Baada ya DR Congo kuingia EAC, sasa changamkieni fursa kama ifuatavyo

Hapa udanganya bana nipo congo mwaka wa kumi sasa natembea sehemu tofauti congo kinacholipa ni biashara hasa ya vyakula magodoro lkn sio hizo kazi za afya kwanza wengi wao wanatumia mitishamba kujitibu
 
Hapa udanganya bana nipo congo mwaka wa kumi sasa natembea sehemu tofauti congo kinacholipa ni biashara hasa ya vyakula magodoro lkn sio hizo kazi za afya kwanza wengi wao wanatumia mitishamba kujitibu
Usalama upoje haswa upande kaskazini km jimbo la Kivu kule Goma hadi Beni?
 
Achana na Wakenya wenye elimu yenye tija walioanza kuwekeza kwenye mabenki na IT na kuanza kutafuta masoko ya bidhaa zao za viwandani na wamewekeza kwenye madini.

Achana na Watanzania wa taqwa na classic waliowekeza muda mrefu kwenye usafiri wa mabasi ndani ya DRC, je wewe Mtanzania mjasiliamali mdogo mwenye mtaji wa kuunga unga ufanye nini Congo.
Tuigawe congo katika pande kuu nne kwa milango minne ya kupitia Tanzania.

1. LUBUMBASHI
Hapa mpambanaji utaingilia Tunduma kwenda kasumbalesa then utavuka lubumbashi sasa lubumbashi wewe pambana upeleke vitu vifuatavo kwanza viatu raba, ukiweza nenda pale kariakoo david sports wear ongea nao wale jamaa wakuuzie bei chini zaidi beba pea kadhaa nenda nazo huko, vitambaa vya suti na batiki wewe beba tu utaenda kuuza, Kama uko vizuri peleka Nyama ya ng’ombe na mchele tani zozote unazoweza jua utaenda kuuza tu

2. KISANGANI
Hapa mpambanaji utapitia Uganda kuelekea Bwera to Kasindi Border kwa ufupi hapo utakamata basi za link utapita Beni halafu kasindi mnatoka jioni mtaenda kulala Mambasa hapo utamkuta Said mnyamwezi wa Tabora aliyelowea huko ukisema wewe mbongo pale utaelekezwa mambo yote sasa huku kuna vyuo vingi huku stationaries, bidhaa kama nguo ambazo utachukulia tu kampala maana bei rahisi, kwa ufupi wanamahitaji mengi mno lakini hata maduka ya vifaa vya muziki , yaani vinanda na magita wanapenda sana hapo unaweza kufanya utafiti ukawa unabeba gita hata nne au tano ambazo ni kali za type yao nahakika ukiwauzia vizuri utkuja kupata order makanisa yao yote usuply hizo vifaa vya bendi na muziki,

3. GOMA
Hapa mpambanaji utapitia Rusumo, utaingia Rwanda kigali pale utaingia nyabugogo kigali utapanda costa za kwenda Gisenyi baadhi ya makampuni ni Virunga na Volcano hapo utavuka kuingia goma na bidhaa nyingi zinaingiliana lakini kwa chap chap bidhaa za chakula hapo unaweza kupeleka dagaa wa ziwa victoria wale kauzu kuna jinsi ya kuwaandaa wanakua wa chumvi au unaweza kujitupa mafia, unguja au pangani ukibahatika kubeba wale dagaa nyama ukafikisha goma au lubumbashi kule juu mambo yako yatakua sio mabaya.

4. UVIRA NA KALEMIE, MOBA
kwa ufupi sana hapo unaweza kupitia Kigoma, au Burundi ili kufika uvira na kalemie na moba huko utapitia sumbawanga njia rahisi huko sasa peleka mbuzi, nyanya, ndizi za kupika, viazi mviringo, mawese, dagaa wote hasa wale wa ziwa victoria Mnaita kauzu, batiki, hapa namzungumzia mpambanaji kama mimi asie na mtaji yaani vitu vya kukimbiza chap kukuza mtaji wako.

Kwa ufupi DRC unaweza kuuza chochote unachokijua kwa mfano ukifungua garage huko kwa mafundi ni pesa tupu, ukienda kuuza vifaa vya umeme kama solar onterior parts zao utauza , ukifungua hardware uuze vifaa vya ujenzi ni wewe najua wakenya watavamia hii ya hardware kama ilivowanufaisha sudan kusini, mafuta ya kula haya korie sijui masafi huko ndio penyewe, ukijenga ukumbi mzuri wa sherehe congo utapata pesa ni wewe kusoma location, haya maduka ya spare za magari na lubricants hapo kuna fursa ni wewe ukasome soko then ujiongeze, wazee wa kupimp magari ndio mahala pake.
We jamaa bado upo Congo ?
Vipi kuhusu hali yà ushuru na rushwa ? maana Congo biashara ni ngumu sana kwa wageni sababu hiyo askari rushwa sana na kuna msululu wa kodi si wa nchi hii
 
Back
Top Bottom