Baada ya kukosa uwaziri , Serukamba awachochea wabunge

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,028
2,553
Mwenyekiti wa kamati ya miundo mbinu amesema wabunge wanatakiwa kushirikiana kwa ajili ya kukwamisha bajeti ya serikali kuu inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni mwezi huu.

Alisema kama wabunge watafikia hatua hiyo itakuwa fundisho kwa serikali kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kuwadanganya wabunge.

Chanzo: Magezeti ya leo Nipashe, na Mtanzania
 
Mwenyekiti wa kamati ya miundo mbinu amesema wabunge wanatakiwa kushirikiana kwa ajili ya kukwamisha bajeti ya serikali kuu inayoyarajiwa kuwasilishwa bungeni mwezi huu, alisema kama wabunge watafikia hatua hiyo itakuwa fundisho kwa serikali kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kuwadanganya wabunge.
Chanzo: Magezeti ya leo Nipashe, na Mtanzania

Hayo magazeti yameandika 'Baada ya kukosa uwaziri'? au ni mtizamo wako tu Mh. Makupa
 
Huo ndiyo ukweli alosema Mhe. Serukamba. Mtu akisema uongo anaonekana hana maana, pia akisema ukweli nalo linakuwa tatizo. Mh!! Nchi na wananchi kwanza, Ubunge na Uwaziri baadaye.
 
:bange:duhh! mheshimiwa Serukamba hana nia na Uwaziri kabisa ila anahitaji kuwatumikia watanzania na sisi watu wa kigoma. Hujui kuwa yuko kambi la Lowasa????
 
Mwenyekiti wa kamati ya
miundo mbinu amesema wabunge wanatakiwa kushirikiana kwa ajili ya
kukwamisha bajeti ya serikali kuu inayoyarajiwa kuwasilishwa bungeni
mwezi huu, alisema kama wabunge watafikia hatua hiyo itakuwa fundisho
kwa serikali kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kuwadanganya wabunge.
Chanzo: Magezeti ya leo Nipashe, na Mtanzania

Hivi huyu Serukamba si ndie mshika sumu ya kina Lowassap!
Nasikia wanamagamba hawamkaribisi nyumbani huyu bwana.
 
Serukamba yupo right. Makupa una chuki binafsi na Serukamba.

sio chuki binafs, makupa ni gamba kubwa ambalo liko kund tofaut na serukamba ndani ya chama si unajua magamba na li chama lao la makundi, waache wakanyagane, though alichosema serukamba ndo haswaaa kinachotakiwa!
 
Serukamba yupo right. Makupa una chuki binafsi na Serukamba.
Serukamba ni mchochezi kama alivyo Maige na wenzake , embu Watanzania wenzangu tujiulize matakeo ya kuchochea wabunge na wanachi waichukie serikali iliyoko madarakani maana yake nini?
 
Serukamba sio msafi alichakachua kura jimbo la kigoma mjini na kuhonga mahakama ikapindisha ukweli kama ulivopindishwa Segerea! Pia hii kuanza kushawishi kugomea bajeti ambayo haijasomwa inanipa shida kiasi naamini kuna ajenda nyingine nyuma kwa nini asisubiri bajeti ikawasilishwa wakati wa kuijadili ndio akatoa hoja yake akinukuu vipengele vinavomsukuma au kumuaminisha bajeti hiyo haikithi mahitaji ya watanzania??au basi kama ameshaona vitabu vya bajeti angefunguka zaidi mapungufu yake ndio aseme haifai ipingwe!!
 
For your information budget tayari imeshaandaliwa kinachosubiriwa is just kuisoma bungeni.serukamba yupo sahii tumuunge mkono regardless itikadi tofauti
 
Sijamuona swahiba wangu siku nyingi sana pale kijiweni kwetu RG tukipiga hadithi na bia.
 
Mimi sina shida na huyu bwana ila nilitegema atatueleza kwa nini kamati yake ilipendekeza kampuni ya CCCC ipewe kazi ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam bila ya kushindanishwa (kwa njia ya tenda). Akilitolea maelezo hilo basi sitakua na mashaka na uzalendo wake.
 
Hajasema hivyo kwa kuukosa uwaziri bali jimboni kwake hali ni mbaya, anajaribu kujionyesha kwamba anafanya kazi.
 
Serukamba yupo sahihi kabisa kuzuia bajeti ya wizara kama serikali haikufanya vizuri katika utekelezaji wa maazimio au miapngo yake ya nyuma.Hebu tukumbushane tangu RITES ya wahindi wajiondoe TRL hadi sasa nini kimendelea katika kuboresha miundombinu ya TRL?.Je shirika la Ndege hali yake ikoje mpanka sasa je serikali imetekeleza commitement zake ipasavyo au ni maneno tu?.Serukamba kama amekwisha baini mapungufu katika maeneo hayo ni lazima serikali ichezee kichapo tu wakati wa bajeti na si vingenevyo hata kama kuna mgogoro wa makundi ya maswahiba.
 
Serukamba sio msafi alichakachua kura jimbo la kigoma mjini na kuhonga mahakama ikapindisha ukweli kama ulivopindishwa Segerea! Pia hii kuanza kushawishi kugomea bajeti ambayo haijasomwa inanipa shida kiasi naamini kuna ajenda nyingine nyuma kwa nini asisubiri bajeti ikawasilishwa wakati wa kuijadili ndio akatoa hoja yake akinukuu vipengele vinavomsukuma au kumuaminisha bajeti hiyo haikithi mahitaji ya watanzania??au basi kama ameshaona vitabu vya bajeti angefunguka zaidi mapungufu yake ndio aseme haifai ipingwe!!

uko right mkuu, inaonekana jamaa anafukuzia maslahi fulani ya kibinafsi zaidi huku akiyavika nguo ya utaifa na uzalendo
 
Back
Top Bottom