Baada ya CCM kuzidi kukimbiwa, Nape atoa kauli hii

Mimi binafsi niseme hivi, hakika Nape na WanaCCM mlioko madarakani, hebu acheni propaganda namsome ukweli na uhalisia uliopo ulingoni. Hivi Tanzania ienendavyo ninyi inawafurahisha? Ufisadi unavyozidi hivi hata soni huna kuendelea kuvumilia upuuzi na wendawazimu wa serikali hii? wewe Nape, angalia kama unataka historia ije ikuhukumu vilivyo endelea kutetea system inayokufa huku ukijidanganya kwamab hizo ni propaganda za magazeti na vyombo vya habari tu.
kwa kweli sasa nawachukia kwa moyo wangu wote, kama kufa heri CCM ife hata leo kama inavyokufa arusha, Mwanza, Mbeya na maeneo mengine mengi. Mshauri wa CCM nahisi anaumwa ugonjwa wa kusahau, hata hajui kinachoendela. Nchi au chama kibovu huendelea kuamini kuwa kinaungwa mkono mpaka kinapoelekea kuzimu. Kumbukeni, KANU, na vyama vingi kusini mwa Afrika vilikoenda, Nikuhakishie tu tazama CCM yako in one year utasema mwenyewe, the wind of change is blowing strongly against any greenish colour, the people will reclaim what has always been taken by CCM and its clique of wealth amassing gluttons. Shame on you! madawa yanaoza huku hospitali hazina dawa, aibu nape aibu nape....!!!!!! CCM inayoshabikia walaji na waporaji wakuu mlaaniwe! Kipi nape unataka CCM iendelee kuungwa nacho mkono? kwa rahisi kwenda pikiniki na misafara chungu nzima? serikali kuwa na shirika la ndege ambalo hakuna ndege hata moja inayoruka? serikali kuwa omba omba kuliko hata somalia na Iraq? au kwa kipi, nusu ya wanafunzi wasekondari wanaopata sifuri? asilimia kumi na nane ya watoto wanaojiunga na sekondari wasiojua kusoma na kuandika? au kuwa na vyuo vikuu visivyo na walimu wakutosha? au kwa kipi hasa posho za wakubwa, richmond, agreco, au nini? mimi sijui, kwa mfumuko wa bei wa asilimia zaidi ya 30, au.. hapa nawambia hamtoki fanyeni kitu, bla bla zitawaangamiza hata kabla ya 2015. Mtaikimbia nchi! deni la nchi na mengine yawachefue hata kidogo basi! AU SIKIO LA KUFA NINI?
 
Takwimu ya idadi ya wanachama anayotumia Nape ina mapungufu makubwa kwani ktk idadi hiyo anayotaja kuna wanachama waliingizwa na wagombea wa kura za maoni ili kupata waungaji mkono wao (wagombea kulipia kadi watu) ambao kimsingi ni wanachama maslahi tu. Vile vile wanachama wengine si hai tena na kwa sasa si mashabiki wa CCM.

Hoja za wabunge wa CCM azipime vizuri, kama hao ni wabunge wanaofaidi wanasema hivyo je wanachama wengine wapo au wana mtazamo gani?
Kama rejea ya NEPI ni kura 2010 amekosea hakuweka kura zilizoibwa na hawa fisi wenye magamba yenye madoadoa ya magamba yanayonuka!!
 
WEWE NAPE WEWE,tema mate chini ili kauli yako isikurudie.
kati ya fisadi na mmilya nani gamba?

NAPE TAYARI UMESHABADILI KAULI,MWANZO WAKATI CHADEMA INATANGAZA LIST OF SHAME MLIKUWA WA KWANZA KUKATAA BAADA YA KUONA MAMBO YANAWAKALIA VIBAYA MKAKUBALI NA KUTANGAZA KUJIVUA GAMBA ZOEZI AMBALO KILA MKIJARIBU MNATAPIKA.MLITAKA ROSTAM,LOWASA NA CHENGE WAANZE KUJIVUA GAMBA KWA SABABU NI MAFISADI NA WAMEILETEA CCM PICHA MBAYA KWA WATANZANIA.

SASA UNATUAMBIA KUWA MILLYA NI GAMBA,TUAMBIE KUWA HUYU ALIIBA SH NGAPI?
KWA HIYO ALIJIVUA GAMBA AU GAMBA NI WALE WANAOKUWA NA MAWAZO TOFAUTI NDANI YA CHAMA?

NAPE UNADHARAULIKA NA NAKUHAHAKIKISHIA UTADHARAULIKA MPAKA UTATEMEWA MATE.MIMI SI MNAFIKI UKWELI NAITA UKWELI NA UONGO NAITA UONGO.
 
natamani sana kujibu hayo yote yaliyojengwa kimawazo na bwana Nape hapo juu ila natumia simu button ni ndogo sana.
Nape ananifundisha jambo moja kuhusu yeye binafsi kuwa yupo tu na akiamka anaongea kuhusu leo hajali alichokwisha ongea nyuma na wala hatambui kuwa tz ya leo cya juzi, anazidi kuiaibisha ccm yke na wanamagamba wenzie. naomba niongee jambo moja hapa ambalo amelitaja kwamba milya kaamua kuvua gamba ooho! yaani kujitoa uanachama ndiyo kuvua gamba?? dah kweli nape unachekesha.
Je mnakumbuka kwenye kikao cha nec ya ccm kilichopita kasheshe la kutaka kumwajibisha kikwete wazo likitokea kwa E.L kuwa kama kutenda kosa inatosha kumvua mtu uanachama basi na kikwete avuliwe uanachama Nape alijibu nini? navyokumbuka mimi baada ya mvutano mrefu wa mkama na nape kuwa gamba si watu bali na tabia chafu, Nape akidai magamba ni watu na Mkama akiasema si watu, Nape ghafla alikaa naw waandishi wa habari kusawazisha kauli na kusema gamba si watu ila ilikuwa na maana ya ccm inabadili tabia kutoka mbovu na kuwa nzuri akiwa anahofia mkuu wa chama alikuwa anaenda chini maana EL alikuwa amepanga kwenda na mtu hata chenge nae alitoa kauli kuwa gamba liko kiunoni wa kulitoa aje na shoka mnakumbuka? pia katika orodha ya magamba milya hakuwepo, waliokuwanatajwa ni akina rostam, EL, chenge nk. milya hakuwepo sasa iweje leo aamke aseme milya ni gamba tena, unafki! na je haya maonyo au kalipio aliyestahili kupewa ni milya tu? hajui analo ongea! ataje mwingine aliye katika kalipio je hao madiwani nao wanakalipio? hojaless! nape ni kj aka. kubwa jinga
 
nape amechanganyikiwa hajui asemalo hata spika sita alishamwita vuvuzela anacheza mpira ambao hajui sheria zake
 
Political gammon shall not last forever...

Hiki kipigo wanachopata magamba ni lazima kiendelee...

Mind you Mr. Nape 'Chama ni lazima kiwasemee watu' J. K. Nyerere, 1968.
 
Taarifa yake naifananisha na VUVUZELa linalopigwa na mtu dhaifu, asiyeweza kupuliza sawasawa!!

Siye yetu macho tu:A S shade:

Hili kweli ni VUVUZELA kwani nani asiyejua kuwa Mwenyekiti wenu wa chama cha magamba pia ndio Rais anaewateua hao mawaziri wezi!! Sasa kama anashindwa au anashirikiana na wakina Mkullo kuhujumu nchi atawezaje kuwathibiti washirika wake? Ni misingi hiyo hiyo iliyompa kigugumizi kumuadhibu Jairo ingawa bunge lilimtia hatiani!!!
 
tumpe support NAPE kama tunavyowapa support akina DEO FILIKUNJOMBE,ZITTO,January Makamba,Mnyika nk.Kwani kupitia NAPE mwenyewe aliweza kuanika UFISADI wa JENGO la UVCCM...Tuache itikadi zetu katika mapambano,Siyo lazima VIJANA wote wawe wana CHADEMA hiyo siyo demokrasia...Nani atawakosoa wakiharibu?Tuache mfumo wa vyama vingi ufanye kazi bila chuki kwa VIJANA kama NAPE,MTATIRO nk
 
by nape moses nnauye

uzalendo ni upendo kwa taifa

kwa muda sasa nimekuwa nikipokea meseji mbalimbali kutoka kwa vijana mbalimbali wakitaka kujua hali halisi juu ya yanayoendelea sasa huko arusha,mwanza na tandahimba lakini pia wanaonesha kushtushwa kwao pale wanaposoma magazeti na kusikiliza baadhi ya radio. Wanahoji kuhusu hali ya vijana wa chama cha mapinduzi lakini pia hili wanatoa maoni juu msimamo wa vijana na nafasi yao katika chama.

Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.

Mimi ninao ushahidi wa kimazingira kwani nimefanya ziara nchi nzima na sehemu zote nilipokelewa na makundi ya vijana ambao ni wanachama wa ccm, lakini hata ushahidi wa takwimu unaonyesha hilo kwani katika wanachama takriban milioni sita (6,000,000) tulionao idadi ya vijana ni kubwa ukilinganisha na makundi-rika mengine.

(i) mimi nikiwa kama msimamizi mkuu wa shughuli za uenezi wa itikadi, siasa na sera za ccm. Ninalo jukumu ndani ya idara yangu, kutafakari kwa kina juu ya hali ya sasa ya siasa ndani na nje ya chama lakini pia ni katika majukumu yangu kuwaeleza na kuwajibu maswali mnayoniuliza juu ya upepo wa sasa wa siasa ndani ya chama.

Ni wazi kuwa upo mgongano wa mawazo na utofauti wa mitazamo juu ya namna ya uendeshaji wa shughuli za chama lakini pia juu ya maamuzi na mahusiano ya chama na wanachama wake na wananchi kwa ujumla hususani kundi la vijana ambalo ni kundi kubwa.

Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni afya kwa chama na ni kitu kinachodhihirisha uhai wa chama cha mapinduzi, ni ushahidi kuwa ccm inatoa nafasi kwa wanachama wake kuhoji, kushauri, kupendekeza na kukosoa. Lakini pia ni kuonesha bayana kuwa wanachama wa ccm ni makini na wenye mawazo huru muda wote. Ila inapotokea kuwa njia za kukosoa ama kushauri ni potofu huwa tunasahihisha juu ya njia iliyotumika lakini tunachukua ushauri na mapendekezo hayo.

Baadhi ya walioniandikia wanahoji ikiwa hili la milya na madiwani linahusiana na hali hii ya migongano ya mawazo nami nawajibu kuwa ,hili la milya linahusiana zaidi na maamuzi ya vikao vya chama vya kamati ya maadili, ambayo ilimuona milya kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaohitajika kupewa karipio na kuonywa juu ya mwenendo wake lakini pia kujitafakari na ikibidi “ajivue gamba” na naamini kuwa alifanya hivyo na kukiri kwa utashi wake kuwa namna ya matendo yake na hulka zake haziendani na mwanachama muadilifu wa ccm na hivyo kwa kuwa hawezi kubadilika aliamua kujivua gamba, uamuzi ambao si tu kuwa tumeuheshimu lakini pia tumeukubali. Pia kuhusu madiwani ambao nao wanaungana na milya ni watu ambao wameshindwa kuwaza sawasawa na wanaofuata mkumbo, wameshindwa kutumia fursa kama viongozi ndani ya chama, wameshindwa kujielewa hivyo wameshindwa kuelewesha wengine.

(ii) hata hivyo, muundo wa chama cha mapinduzi kikatiba unawapa vijana fursa na nafasi ya kujipanga na kufanya kazi za chama kwa kiwango cha uelewa wao na uwezo wao. Chama kimeweka jumuiya ya vijana, ambako huko vijana wanakuwa recruited, nurtured na utilized kwa manufaa ya chama. Jumuiya hii inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa tanzania linakuwa ni kundi la vijana wa ccm.
Na ikasemwa wazi kuwa ‘kutakuwa na jumuiya ya vijana ambamo kutakuwepo vijana wote wanaokubali imani, malengo na madhumuni ya ccm.


(iii) nikiachana na hayo; mimi binafsi nimeshtushwa na taarifa zilizotolewa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (cag) lakini pia kamati za mh; cheyo, mrema na zito,.ambazo zinaonesha kuwepo kwa ufisadi na matumizi ya hovyo katika mamlaka,taasisi na halmashauri mbalimbali ndani ya serikali. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kutafakari juu ya hali hii. Nikiwa kama mwanaccm ambaye naamini katika imani ya ccm, imani yangu inayotokana na ccm ni kuwa “rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa” lakini kama mwanaccm nimekula kiapo kuwa "nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Taarifa hizi za mkaguzi wa serikali zinaonyesha kuwepo kwa rushwa, ufisadi na utendaji mbovu wa waajiriwa wa serikali, lakini pia zinaonyesha kwa kiasi gani tatizo la ufisadi lilivyokithiri katika jamii ya watanzania na hasa wataalam ambao kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma. Kwani pamoja na kuwepo vyombo mbalimbali vya kushughulikia rushwa na ufisadi bado ufisadi wa kiasi hiki unaendelea, naamini kuwa kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ufisadi na utendaji mbovu ni tabia inayojengeka kwenye jamii yetu, namna ya kukabiliana na hali hii ni wazi kuwa jamii yote inatakiwa kubadili namna ya kujilea, ni lazima utamaduni wa kupinga ufisadi na kufatilia na kutenda haki uimarishwe katika level ya familia, lazima tujilazimishe kusema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kwetu, lazima tujenge msingi wa maadili katika mfumo wetu wa elimu na ajira, na lazima azimio la kuyafanya haya lianzie kwenye mioyo yetu.

Tufanye maamuzi, maamuzi haya hayatalenga mtu wala koo wala kanda bali yawe maamuzi ya watanzania wote, leo nape anapopiga kelele na kupinga ufisadi asipingwe kwa kuwa ni nape-katibu wa itikadi ccm lakini aungwe mkono kama mtanzania mwenye nia ya kuona watanzania wote wanaishi maisha bora, katika hili lazima jamii iungane, nimefuraishwa na wabunge hasa wa ccm walipokuwa wakichangia taarifa za kamati za bunge, waliungana na wabunge wengine katika kulielezea hili na kupendekeza namna ya kulishughulikia.

Mimi binafsi nimesikitishwa lakini pia ni changamoto inayohitaji kushughulikiwa na kutolewa maamuzi. Katika level ya chama tutafanya yale ambayo yapo katika wigo wetu lakini pia tutashauri serikali kupitia vyombo vyake vya haki kulifuatilia hili kwa umakini mkubwa na kulitolea maamuzi, lakini pia tutawaomba wananchi watuunge mkono na kutuamini katika utekelezaji wa maamuzi na ushauri wetu.

toka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Pole sana, kiri kushindwa kwa SSM yako. Nakushauri uje CDM tukufanyie kwanza probation ya 5 years!!! Usipoangalia SSM watakutumia na mwishowe utaishia kufa maskini!!! I recall what happened to your......RIP! Kuna wanaokutumi kupenyeza agenda zao, ukiwakamilishia, hakuna malipo, jua hilo and take my words seriously!!!
 
By Nape Moses Nnauye

UZALENDO NI UPENDO KWA TAIFA

Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea meseji mbalimbali kutoka kwa vijana mbalimbali wakitaka kujua hali halisi juu ya yanayoendelea sasa huko Arusha,Mwanza na Tandahimba lakini pia wanaonesha kushtushwa kwao pale wanaposoma magazeti na kusikiliza baadhi ya radio. Wanahoji kuhusu hali ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia hili wanatoa maoni juu msimamo wa vijana na nafasi yao katika Chama.

Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
Kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha Mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.

Mimi ninao ushahidi wa kimazingira kwani nimefanya ziara nchi nzima na sehemu zote nilipokelewa na makundi ya vijana ambao ni wanachama wa CCM, lakini hata ushahidi wa takwimu unaonyesha hilo kwani katika wanachama takriban milioni sita (6,000,000) tulionao idadi ya vijana ni kubwa ukilinganisha na makundi-rika mengine.

(i) Mimi nikiwa kama msimamizi mkuu wa shughuli za uenezi wa itikadi, siasa na sera za CCM. Ninalo jukumu ndani ya Idara yangu, kutafakari kwa kina juu ya hali ya sasa ya siasa ndani na nje ya chama lakini pia ni katika majukumu yangu kuwaeleza na kuwajibu maswali mnayoniuliza juu ya upepo wa sasa wa siasa ndani ya chama.

Ni wazi kuwa upo mgongano wa mawazo na utofauti wa mitazamo juu ya namna ya uendeshaji wa shughuli za chama lakini pia juu ya maamuzi na mahusiano ya chama na wanachama wake na wananchi kwa ujumla hususani kundi la vijana ambalo ni kundi kubwa.

Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni Afya kwa chama na ni kitu kinachodhihirisha uhai wa chama cha Mapinduzi, ni ushahidi kuwa CCM inatoa nafasi kwa wanachama wake kuhoji, kushauri, kupendekeza na kukosoa. Lakini pia ni kuonesha bayana kuwa wanachama wa CCM ni makini na wenye mawazo huru muda wote. Ila inapotokea kuwa njia za kukosoa ama kushauri ni potofu huwa tunasahihisha juu ya njia iliyotumika lakini tunachukua ushauri na mapendekezo hayo.

Baadhi ya walioniandikia wanahoji ikiwa hili la Milya na madiwani linahusiana na hali hii ya migongano ya mawazo nami nawajibu kuwa ,hili la Milya linahusiana zaidi na maamuzi ya vikao vya chama vya kamati ya maadili, ambayo ilimuona Milya kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaohitajika kupewa karipio na kuonywa juu ya mwenendo wake lakini pia kujitafakari na ikibidi “ajivue gamba” na naamini kuwa alifanya hivyo na kukiri kwa utashi wake kuwa namna ya matendo yake na hulka zake haziendani na mwanachama muadilifu wa CCM na hivyo kwa kuwa hawezi kubadilika aliamua kujivua gamba, uamuzi ambao si tu kuwa tumeuheshimu lakini pia tumeukubali. Pia kuhusu madiwani ambao nao wanaungana na milya ni watu ambao wameshindwa kuwaza sawasawa na wanaofuata mkumbo, wameshindwa kutumia fursa kama viongozi ndani ya chama, wameshindwa kujielewa hivyo wameshindwa kuelewesha wengine.

(ii) Hata hivyo, Muundo wa Chama cha Mapinduzi kikatiba unawapa vijana fursa na nafasi ya kujipanga na kufanya kazi za chama kwa kiwango cha uelewa wao na uwezo wao. Chama kimeweka jumuiya ya vijana, ambako huko vijana wanakuwa recruited, nurtured na utilized kwa manufaa ya chama. Jumuiya hii inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa Tanzania linakuwa ni kundi la vijana wa CCM.
Na ikasemwa wazi kuwa ‘kutakuwa na jumuiya ya vijana ambamo kutakuwepo vijana wote WANAOKUBALI IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI YA CCM.


(iii) Nikiachana na hayo; Mimi binafsi nimeshtushwa na taarifa zilizotolewa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) lakini pia kamati za Mh; Cheyo, Mrema na Zito,.ambazo zinaonesha kuwepo kwa ufisadi na matumizi ya hovyo katika mamlaka,taasisi na halmashauri mbalimbali ndani ya serikali. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kutafakari juu ya hali hii. Nikiwa kama mwanaCCM ambaye naamini katika imani ya CCM, imani yangu inayotokana na CCM ni kuwa “rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa” lakini kama mwanaCCM nimekula kiapo kuwa "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Taarifa hizi za mkaguzi wa serikali zinaonyesha kuwepo kwa rushwa, ufisadi na utendaji mbovu wa waajiriwa wa serikali, lakini pia zinaonyesha kwa kiasi gani tatizo la ufisadi lilivyokithiri katika jamii ya watanzania na hasa wataalam ambao kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma. Kwani pamoja na kuwepo vyombo mbalimbali vya kushughulikia rushwa na ufisadi bado ufisadi wa kiasi hiki unaendelea, naamini kuwa kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ufisadi na utendaji mbovu ni tabia inayojengeka kwenye jamii yetu, namna ya kukabiliana na hali hii ni wazi kuwa jamii yote inatakiwa kubadili namna ya kujilea, ni lazima utamaduni wa kupinga ufisadi na kufatilia na kutenda haki uimarishwe katika level ya familia, lazima tujilazimishe kusema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kwetu, lazima tujenge msingi wa maadili katika mfumo wetu wa elimu na ajira, na lazima azimio la kuyafanya haya lianzie kwenye mioyo yetu.

Tufanye maamuzi, maamuzi haya hayatalenga mtu wala koo wala kanda bali yawe maamuzi ya watanzania wote, leo Nape anapopiga kelele na kupinga ufisadi asipingwe kwa kuwa ni Nape-katibu wa itikadi CCM lakini aungwe mkono kama mtanzania mwenye nia ya kuona watanzania wote wanaishi maisha bora, Katika hili lazima jamii iungane, nimefuraishwa na wabunge hasa wa CCM walipokuwa wakichangia taarifa za kamati za bunge, waliungana na wabunge wengine katika kulielezea hili na kupendekeza namna ya kulishughulikia.

Mimi binafsi nimesikitishwa lakini pia ni changamoto inayohitaji kushughulikiwa na kutolewa maamuzi. Katika level ya Chama tutafanya yale ambayo yapo katika wigo wetu lakini pia tutashauri serikali kupitia vyombo vyake vya haki kulifuatilia hili kwa umakini mkubwa na kulitolea maamuzi, lakini pia tutawaomba wananchi watuunge mkono na kutuamini katika utekelezaji wa maamuzi na ushauri wetu.
hongera mkuu tunapenda viongozi kama nyie,mpe hi JK,mwambie tuko pamoja kukomboa watanzania ndio cha msingi,siasa baadae
 
Ripoti ya tathmini ya CHama Haimtaji Millya kama mmoja wa magamba lakini kaondoka ndo wanamuona Gamba mbona waliotajwa na chama kama mna nia ya dhati ya kusafisha CHAMA HAMUGUSI MAPAPA
 
By Nape Moses

Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
Kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha Mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.


Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni Afya kwa chama

mi naona Nape kwa kauli hizi hana tofauti Na TARIK AZZIZ wa Iraq anti zake.
 
Back
Top Bottom