Baa Maarufu Mkoani Kilmanjaro Yauza Nyama ya Mbwa...

MPAMBANAJI.COM

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
712
331
Kama nipesa basi Mji wa wagumu Mkoani Kilimanjaro Unaongoza kwa Mungu Onisha Sasa Hela ilipo(MOSHI).

Polisi Mkoani kilimanjaro inashikilia wauzaji maarufu wa nyama ya mbuzi katika Baa ijulikanayo kama MAKANYAGA mitaa ya SOWETO kwa kukamatwa wakiwa wanatundika nyama ya Mbwa kama sehemu ya nyama ya mbuzi.Tukio hili limetokea jana, huku likivuta umati mkubwa wa watu.

Ni masikitiko kwani hata mie niliyekua mgeni kwa kuoneshwa na wenyeji nilifurahia sana ile nyama ila chakusikitika sana nilikua nahisi kiu sana baada ya kula.Mashaka yangu, je namie ni miongoni mwa waliokula kitoweo cha mbwa?

Inasemekana pia baa hii ni maarufu kwa uchomaji wa Mbuzi na mwaka jana tuu ilipata tuzo ya zawadi ya tshs 1,000,000 toka Safari lager waghamini toka TBL.

Tukio hili linaonekana kuwakera wengi na wote wanasema nashukuru Mungu sijawahi kula pale ila nachoamini mkuki Moyoni

Nikiripoti kutoka hapa eneo la tukio ni wenu mwanaJF HABARI ZA KITAA
Nitarejea.

Moshi sintorudi tena.
 
Walijuaje kama hizo nyama ni nyama za mbwa na si mbuzi? Walikuwepo wakati hao mbwa wanachinjwa na kuchunwa ngozi?
 
Sishangai! Huko kwa wagumu mbona hilo dogo? Watu walishalihswa nyama ya mtu huko, hamkumbuki?
 
Mbwa ni kitoweo cha kawaida tu mbona china wanakula!!! Na wenzetu wa hehe wanakula mpaka leo!!!
!!!!
 
Nyama ya mbwa ina shida gani ? Kumbuka kile usichkula wewe kulingana na mahali ulipokulia, wenzako wanakula. Vipi kuhusu chamaki nchanga ?
 
Haya mambo ya kuchagua vyakula ndo yanaturudisha nyuma sometimes!
We are too selective kama wachina mabo ni role model kwenye dvt wanakunguta mpaka kobe na nyoka why not us.
Alafu twalalamika Njaa wakati hao wanyama wanarandaranda mitaaani
 
Yewooooooomiiiiiiiii! Mkuu kama umekula, wewe na wote waliokula walah mtapata kichaa cha mbwa na kuanza kubweka then death is inevitable. Kimbia haraka hospitali ukapate Anti-Rabies-Vaccine, utakufa hata kama unasema hurudi moshi tena.
 
Mbwa wangu wawili wamepotea tangia juzi au ndo hao waliofanywa kitoweo? ngoja niende huko soweto wakanipe hata mifupa tu nikapime DNA
 
Baa nyingi za Dar sasa zinayza nyama ya Kondoo wakisingizia ni mbuzi...mbuzi gani haina ladga imepooza...tuendapo sipo kabisaaa
 
aaaarrrrrrrggggggggg mkuu nipo moshi wiki sasa tunazulula kila jioni kwenda kula mbuzi kwenye mabaaa kumbe baa zingine wanauza dog. duh ham yote imeniisha. hata kama wengine wanakula wao ni wao mi kwangu mbwa ni kinyaaa balaaa. leo ni mwendo wa wali haragwe sitaki tena nyama hata ya kuku sitaki.
 
aaaarrrrrrrggggggggg mkuu nipo moshi wiki sasa tunazulula kila jioni kwenda kula mbuzi kwenye mabaaa kumbe baa zingine wanauza dog. duh ham yote imeniisha. hata kama wengine wanakula wao ni wao mi kwangu mbwa ni kinyaaa balaaa. leo ni mwendo wa wali haragwe sitaki tena nyama hata ya kuku sitaki.

Kwani mliambiwa Moshi sehemu ya KUZURURA! Mngekuwa mnatembelea Moshi tungewapokea lakini mmekuja kuzurura! Angalia sasa mnaenda mpaka Makanyaga!
 
Mbwa ni kitoweo cha kawaida tu mbona china wanakula!!! Na wenzetu wa hehe wanakula mpaka leo!!!
!!!!
..Mkuu hao wanataka kutengeneza tu habari kwa ajili ya media. Kama waliokula hawajadhurika na may be hawajalalamika tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom