Baada ya Dk. Slaa na Prof. Lipumba, nani wengine dhamira zitawasuta?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
“KWANGU mimi kuingia Ikulu ni tunda la lengo kuu ambalo ni kurudisha maadili ndani ya nchi hii. Nani hajaona matumizi ya rushwa kwenye mchakato wa Lowassa kutafuta wadhamini? Leo fedha zinazotumika ni za kina Rostam Aziz – wale wale ambao tukisimama jukwaani tumekuwa tukiwaita mafisadi. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu kwa kuwa naamini Mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu” (Dk. Slaa – Agosti 3, 2015).

“Nawaomba radhi sana wanachama na wananchi walioniamini na kuonyesha mapenzi makubwa kwangu na uongozi wangu. Nimeshiriki vikao vya Ukawa vilivyotufikisha hapa. Hata hivyo, dhamira na nafsi yangu inanisuta kuwa katika uamuzi wetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia tunu za Taifa za utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji” (Profesa Lipumba – Agosti 6, 2015).

Ndugu zangu, nimeshawishika kuanza na nukuu hizo mbili za waliokuwa vigogo wa Ukawa walioachia nyadhifa zao hivi karibuni kwa kusutwa na dhamira zao juu ya ujio wa Edward Lowassa katika umoja huo. Namaanisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Slaa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba.

Wote wawili wameziachia nyadhifa zao walizozishika kwa miaka mingi kwa sababu ya kusutwa na dhamira zao baada ya Ukawa kumpokea Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais wao kupitia Chadema. Ni hatua ambazo zinathibitisha busara zao, ukomavu wao kisiasa, weledi, uadilifu na heshima zao kwa umma.

Daima nitawaheshimu watu ambao hupoteza karibu ‘kila kitu’ kwa kujiuzulu nyadhifa zao za uongozi kwa sababu tu ya kusutwa na dhamira zao. Si siri kwamba dunia ina watu wachache wenye ujasiri huo wa kutii na kuheshimu dhamira zao.

Katika andiko lake – A Testament of Hope, mpigania haki za watu weusi wa zamani wa Marekani, Martin Luther King Jr. anasema hivi: “There comes a time when one must take a position that is neither safe nor popular but he must take it because conscience tells him it is right (kuna wakati ambapo mtu huchukua hatua au msimamo ambao si salama wala unaopendwa lakini ni lazima auchukue kwa kuwa dhamira inamwelekeza ya kuwa ni kitu sahihi kukifanya).

Kwa mantiki hiyo, nawapongeza Dk. Slaa na Profesa Lipumba kwa kuketi chini, kutafakari na kusemezana na nafsi zao, na kisha kufikia hatua ya kujiuzulu nyadhifa zao kuliko kuendelea na Ukawa ya Edward Lowassa. Wasingefanya hivyo, dhamira zingeendelea kuwasuta maisha yao yote kwa sababu walishiriki kueneza imani nchini kuwa ni fisadi. Nawapongeza kwa kuzishinda roho za kinafiki na za ubinafsi zilizojaa uchu wa pesa na madaraka.

Kwa hiyo, historia itakuja kuandikwa ya kwamba Dk. Slaa na Profesa Lipumba waliachia nyadhifa zao baada ya dhamira kuwasuta kwa kushiriki mchakato wa kumkaribisha Lowassa katika Ukawa, na hata kumfanya mgombea urais wao. Yaani Lowassa yule yule ambaye kwa miaka kadhaa walikuwa wakimpigia kelele nchi nzima kuwa ni fisadi! Yaani Lowassa yule yule aliyeibariki na kuipigia kura ya NDIYO Katiba Pendekezwa inayopingwa na Ukawa!

Ndiyo maana katika kutafakari hatua yao hiyo ya kijasiri, nimesononeshwa na lugha aliyoitumia kijana John Mnyika wa Chadema katika kumkosoa Profesa Lipumba kwa kuchukua hatua aliyoichukua. Mnyika ni kijana mdogo mno kwa Profesa Lipumba. Mnyika hamkaribii kisiasa, kielimu wala kiumri Profesa Lipumba, na hivyo alipaswa kumkosoa kiungwana.

