendeleo ya wa tz. Pamoja na kutoifahamu vizuri katika hii inayokwendakubadilishwa bado wananchi wameifahamu kwa namna moja au nyingine kupitia utendaji wake. kwa mfano swala la kutokuwa na tume huru ya uchaguzi. haya ni mapungufu ya katiba na wananchi wanajua....swala la raisi kuwa na madaraka makubwa...haya ni mapungu ya katiba na wananchi wanajua...swala la uwakilishi bungeni...haya ni mapungufu na wananchi wanajua...swala la watendaji wa mikoa na wilaya kuchaguliwa na raisi haya ni mapungufu na watu wanajua...nk nk......Katiba Mpya haiepukiki.....Tuandae mchakato na ushirikishe wananchi wote.....ikiwezekana....tuige utaratibu wa kenya
 
Kila mtu anajua umuhimu wa katiba mpya, lakini kusipokuwa na tume huru ya kuratibu kura za maoni tutaambiwa 95% hawataki katiba mpya nasisi tutaishia tu kusema hatuyatambui hayo matokeo, kama ilivyo sasa kwa Urais wa mashaka jk hatukumchagua lakini yupo ikuru anaishi na familia yake
 
Bado kuna watanzania wengi hawajui hata neno Katiba maana yake nini. Na inaonekana katiba inatakwa na wanasiasa, sio wananchi walio wengi. Wananchi wengi hawajui au hawaamini kama katiba mpya italeta mabadiliko ktk unafuu wa maisha yao. Ni kama watu walivyoshawishiwa kupiga kura kwa wingi wapate mabadiliko,
 
Najaribu kujiuliza hivi mchakato wa kupata katiba mpya si lazima utaanza kwa kupata maoni ya watanzania ili kujua kama kweli wanahitaji katiba mpya?

Kama kutatakiwa kupata maoni ya watanzania ni tume gani itasimamia hizo kura za maoni, ninaamini kama tume itakayosimamia kura za maoni itatokana na uteuzi wa baba Ridhiwani kuna uwezekano wa kusikia 95% ya watanzania hawataki katiba mpya. Subirini:drum:

Nadhani Ezan unaifahamu Tanzania vizuri. Hapa ndio tunatakiwa tuanze kujadili mkakati wa kufikia katiba mpya bila ya CCM kuchakachua mchakato wa kuipata katiba mpya.

Mimi kwa mtazamo wangu hawatafuata njia hii ya kuwauliza wananchi kwa kura ya maoni ikiwa wanataka katiba mpya au la. Kwa sababu hawana uhakika kama kweli wengi watakataa katiba mpya hasa baada ya matokeo yaliyowashangaza ya uchaguzi mkuu.

Watakachofanya ni kuuliza kupitia bunge "kibogoyo" lililopo kama inatakiwa katiba mpya au vinatakiwa viraka juu ya hii iliyopo. Na kwa kuwa hii iliyopo tayari inawapa mamlaka makubwa basi watapenda kuiwekea viraka kupitia kwenye bunge la jamhuri kwani bado wana wabunge wengi wa CCM bungeni na ni rahisi.

Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa mjadala wa katiba mpya hautekwi nyara na hili bunge la CCM kwani wakifanya hivyo tutasahau uwezekano wa kupata katiba mpya. Hoja kubwa watakayotumia kupitishia mchakato huu kwenye bunge ni kuwa lina wawakilishi wa wananchi na hivyo hakuna haja tena ya kwenda kwa wananchi kupiga kura ya maoni. Na tayari wameshajenga hoja (kupitia kwa Waziri Kombani) kuwa hawana pesa ya mchakato huu wa katiba.
 
95% of what? kama ni kwa milion 5 alizoshinda its OKAY lakini wanaobaki ni wengi mamilioni zaidi ya 30 .
 
Najaribu kujiuliza hivi mchakato wa kupata katiba mpya si lazima utaanza kwa kupata maoni ya watanzania ili kujua kama kweli wanahitaji katiba mpya?

Kama kutatakiwa kupata maoni ya watanzania ni tume gani itasimamia hizo kura za maoni, ninaamini kama tume itakayosimamia kura za maoni itatokana na uteuzi wa baba Ridhiwani kuna uwezekano wa kusikia 95% ya watanzania hawataki katiba mpya. Subirini:drum:

Best unatisha sana nahiyo avatar yako. Nadhani wengi wanakula kona wakikuona khaa
 
nasikikitika sana mnaoki brand Udom vubaya. ni kweli kimekaa ki ccm bt content yake i can asure u sio y ki ccm ni ya kimageuzi na nina hakika wengi watataka katiba mpya kuliko mnavyofikiria. mnaoiponda udom, jambo usilolijua ni kama usiku wa giza
 
Hakuna swali au mjadala kuhusu kama mnataka ama hamtaki katiba mpya Swali lililopo ni jinsi ya kupeleka maoni yako Kuhusiana na katiba mpya nini kiongezwe /kifutwe au yaliyopo yafutwe yote yaandikwe mapya SAWA dogo;?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom