Akamatwa na Polisi kwa kuwalisha wananchi nyama ya mbwa akiwaambia ni ya mbuzi

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Mkazi wa kijiji cha Mitonji,kata ya Mbuyuni wilayani Masasi Mkoani Mtwara,Dismasi Malikitu maarufu kizito,anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuwauzia wananchi nyama ya mbwa huku akiwadanganya ni nyama ya mbuzi.

Mtendaji wa Kijiji cha Mitonji,Yunisi Makolo amethibitisha kuhusu tukio hilo.

Chanzo: Malunde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ni ngumu mtaani jamani bila kujiongeza mambo hayaendi kabisa.

Mandhali nyama hiyo haijawadhuru aaaagh ya nini kumng'ang'ania?
 
Shida ni nini hapo maana watu hudai vyote ni halali kuliwa au hulali ni kwa nguruwe tu
Yaani hujaona shida wakati jamaa kadanganya kuwa ni mbuzi wakati ni mbwa! Tatizo linaanza kwanini adanganye, kwani angesema ukweli kuna nini
 
Katika vyakula sipendi kununua ni mishikaki asilimia kubwa ni vibudu na wala sio nyama ya mbuzi wala ng'ombe.
 
Mie niliachaga kula mishkaki au nyama kwa mtu ambae simfahamu mda sana kuna kipindi niliwahi kila nyama ya ajabu japo mi sikupata shida ila rafiki yangu aliteseka sana ikabidi tufanye upepelez kitoweo tulichokula aiseeee tulivyoambiawa acha tu yani tumekula nyama ya....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom