BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Clouds Media Group imethibitisha taarifa za kurejea kwa kiungo huyu muhimu na Mkongwe ambaye kipaji chake, ubunifu wake na umahiri wake vina mchango mkubwa sana kwenye media hii na sasa ni rasmi anarudi kuanzia alipoishia kwenye show yake ya siku zote ya XXL kuanzia Jumatatu May 26 2023.
Mkali huyu ambaye mwezi huu wa June anatimiza miaka 20 toka aanze kufanya kazi ya utangazaji kwenye Radio, aliondoka @CloudsFMTZ tarehe 31 May 2020 na kujiunga na EFM kabla ya kurejea rasmi hii leo ikiwa ni miaka mitatu baadaye.
B Twangala alianzia kutangaza Redioni CloudFM Arusha mwaka 2003 akiwa Mwanafunzi wa Sekondari Arusha Sec. huku akifanya kipindi cha DR. BEAT ( saa nane mchana hadi saa kumi) na ni miongoni mwa Waasisi wa show ya XXL ambayo ilianzishwa mwaka 2007 (saa 7 hadi 10 jioni).
Umahiri wa @Bdozen haupo tu kwenye Radio bali hata nje ya Radio ambako ameshiriki ku-host Matamasha mbalimbali ya FIESTA ambako Mastaa wa muziki duniani kama Jay Z, Busta Rymes, Fat Joe, 50 Cent, Ja Rule, Eve, Ludacris na wengine wali-perform.