Baada ya DR Congo kuingia EAC, sasa changamkieni fursa kama ifuatavyo

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,034
Achana na Wakenya wenye elimu yenye tija walioanza kuwekeza kwenye mabenki na IT na kuanza kutafuta masoko ya bidhaa zao za viwandani na wamewekeza kwenye madini.

Achana na Watanzania wa taqwa na classic waliowekeza muda mrefu kwenye usafiri wa mabasi ndani ya DRC, je wewe Mtanzania mjasiliamali mdogo mwenye mtaji wa kuunga unga ufanye nini Congo.
Tuigawe congo katika pande kuu nne kwa milango minne ya kupitia Tanzania.

1. LUBUMBASHI
Hapa mpambanaji utaingilia Tunduma kwenda kasumbalesa then utavuka lubumbashi sasa lubumbashi wewe pambana upeleke vitu vifuatavo kwanza viatu raba, ukiweza nenda pale kariakoo david sports wear ongea nao wale jamaa wakuuzie bei chini zaidi beba pea kadhaa nenda nazo huko, vitambaa vya suti na batiki wewe beba tu utaenda kuuza, Kama uko vizuri peleka Nyama ya ng’ombe na mchele tani zozote unazoweza jua utaenda kuuza tu

2. KISANGANI
Hapa mpambanaji utapitia Uganda kuelekea Bwera to Kasindi Border kwa ufupi hapo utakamata basi za link utapita Beni halafu kasindi mnatoka jioni mtaenda kulala Mambasa hapo utamkuta Said mnyamwezi wa Tabora aliyelowea huko ukisema wewe mbongo pale utaelekezwa mambo yote sasa huku kuna vyuo vingi huku stationaries, bidhaa kama nguo ambazo utachukulia tu kampala maana bei rahisi, kwa ufupi wanamahitaji mengi mno lakini hata maduka ya vifaa vya muziki , yaani vinanda na magita wanapenda sana hapo unaweza kufanya utafiti ukawa unabeba gita hata nne au tano ambazo ni kali za type yao nahakika ukiwauzia vizuri utkuja kupata order makanisa yao yote usuply hizo vifaa vya bendi na muziki,

3. GOMA
Hapa mpambanaji utapitia Rusumo, utaingia Rwanda kigali pale utaingia nyabugogo kigali utapanda costa za kwenda Gisenyi baadhi ya makampuni ni Virunga na Volcano hapo utavuka kuingia goma na bidhaa nyingi zinaingiliana lakini kwa chap chap bidhaa za chakula hapo unaweza kupeleka dagaa wa ziwa victoria wale kauzu kuna jinsi ya kuwaandaa wanakua wa chumvi au unaweza kujitupa mafia, unguja au pangani ukibahatika kubeba wale dagaa nyama ukafikisha goma au lubumbashi kule juu mambo yako yatakua sio mabaya.

4. UVIRA NA KALEMIE, MOBA
kwa ufupi sana hapo unaweza kupitia Kigoma, au Burundi ili kufika uvira na kalemie na moba huko utapitia sumbawanga njia rahisi huko sasa peleka mbuzi, nyanya, ndizi za kupika, viazi mviringo, mawese, dagaa wote hasa wale wa ziwa victoria Mnaita kauzu, batiki, hapa namzungumzia mpambanaji kama mimi asie na mtaji yaani vitu vya kukimbiza chap kukuza mtaji wako.

Kwa ufupi DRC unaweza kuuza chochote unachokijua kwa mfano ukifungua garage huko kwa mafundi ni pesa tupu, ukienda kuuza vifaa vya umeme kama solar onterior parts zao utauza , ukifungua hardware uuze vifaa vya ujenzi ni wewe najua wakenya watavamia hii ya hardware kama ilivowanufaisha sudan kusini, mafuta ya kula haya korie sijui masafi huko ndio penyewe, ukijenga ukumbi mzuri wa sherehe congo utapata pesa ni wewe kusoma location, haya maduka ya spare za magari na lubricants hapo kuna fursa ni wewe ukasome soko then ujiongeze, wazee wa kupimp magari ndio mahala pake.
 
nitafuga Kitimoto nijaribu soko la huko

Hata usifuge wewe nenda Burundi upitie wilaya ya kakonko uende kijiji cha muhange uingie burundi upande ule wanafuga nguruwe sana hadi wa elfu hamsini unapata kata vibali then fungua bucha ya viti moto ukinunua burundi unakuja kuchinja bongo then unapack vizuri na kuweka nenmbo zako omba vibali kawauzie nyamba pale goma na station yako uiweke nyakanazi pale ndio uweke center yako kuelelekea Goma
 
Gharama na process za kupata passport na visa zipoje

Hapa unaweza kukata passport ya sadec au ile ya east africa ya karatasi, au pass ya kitabu la laki na nusu wana visa yao moja ya ujirani mwema kwa ubalozi wao mdogo kule kigoma ni dola mia moja na unapata miezi mitatu kuingia na kutoka au ile on arrival visa ya dola 50 ya siku saba ambayo unapata boda yao yoyote naamini wameingia east africa now wataondosha hayo yote na wao watakua hawalipi huku kwetu hivo itakua kujiachia tu
 
Achana na wakenya wenye elimu yenye tija walioanza kuwekeza kwenye mabenki na IT na kuanza kutafuta masoko ya bidhaa zao za viwandani na wamewekeza kwenye madini.
Achana na Watanzania wa taqwa na classic waliowekeza muda mrefu kwenye usafiri wa mabasi ndani ya DRC , je wewe mtanzania mjasiliamali mdogo mwenye mtaji wa kuunga unga ufanye nini Congo.
Tuigawe congo katika pande kuu nne kwa milango minne ya kupitia Tanzania.
1. LUBUMBASHI-
Hapa mpambanaji utaingilia Tunduma kwenda kasumbalesa then utavuka lubumbashi sasa lubumbashi wewe pambana upeleke vitu vifuatavo kwanza viatu raba, ukiweza nenda pale kariakoo david sports wear ongea nao wale jamaa wakuuzie bei chini zaidi beba pea kadhaa nenda nazo huko, vitambaa vya suti na batiki wewe beba tu utaenda kuuza, Kama uko vizuri peleka Nyama ya ng’ombe na mchele tani zozote unazoweza jua utaenda kuuza tu

2.KISANGANI-
Hapa mpambanaji utapitia Uganda kuelekea Bwera to Kasindi Border kwa ufupi hapo utakamata basi za link utapita Beni halafu kasindi mnatoka jioni mtaenda kulala Mambasa hapo utamkuta Said mnyamwezi wa Tabora aliyelowea huko ukisema wewe mbongo pale utaelekezwa mambo yote sasa huku kuna vyuo vingi huku stationaries, bidhaa kama nguo ambazo utachukulia tu kampala maana bei rahisi, kwa ufupi wanamahitaji mengi mno lakini hata maduka ya vifaa vya muziki , yaani vinanda na magita wanapenda sana hapo unaweza kufanya utafiti ukawa unabeba gita hata nne au tano ambazo ni kali za type yao nahakika ukiwauzia vizuri utkuja kupata order makanisa yao yote usuply hizo vifaa vya bendi na muziki,

3.-GOMA
Hapa mpambanaji utapitia Rusumo, utaingia Rwanda kigali pale utaingia nyabugogo kigali utapanda costa za kwenda Gisenyi baadhi ya makampuni ni Virunga na Volcano hapo utavuka kuingia goma na bidhaa nyingi zinaingiliana lakini kwa chap chap bidhaa za chakula hapo unaweza kupeleka dagaa wa ziwa victoria wale kauzu kuna jinsi ya kuwaandaa wanakua wa chumvi au unaweza kujitupa mafia, unguja au pangani ukibahatika kubeba wale dagaa nyama ukafikisha goma au lubumbashi kule juu mambo yako yatakua sio mabaya.

4.-UVIRA NA KALEMIE , MOBA
kwa ufupi sana hapo unaweza kupitia Kigoma, au Burundi ili kufika uvira na kalemie na moba huko utapitia sumbawanga njia rahisi huko sasa peleka mbuzi, nyanya, ndizi za kupika, viazi mviringo, mawese, dagaa wote hasa wale wa ziwa victoria Mnaita kauzu, batiki, hapa namzungumzia mpambanaji kama mimi asie na mtaji yaani vitu vya kukimbiza chap kukuza mtaji wako.

Kwa ufupi DRC unaweza kuuza chochote unachokijua kwa mfano ukifungua garage huko kwa mafundi ni pesa tupu, ukienda kuuza vifaa vya umeme kama solar onterior parts zao utauza , ukifungua hardware uuze vifaa vya ujenzi ni wewe najua wakenya watavamia hii ya hardware kama ilivowanufaisha sudan kusini, mafuta ya kula haya korie sijui masafi huko ndio penyewe, ukijenga ukumbi mzuri wa sherehe congo utapata pesa ni wewe kusoma location, haya maduka ya spare za magari na lubricants hapo kuna fursa ni wewe ukasome soko then ujiongeze, wazee wa kupimp magari ndio mahala pake.
Mkuu vipi ufundi vifaa vya umeme unalipa nizamie huko
 
Hapo utawakuta wachaga, wapare, wanyakyusa, wakinga na waha hayo makabila wanatembea weka na mkulya, sasa waliowengi hawatembei eti wanaogopa kufa wakati hata akiwa kwao au kitandani atakufa tu
Waha wamanyema usiwataje kwa sababu ni sehemu ya kongo, yaani blood brother kama masai TZ na Kenya au mjaluo TZ na Uganda na Kenya kwa kifupi huko ni kama kwao.
Hio fursa inakuwampya kwa makabika mengine kigoma walianza muda mrefu sana kufanya biashara huko ila changamoto ilikuwa usalama.
Mtoa mada amesahau fursa ya Usafiri wa majini na sabuni.
Kongo wanategemea sabuni TZ.
Lakini kuna kilimo, nasikia wana ardhi yenye rutuba sana.
Serikali ya Kongo ituhakikishie usalama tu kwa sababu wakongo aka banyamurenge hupora mali za Watanzia.
 
Hivyo vyote ulivyosema hata hapa bongo vinauzika na pesa ipo.
Formula ni ile ile, biashara inahitaji akili kubwa ili kuifanya. Kama bado akili sio kubwa hata ukienda huko utachemsha tu kwa kuwa sio kwamba wewe ndio unakua wa kwanza kuuza hvyo vitu.
Wauzaji wapo wengi, kufanikisha ni Kama nilivyosema
 
Back
Top Bottom