Namshauri amsome mwanafalsafa wa zamani wa Ufaransa, Jean-Jacques Rousseau katika andiko lake kuhusu asili ya kupotea kwa usawa duniani (Origins of Inequality – page 81 part two). Rousseau anasema hivi: “Contrary to the law of nature however it may be defined, for a child to command an old man, for an imbecile to lead a wise man, and for a handful of people to gorge themselves on superfluities while the starving multitudes lacks necessities.”

Kwa ufupi anashomaanisha Rousseau, miongoni mwa mambo mengine, ni kwamba ni kinyume cha sheria ya asili kwa mdogo kumfokea au kumwamrisha mkubwa. Kosa hilo ni sawa na lile la mjinga kumwongoza mwerevu. Naamini Mnyika ananielewa, na kama ananielewa, basi naye iko siku dhamira itamsuta na kumwomba radhi Profesa Lipumba!

Hayo pembeni, turejee kwenye lile suala la kujiuzulu nyadhifa zao kwa waliokuwa vigogo wa Ukawa – Dk. Slaa na Profesa Lipumba. Hakika, kuondoka kwao Ukawa kumeibua tafsiri nyingi na mitazamo mingi kwa Watanzania.

Kuna maswali mengi yanaulizwa mitaani baada ya wiki iliyopita Lipumba naye kuachia ngazi Ukawa. Baadhi ya maswali hayo ni haya: Inakuaje Lowassa akimbiwe kule alikokimbilia? Je, nani wengine ndani ya Chadema, CUF na NCCR wataachia ngazi kwa kusutwa na dhamira zao juu ya suala la kumpokea Lowassa? Je, kuondoka kwa Slaa na Lipumba kumedhoofisha kiasi gani kampeni ya Lowassa ya kuusaka urais kupitia Upinzani?

Kwanza, labda nianze kwa kusema ya kwamba kuondoka kwa Dk. Slaa (Chadema) na baadaye Profesa Lipumba (CUF) kunathibitisha kwamba tangu mwanzo wawili hao hawakupendezwa na hatua ya Ukawa kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea urais wake kupitia Chadema.

Kama hivyo ndivyo, mtu unaweza kujiuliza ni nani hasa walikuwa vinara wa kumkaribisha Lowassa Ukawa na hata kwenye majadiliano ya iwapo aruhusiwe kugombea urais au asiruhusiwe? Hisia za wengi ni kwamba waliokuwa vinara wa kumkaribisha Lowassa Ukawa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR, James Mbatia. Dk. Emmanuel Makaidi hatajwi kwa sababu chama chake hakina ushawishi wowote mkubwa nchini japo kimo kwenye Ukawa. Ilivyo hivi sasa, Ukawa imebaki ni ya Mbowe na Mbatia.

Sasa, baada ya Dk. Slaa na Profesa Lipumba kujiondoa, hao wawili (Mbatia na Mbowe) ndio watapaswa wazunguke naye mikoani wakati wa kampeni za urais ili ‘kumsafisha’ dhidi ya tuhuma za ufisadi ambazo zimemwandama kwa miaka 20.

Ikizingatiwa kwamba Mbowe na Mbatia wanatoka Kaskazini (ni Wachaga) ambako pia anatoka mgombea urais Lowassa, utakubaliana nami ya kwamba si watu wanaofaa sana kumpigia kampeni ya urais. Maswali yataulizwa juu ya u-kaskazini wa hao watatu – Mbowe, Mbatia na Lowassa. Hakika, picha ingekuwa tofauti kama angekuwemo Lipumba kwenye kampeni.

Lakini pia lipo suala la Mbowe na Mbatia kugombea ubunge kwenye majimbo yao kule Uchagani. Sioni ni vipi wawili hao wanaweza kuandamana mikoani na Lowassa muda wote wa kampeni ‘kumsafisha’ badala ya kujipigia wenyewe kampeni kwenye majimbo yao Uchagani!

Itapaswa wachague moja - kujipigia kampeni majimboni au kuandamana na Lowassa mikoani kwenye kampeni za urais ili ‘kumsafisha’. Na kama wataamua kubaki majimboni, ni nani wengine ambao hawagombei ubunge wataandamana na Lowassa mikoani ‘kumsafisha!? Au itabidi Lowassa ‘ajisafishe’ mwenyewe wakati wa kampeni?

Nasisitiza tena kwamba hali ingekuwa ni tofauti kama Dk. Slaa na Lipumba wangelikuwa bado ni viongozi wakuu wa Chadema na CUF. Wawili hao wangeliweza kuifanya vyema kazi hiyo si tu kwa sababu wao hawagombei ubunge, lakini pia kwa sababu wanafahamika kote nchini na wana uzoefu wa kampeni za urais kwa kuwa walishawahi kugombea nafasi hiyo.

Ndugu zangu, ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba kujitoa kwa Slaa na sasa Lipumba ni pigo kubwa kwenye kampeni ya urais ya Edward Lowassa kupitia Ukawa. Na hiyo inanifanya nizidi kuamini ya kwamba itakuwa vigumu mno kwa Edward Lowassa kuutwaa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Sote tunajua ya kwamba Lowassa si mzungumzaji mzuri jukwaani na pia afya yake si nzuri sana. Katika hali hiyo, alihitaji sana msaada wa wazungumzaji wazuri kama Profesa Lipumba, Dk. Slaa au Mbowe na Mbatia ambao nimeshasema kuna shaka kama watakuwanaye (Lowassa) muda wote wa kampeni.

Kuna wasomaji wangu walinitumia meseji eti kwamba umaarufu na utajiri wa Lowassa vyenyewe ni kampeni tosha ya kumwingiza Ikulu! Kwamba eti mapesa yake na umaarufu wake vinatosha, na kwamba hahitaji sana kupigiwa kampeni na watu wengine.

Mimi nakataa. Kama mapesa na umaarufu peke yake vinatosha, mbona mwaka 2010 Godbless Lema alishinda ubunge kwa kumbwaga Dk. Matilda Buriani ambaye alisaidiwa na Lowassa kwenye kampeni? Kama mapesa na umaarufu tu vinatosha, mbona hakumwezesha swahiba wake huyo kushinda ubunge?

Lakini pia mbona Lowassa hakufanikiwa kumsaidia mkwewe kumbwaga Joshua Nassari katika uchaguzi ule mdogo wa Arumeru Mashariki licha kwamba yeye (Lowassa) aliamua kujitosa mwenyewe kwenye kampeni kumsaidia mkwewe?

Hapana ndugu zangu, umaarufu na utajiri peke yake havitoshi kumfanya mtu ashinde urais. Yapo mambo mengine mengi ya kuzingatia kama vile uadilifu, weledi, uchapakazi, maono, itikadi nk. Kama mapesa na umaarufu vingekuwa pekee yake vinatosha, basi uchaguzi wa mwaka 2010 Chadema isingeambulia jimbo hata moja mkoani Arusha ambako ndiko ngome kuu ya Lowassa!

Kwa hiyo, wanaoamini ya kuwa Lowassa atashinda urais kwa sababu tu ni maarufu na tajiri wanajidanganya. Wanaoamini ya kwamba utajiri na umaarufu wa Lowassa utawafanya wapiga kura wasahau kabisa tuhuma za ufisadi zinazomwandama kwa miaka 20, watasononeka ukweli utakapojulikana Oktoba mwaka huu.

Hao ni wale wale walioamini au walioaminishwa na kina Mbowe kwamba eti Lowassa akihamia Chadema, basi maelfu ya wanachama wa CCM watamfuata, na hivyo Chadema itashinda kirahisi Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Mpaka sasa wiki imeshapita tangu Lowassa ahamie Chadema, na bado hatujayaona hayo maelfu ya wanachama wa CCM wakimfuata! Hali hii inaififisha ile hoja ya umaarufu wake iliyotumiwa na Mbowe na wenzake kumsimamisha agombee urais kupitia Chadema.

Kwa hakika, hata wale waliokuwa maswahiba wake wa karibu katika CCM kama vile Peter Serukamba, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Emmanuel Nchimbi, Adam Kimbisa, Sophia Simba nk mpaka sasa wameamua kubaki huko huko CCM! Mbona hawajamfuata Chadema? Katika hali ya kawaida hao si ndo walipaswa kuwa wa kwanza kutimka naye Chadema kabla hao maelfu wengine hawajamfuata?

Ndugu zangu, nihitimishe kwa kusisitiza kile nilichokiandika wiki iliyopita; nacho ni kwamba, kwa kuitosa ajenda ya ufisadi ili kumpokea Lowassa, Chadema kimeipoteza nguvu yake kuu ambayo kwayo kilipata umaarufu kilio nao hivi sasa.

Kwa kuwa itakuwa vigumu kwa Chadema kuwaendea wapiga kura mikoani kikiwa na Lowassa na ajenda hiyo ya ufisadi kibindoni, sioni namna yoyote kinavyoweza kushinda uchaguzi wa Oktoba hasa baada ya kuwapoteza Slaa na Lipumba.

Na hapa bado sijaizingatia hoja nyingine kuwa CCM kitaongeza nguvu zake maradufu kuhakikisha Lowassa hatwai dola - iwe ni kwa kuiba kura au mizengwe mingine. Kwa maneno mengine, kama kilipanga mkakati wa ‘bao la mkono’ sasa kinapanga mkakati wa ‘mabao ya mikono’ ili tu kujaribu kuudhihirishia umma kwamba huyo bwana kisiasa hana nguvu na umaarufu huo mkubwa anaohusishwa nao.

Kwa ufupi, lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati kwa Chadema kumpokea Lowassa na kumsimamisha kama mgombea urais wake. Kosa hilo la kina Mbowe limetukatisha tamaa wengi wetu ambao tuliamini kuwa Chadema ni chama bora kinachopinga ufisadi kinachostahili kuwa mbadala wa CCM.

CHANZO: Gazeti la RaiaMwema.
 
Huhitaji kuwa political analyst kutambua kama uchaguzi wa mwaka huu utakuwa umewavunja moyo wale wana mageuzi halisi wengi huku wengine wakishangilia katika kambi za upinzani baada ya ujio wa Lowassa kama mgombea Urais wa mwanvuli wa UKAWA.

Huhitaji kuwa political analyst kutambua kuwa yale makundi makubwa mawili ndani ya CCM kwa sasa yameanza kuchukua safari zake kwa kutumia njia tofauti kuelekea Ikulu.

Kundi moja bado limebaki ndani ya CCM wakati kundi jingine kwa sasa liko mbioni kuelekea CHADEMA kama political pit stop kabla ya kuanza kampeni za kuingia Ikulu.

Ninaamini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na twists and turns kabla ya kumalizika!

Yangu Macho na Masikio!
 
wewe gamba kwa nini usitumie huu muda kuelezea uzuri wa magufuri kuliko kuangalia nyumba ya jiran kuna nini wakati kwako umepaacha
 
Mimi imenifanya nijue kuwa chadema ni chama cha wafanyabiashara wanaangalia zaidi pesa kuliko kuwatumikia watanzania fisadi Lowasa kauziwa chama kwa pesa zake za kifisadi.

Kwa vyovyote kakinunua chama kwa pesa nyingi sana ambazo haingekuwa rahisi kuzibeba kwenye viroba na mifuko ya sandarusi, kwahiyo kuna bank transactions zilifanyika kwahiyo ukituwekea bank zilizohusika na hii miamala, tarehe, muda, aliyepokea aliyetoa litakuwa jambo bora sana kwakuwa hapa JF hakuna cha kuficha

Lakini vilevile hii haikuwa biashara ya watu wawili tu kwenye fedha nyingi kama hizi unazozitaja wewe huhusisha watu mbalimbali wahasibu, mateller, makarani na wafanyakazi wengine kama madereva nk..haiwezekani kati ya wote Hawa asijitokeze hata mmoja kusema chochote (pengine wanaogopa) kwahiyo waweza tutajia japo wawili watatu

Ishu kama hii ina kulinda maslahi ya kila mmoja/kila upande, kwahiyo kuogopa kutapeliwa au la kuepusha migongano hasa ya cash basi lazima kuna wanasheria na kampuni zao walihusika kuandaa mikataba ya kisheria kuhusiana na hili... Si vibaya ukitutajia japo mmoja

Kinyume cha kushindwa kufanya hivi wewe Simiyu Yetu na wengine wote mnaoeneza hizi habari tutawachukulia kama ni wazushi na waongo wakubwa, wazandiki na wahuni wanafanya siasa za majitaka kwa ujira kiduchu....huku ni kutumika na hakuna neno baya kama mwanaume 'kutumika'
 
Last edited by a moderator:
Punda (CCM) Hatakiwi Kwa Sasa, Kinachohitajika Punda Afe Regardless the Means.Mambo ya Dhamira zao Kuwasuta Ili Waendelee

kuwa Wapinzani Milele Sisi Haituhusu. Kazi Iliyopo Mbele yetu Ni Moja Tu Punda Afe.
 
Mimi imenifanya nijue kuwa chadema ni chama cha wafanyabiashara wanaangalia zaidi pesa kuliko kuwatumikia watanzania fisadi Lowasa kauziwa chama kwa pesa zake za kifisadi.
Umesahau slogan ya Chama cha Mapinduzi kama ilivyowahi kutolewa na viongozi wake waandamizi huko nyuma...ilisema hivi,"ukitaka biashara yako ifanikiwe, jiunge na CCM". Sina hakika ni lini CCM ilifuta kauli hii.
 
Mimi imenifanya nijue kuwa chadema ni chama cha wafanyabiashara wanaangalia zaidi pesa kuliko kuwatumikia watanzania fisadi Lowasa kauziwa chama kwa pesa zake za kifisadi.

haya ndiyo makosa ambayo ccm watayajutia sana .....bbadala ya ku-invest fair politics ili kurudisha imani kwa wapiga kura na kuangalia mahali walipopotoka na kujirekebisha .... blindly ccm wanawatumia watu wenye uelewa mdogo sana Wa analysis kazi yap ni kuongea upotoshaji na uongo ambao hata mjinga hawezi akaukubali
 
wabunge wengine ambao bado nafsi zina wasuta na naamini ipo siku watkuja sema katika mazingira yoyote atakama ni 2020
TUNDU LISSU,WENJE,MSIGWA ,MNYIKA NA KAFULILA.
M naamin hawa wote nafsi zao zina wasuta ipo siku watasema.
 
“kwangu mimi kuingia ikulu ni tunda la lengo kuu ambalo ni kurudisha maadili ndani ya nchi hii. Nani hajaona matumizi ya rushwa kwenye mchakato wa lowassa kutafuta wadhamini? Leo fedha zinazotumika ni za kina rostam aziz – wale wale ambao tukisimama jukwaani tumekuwa tukiwaita mafisadi. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu kwa kuwa naamini mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu” (dk. Slaa – agosti 3, 2015).

“nawaomba radhi sana wanachama na wananchi walioniamini na kuonyesha mapenzi makubwa kwangu na uongozi wangu. Nimeshiriki vikao vya ukawa vilivyotufikisha hapa. Hata hivyo, dhamira na nafsi yangu inanisuta kuwa katika uamuzi wetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia tunu za taifa za utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji” (profesa lipumba – agosti 6, 2015).

Ndugu zangu, nimeshawishika kuanza na nukuu hizo mbili za waliokuwa vigogo wa ukawa walioachia nyadhifa zao hivi karibuni kwa kusutwa na dhamira zao juu ya ujio wa edward lowassa katika umoja huo. Namaanisha aliyekuwa katibu mkuu wa chadema, dk. Slaa na aliyekuwa mwenyekiti wa cuf, profesa lipumba.

Wote wawili wameziachia nyadhifa zao walizozishika kwa miaka mingi kwa sababu ya kusutwa na dhamira zao baada ya ukawa kumpokea lowassa na kumteua kuwa mgombea urais wao kupitia chadema. Ni hatua ambazo zinathibitisha busara zao, ukomavu wao kisiasa, weledi, uadilifu na heshima zao kwa umma.

Daima nitawaheshimu watu ambao hupoteza karibu ‘kila kitu’ kwa kujiuzulu nyadhifa zao za uongozi kwa sababu tu ya kusutwa na dhamira zao. Si siri kwamba dunia ina watu wachache wenye ujasiri huo wa kutii na kuheshimu dhamira zao.

Katika andiko lake – a testament of hope, mpigania haki za watu weusi wa zamani wa marekani, martin luther king jr. Anasema hivi: “there comes a time when one must take a position that is neither safe nor popular but he must take it because conscience tells him it is right (kuna wakati ambapo mtu huchukua hatua au msimamo ambao si salama wala unaopendwa lakini ni lazima auchukue kwa kuwa dhamira inamwelekeza ya kuwa ni kitu sahihi kukifanya).

Kwa mantiki hiyo, nawapongeza dk. Slaa na profesa lipumba kwa kuketi chini, kutafakari na kusemezana na nafsi zao, na kisha kufikia hatua ya kujiuzulu nyadhifa zao kuliko kuendelea na ukawa ya edward lowassa. Wasingefanya hivyo, dhamira zingeendelea kuwasuta maisha yao yote kwa sababu walishiriki kueneza imani nchini kuwa ni fisadi. Nawapongeza kwa kuzishinda roho za kinafiki na za ubinafsi zilizojaa uchu wa pesa na madaraka.

Kwa hiyo, historia itakuja kuandikwa ya kwamba dk. Slaa na profesa lipumba waliachia nyadhifa zao baada ya dhamira kuwasuta kwa kushiriki mchakato wa kumkaribisha lowassa katika ukawa, na hata kumfanya mgombea urais wao. Yaani lowassa yule yule ambaye kwa miaka kadhaa walikuwa wakimpigia kelele nchi nzima kuwa ni fisadi! Yaani lowassa yule yule aliyeibariki na kuipigia kura ya ndiyo katiba pendekezwa inayopingwa na ukawa!

Ndiyo maana katika kutafakari hatua yao hiyo ya kijasiri, nimesononeshwa na lugha aliyoitumia kijana john mnyika wa chadema katika kumkosoa profesa lipumba kwa kuchukua hatua aliyoichukua. Mnyika ni kijana mdogo mno kwa profesa lipumba. Mnyika hamkaribii kisiasa, kielimu wala kiumri profesa lipumba, na hivyo alipaswa kumkosoa kiungwana.

Namshauri amsome mwanafalsafa wa zamani wa ufaransa, jean-jacques rousseau katika andiko lake kuhusu asili ya kupotea kwa usawa duniani (origins of inequality – page 81 part two). Rousseau anasema hivi: “contrary to the law of nature however it may be defined, for a child to command an old man, for an imbecile to lead a wise man, and for a handful of people to gorge themselves on superfluities while the starving multitudes lacks necessities.”

kwa ufupi anashomaanisha rousseau, miongoni mwa mambo mengine, ni kwamba ni kinyume cha sheria ya asili kwa mdogo kumfokea au kumwamrisha mkubwa. Kosa hilo ni sawa na lile la mjinga kumwongoza mwerevu. Naamini mnyika ananielewa, na kama ananielewa, basi naye iko siku dhamira itamsuta na kumwomba radhi profesa lipumba!

Hayo pembeni, turejee kwenye lile suala la kujiuzulu nyadhifa zao kwa waliokuwa vigogo wa ukawa – dk. Slaa na profesa lipumba. Hakika, kuondoka kwao ukawa kumeibua tafsiri nyingi na mitazamo mingi kwa watanzania.

Kuna maswali mengi yanaulizwa mitaani baada ya wiki iliyopita lipumba naye kuachia ngazi ukawa. Baadhi ya maswali hayo ni haya: Inakuaje lowassa akimbiwe kule alikokimbilia? Je, nani wengine ndani ya chadema, cuf na nccr wataachia ngazi kwa kusutwa na dhamira zao juu ya suala la kumpokea lowassa? Je, kuondoka kwa slaa na lipumba kumedhoofisha kiasi gani kampeni ya lowassa ya kuusaka urais kupitia upinzani?

Kwanza, labda nianze kwa kusema ya kwamba kuondoka kwa dk. Slaa (chadema) na baadaye profesa lipumba (cuf) kunathibitisha kwamba tangu mwanzo wawili hao hawakupendezwa na hatua ya ukawa kumpokea lowassa na kumfanya mgombea urais wake kupitia chadema.

Kama hivyo ndivyo, mtu unaweza kujiuliza ni nani hasa walikuwa vinara wa kumkaribisha lowassa ukawa na hata kwenye majadiliano ya iwapo aruhusiwe kugombea urais au asiruhusiwe? Hisia za wengi ni kwamba waliokuwa vinara wa kumkaribisha lowassa ukawa ni mwenyekiti wa chadema, freeman mbowe na mwenyekiti wa nccr, james mbatia. Dk. Emmanuel makaidi hatajwi kwa sababu chama chake hakina ushawishi wowote mkubwa nchini japo kimo kwenye ukawa. Ilivyo hivi sasa, ukawa imebaki ni ya mbowe na mbatia.

Sasa, baada ya dk. Slaa na profesa lipumba kujiondoa, hao wawili (mbatia na mbowe) ndio watapaswa wazunguke naye mikoani wakati wa kampeni za urais ili ‘kumsafisha’ dhidi ya tuhuma za ufisadi ambazo zimemwandama kwa miaka 20.

Ikizingatiwa kwamba mbowe na mbatia wanatoka kaskazini (ni wachaga) ambako pia anatoka mgombea urais lowassa, utakubaliana nami ya kwamba si watu wanaofaa sana kumpigia kampeni ya urais. Maswali yataulizwa juu ya u-kaskazini wa hao watatu – mbowe, mbatia na lowassa. Hakika, picha ingekuwa tofauti kama angekuwemo lipumba kwenye kampeni.

Lakini pia lipo suala la mbowe na mbatia kugombea ubunge kwenye majimbo yao kule uchagani. Sioni ni vipi wawili hao wanaweza kuandamana mikoani na lowassa muda wote wa kampeni ‘kumsafisha’ badala ya kujipigia wenyewe kampeni kwenye majimbo yao uchagani!

Itapaswa wachague moja - kujipigia kampeni majimboni au kuandamana na lowassa mikoani kwenye kampeni za urais ili ‘kumsafisha’. Na kama wataamua kubaki majimboni, ni nani wengine ambao hawagombei ubunge wataandamana na lowassa mikoani ‘kumsafisha!? Au itabidi lowassa ‘ajisafishe’ mwenyewe wakati wa kampeni?

Nasisitiza tena kwamba hali ingekuwa ni tofauti kama dk. Slaa na lipumba wangelikuwa bado ni viongozi wakuu wa chadema na cuf. Wawili hao wangeliweza kuifanya vyema kazi hiyo si tu kwa sababu wao hawagombei ubunge, lakini pia kwa sababu wanafahamika kote nchini na wana uzoefu wa kampeni za urais kwa kuwa walishawahi kugombea nafasi hiyo.

Ndugu zangu, ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba kujitoa kwa slaa na sasa lipumba ni pigo kubwa kwenye kampeni ya urais ya edward lowassa kupitia ukawa. Na hiyo inanifanya nizidi kuamini ya kwamba itakuwa vigumu mno kwa edward lowassa kuutwaa urais kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba.

Sote tunajua ya kwamba lowassa si mzungumzaji mzuri jukwaani na pia afya yake si nzuri sana. Katika hali hiyo, alihitaji sana msaada wa wazungumzaji wazuri kama profesa lipumba, dk. Slaa au mbowe na mbatia ambao nimeshasema kuna shaka kama watakuwanaye (lowassa) muda wote wa kampeni.

Kuna wasomaji wangu walinitumia meseji eti kwamba umaarufu na utajiri wa lowassa vyenyewe ni kampeni tosha ya kumwingiza ikulu! Kwamba eti mapesa yake na umaarufu wake vinatosha, na kwamba hahitaji sana kupigiwa kampeni na watu wengine.

Mimi nakataa. Kama mapesa na umaarufu peke yake vinatosha, mbona mwaka 2010 godbless lema alishinda ubunge kwa kumbwaga dk. Matilda buriani ambaye alisaidiwa na lowassa kwenye kampeni? Kama mapesa na umaarufu tu vinatosha, mbona hakumwezesha swahiba wake huyo kushinda ubunge?

Lakini pia mbona lowassa hakufanikiwa kumsaidia mkwewe kumbwaga joshua nassari katika uchaguzi ule mdogo wa arumeru mashariki licha kwamba yeye (lowassa) aliamua kujitosa mwenyewe kwenye kampeni kumsaidia mkwewe?

Hapana ndugu zangu, umaarufu na utajiri peke yake havitoshi kumfanya mtu ashinde urais. Yapo mambo mengine mengi ya kuzingatia kama vile uadilifu, weledi, uchapakazi, maono, itikadi nk. Kama mapesa na umaarufu vingekuwa pekee yake vinatosha, basi uchaguzi wa mwaka 2010 chadema isingeambulia jimbo hata moja mkoani arusha ambako ndiko ngome kuu ya lowassa!

Kwa hiyo, wanaoamini ya kuwa lowassa atashinda urais kwa sababu tu ni maarufu na tajiri wanajidanganya. Wanaoamini ya kwamba utajiri na umaarufu wa lowassa utawafanya wapiga kura wasahau kabisa tuhuma za ufisadi zinazomwandama kwa miaka 20, watasononeka ukweli utakapojulikana oktoba mwaka huu.

Hao ni wale wale walioamini au walioaminishwa na kina mbowe kwamba eti lowassa akihamia chadema, basi maelfu ya wanachama wa ccm watamfuata, na hivyo chadema itashinda kirahisi uchaguzi mkuu wa oktoba. Mpaka sasa wiki imeshapita tangu lowassa ahamie chadema, na bado hatujayaona hayo maelfu ya wanachama wa ccm wakimfuata! Hali hii inaififisha ile hoja ya umaarufu wake iliyotumiwa na mbowe na wenzake kumsimamisha agombee urais kupitia chadema.

Kwa hakika, hata wale waliokuwa maswahiba wake wa karibu katika ccm kama vile peter serukamba, rostam aziz, andrew chenge, emmanuel nchimbi, adam kimbisa, sophia simba nk mpaka sasa wameamua kubaki huko huko ccm! Mbona hawajamfuata chadema? Katika hali ya kawaida hao si ndo walipaswa kuwa wa kwanza kutimka naye chadema kabla hao maelfu wengine hawajamfuata?

Ndugu zangu, nihitimishe kwa kusisitiza kile nilichokiandika wiki iliyopita; nacho ni kwamba, kwa kuitosa ajenda ya ufisadi ili kumpokea lowassa, chadema kimeipoteza nguvu yake kuu ambayo kwayo kilipata umaarufu kilio nao hivi sasa.

Kwa kuwa itakuwa vigumu kwa chadema kuwaendea wapiga kura mikoani kikiwa na lowassa na ajenda hiyo ya ufisadi kibindoni, sioni namna yoyote kinavyoweza kushinda uchaguzi wa oktoba hasa baada ya kuwapoteza slaa na lipumba.

Na hapa bado sijaizingatia hoja nyingine kuwa ccm kitaongeza nguvu zake maradufu kuhakikisha lowassa hatwai dola - iwe ni kwa kuiba kura au mizengwe mingine. Kwa maneno mengine, kama kilipanga mkakati wa ‘bao la mkono’ sasa kinapanga mkakati wa ‘mabao ya mikono’ ili tu kujaribu kuudhihirishia umma kwamba huyo bwana kisiasa hana nguvu na umaarufu huo mkubwa anaohusishwa nao.

Kwa ufupi, lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati kwa chadema kumpokea lowassa na kumsimamisha kama mgombea urais wake. Kosa hilo la kina mbowe limetukatisha tamaa wengi wetu ambao tuliamini kuwa chadema ni chama bora kinachopinga ufisadi kinachostahili kuwa mbadala wa ccm.

chanzo: Gazeti la raiamwema.

andikeni kwa kupoteza muda wenu tu kuandika pumba: Maamuzi tuliishayafanya zamani:eek:ktoba 25 kura ni kwa lowassa
 
Punda (CCM) Hatakiwi Kwa Sasa, Kinachohitajika Punda Afe Regardless the Means.Mambo ya Dhamira zao Kuwasuta Ili Waendelee

kuwa Wapinzani Milele Sisi Haituhusu. Kazi Iliyopo Mbele yetu Ni Moja Tu Punda Afe.
Mkuu,
Kumuua punda lazima uwe na uwezo na nyezo za kuifanya hiyo kazi ya kumuua punda!

Unaweza ukajikuta uko matatani baada ya kupigwa teke na punda!
 
Thread yako itakumbukwa mwezi October 26
Mkuu,
Nitashukuru kama itakumbukwa kwa sababu Watanzania tuko wepesi sana katika kusahau!

Unaweza kuamini kama Dk. Slaa ameanza kusahaulika kwa sasa katika medani za kisiasa nchini?

Hii ndio Tanzania!
 
Umesahau slogan ya Chama cha Mapinduzi kama ilivyowahi kutolewa na viongozi wake waandamizi huko nyuma...ilisema hivi,"ukitaka biashara yako ifanikiwe, jiunge na CCM". Sina hakika ni lini CCM ilifuta kauli hii.

Mag3.

Sasa hivi ile list yako ya mafisadi iliyotolewa pale Mwembe Yanga na Dr.W.Slaa ambayo uwa unapenda kuitumia kama reference kwenye hoja zako sasa hivi unaiogopa kama ukoma kuileta JF.

Njaa mbaya...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom