mtume pauli
Member
- Mar 8, 2012
- 44
- 6
By Nape Moses Nnauye
UZALENDO NI UPENDO KWA TAIFA
Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea meseji mbalimbali kutoka kwa vijana mbalimbali wakitaka kujua hali halisi juu ya yanayoendelea sasa huko Arusha,Mwanza na Tandahimba lakini pia wanaonesha kushtushwa kwao pale wanaposoma magazeti na kusikiliza baadhi ya radio. Wanahoji kuhusu hali ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia hili wanatoa maoni juu msimamo wa vijana na nafasi yao katika Chama.
Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
Kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha Mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.
Mimi ninao ushahidi wa kimazingira kwani nimefanya ziara nchi nzima na sehemu zote nilipokelewa na makundi ya vijana ambao ni wanachama wa CCM, lakini hata ushahidi wa takwimu unaonyesha hilo kwani katika wanachama takriban milioni sita (6,000,000) tulionao idadi ya vijana ni kubwa ukilinganisha na makundi-rika mengine.
(i) Mimi nikiwa kama msimamizi mkuu wa shughuli za uenezi wa itikadi, siasa na sera za CCM. Ninalo jukumu ndani ya Idara yangu, kutafakari kwa kina juu ya hali ya sasa ya siasa ndani na nje ya chama lakini pia ni katika majukumu yangu kuwaeleza na kuwajibu maswali mnayoniuliza juu ya upepo wa sasa wa siasa ndani ya chama.
Ni wazi kuwa upo mgongano wa mawazo na utofauti wa mitazamo juu ya namna ya uendeshaji wa shughuli za chama lakini pia juu ya maamuzi na mahusiano ya chama na wanachama wake na wananchi kwa ujumla hususani kundi la vijana ambalo ni kundi kubwa.
Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni Afya kwa chama na ni kitu kinachodhihirisha uhai wa chama cha Mapinduzi, ni ushahidi kuwa CCM inatoa nafasi kwa wanachama wake kuhoji, kushauri, kupendekeza na kukosoa. Lakini pia ni kuonesha bayana kuwa wanachama wa CCM ni makini na wenye mawazo huru muda wote. Ila inapotokea kuwa njia za kukosoa ama kushauri ni potofu huwa tunasahihisha juu ya njia iliyotumika lakini tunachukua ushauri na mapendekezo hayo.
Baadhi ya walioniandikia wanahoji ikiwa hili la Milya na madiwani linahusiana na hali hii ya migongano ya mawazo nami nawajibu kuwa ,hili la Milya linahusiana zaidi na maamuzi ya vikao vya chama vya kamati ya maadili, ambayo ilimuona Milya kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaohitajika kupewa karipio na kuonywa juu ya mwenendo wake lakini pia kujitafakari na ikibidi ajivue gamba na naamini kuwa alifanya hivyo na kukiri kwa utashi wake kuwa namna ya matendo yake na hulka zake haziendani na mwanachama muadilifu wa CCM na hivyo kwa kuwa hawezi kubadilika aliamua kujivua gamba, uamuzi ambao si tu kuwa tumeuheshimu lakini pia tumeukubali. Pia kuhusu madiwani ambao nao wanaungana na milya ni watu ambao wameshindwa kuwaza sawasawa na wanaofuata mkumbo, wameshindwa kutumia fursa kama viongozi ndani ya chama, wameshindwa kujielewa hivyo wameshindwa kuelewesha wengine.
(ii) Hata hivyo, Muundo wa Chama cha Mapinduzi kikatiba unawapa vijana fursa na nafasi ya kujipanga na kufanya kazi za chama kwa kiwango cha uelewa wao na uwezo wao. Chama kimeweka jumuiya ya vijana, ambako huko vijana wanakuwa recruited, nurtured na utilized kwa manufaa ya chama. Jumuiya hii inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa Tanzania linakuwa ni kundi la vijana wa CCM.
Na ikasemwa wazi kuwa kutakuwa na jumuiya ya vijana ambamo kutakuwepo vijana wote WANAOKUBALI IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI YA CCM.
(iii) Nikiachana na hayo; Mimi binafsi nimeshtushwa na taarifa zilizotolewa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) lakini pia kamati za Mh; Cheyo, Mrema na Zito,.ambazo zinaonesha kuwepo kwa ufisadi na matumizi ya hovyo katika mamlaka,taasisi na halmashauri mbalimbali ndani ya serikali. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kutafakari juu ya hali hii. Nikiwa kama mwanaCCM ambaye naamini katika imani ya CCM, imani yangu inayotokana na CCM ni kuwa rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa lakini kama mwanaCCM nimekula kiapo kuwa "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Taarifa hizi za mkaguzi wa serikali zinaonyesha kuwepo kwa rushwa, ufisadi na utendaji mbovu wa waajiriwa wa serikali, lakini pia zinaonyesha kwa kiasi gani tatizo la ufisadi lilivyokithiri katika jamii ya watanzania na hasa wataalam ambao kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma. Kwani pamoja na kuwepo vyombo mbalimbali vya kushughulikia rushwa na ufisadi bado ufisadi wa kiasi hiki unaendelea, naamini kuwa kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ufisadi na utendaji mbovu ni tabia inayojengeka kwenye jamii yetu, namna ya kukabiliana na hali hii ni wazi kuwa jamii yote inatakiwa kubadili namna ya kujilea, ni lazima utamaduni wa kupinga ufisadi na kufatilia na kutenda haki uimarishwe katika level ya familia, lazima tujilazimishe kusema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kwetu, lazima tujenge msingi wa maadili katika mfumo wetu wa elimu na ajira, na lazima azimio la kuyafanya haya lianzie kwenye mioyo yetu.
Tufanye maamuzi, maamuzi haya hayatalenga mtu wala koo wala kanda bali yawe maamuzi ya watanzania wote, leo Nape anapopiga kelele na kupinga ufisadi asipingwe kwa kuwa ni Nape-katibu wa itikadi CCM lakini aungwe mkono kama mtanzania mwenye nia ya kuona watanzania wote wanaishi maisha bora, Katika hili lazima jamii iungane, nimefuraishwa na wabunge hasa wa CCM walipokuwa wakichangia taarifa za kamati za bunge, waliungana na wabunge wengine katika kulielezea hili na kupendekeza namna ya kulishughulikia.
Mimi binafsi nimesikitishwa lakini pia ni changamoto inayohitaji kushughulikiwa na kutolewa maamuzi. Katika level ya Chama tutafanya yale ambayo yapo katika wigo wetu lakini pia tutashauri serikali kupitia vyombo vyake vya haki kulifuatilia hili kwa umakini mkubwa na kulitolea maamuzi, lakini pia tutawaomba wananchi watuunge mkono na kutuamini katika utekelezaji wa maamuzi na ushauri wetu.
kama bwana nape unafuatilia michango ktk hii mada uliyoweka humu jamvini, utagundua kuwa woote waliochangia wako against wewe. natumaini wengi ni vijana, ndio inajulikana vijana ndio wachangiaji wakuu humu jamvini japo wapo wazee wachache. ushauri kaa chini tafakari kwa kina jiulize kwa nini wote wamekuponda? je wanakudharau wewe kama nape au wanaidharau ccm? je baada ya miaka 3 au 13 hali itakuwaje kwako na kwa ccm? naaaaape!!!!!!!! what are you doing naaape..... huwezi kushindana na nguvu ya uma nape huwezi..........utasubiri hadi lini???