Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Hakuna hata sera moja ya Nyerere ambayo inatumika TZ sasa hivi.

Nyerere VS Mwinyi
Socialist Free Market
Dictator Democracy

Kwa hiyo Azimio la Arusha ni HISTORY. Ni Sera ambazo zilishapitwa na wakati. " Hatutarudi kwenye Ujamaa" Mwinyi. Ni Capitalism na sera za Mwinyi ndizo zilizoshinda.

Ni kweli hakuna sera ya mwalimu inayoendelea sasa...lakini tujiulize tuko wapi?
 
FMEs heshima mbele mkuu,

NAdhani unaposema kuwa azimio lilishapitwa na wakati unakosea, kwani hayo maadili ya viongozi unayotaka tuyajadili kama taifa tunaweza kuyaona hapa:
(a) The Leadership
1. Every TANU and Government leader must be either a peasant or a worker, and should in no way be associated with the practices or capitalism or feudalism.
2. No TANU or Government leader should hold shares in any company.
3. No TAN U or Government leader should hold directorships in any privately owned enterprise.
4. No TANU or Government leader should receive two or more salaries.
5. No TANU or Government leader should own houses which he rents to others.
6. For the purposes of this Resolution the term ‘leader’ should comprise the following:
Members of the TANU National Executive Committee; Ministers; Members of Parliament; senior officials of organizations affiliated to TANU; senior officers of par-statal organizations; all those appointed or elected under any clause of the TANU Constitution; councilors; and civil servants in the high and middle cadres. (In this context ‘leader’ means a man, or a man and his wife; a woman, or a woman and her husband.)

Maoni yangu, tunaweza kubadilisha baadhi ya vifungu katika azimio ili liendenane na wakati huu, then tatizo la maadili tunaweza kulisolve kwa kiasi fulani.

- Mkuu Mkukuti, wale wote mnaodai tulirudishe Azimio ndio mnaokosea, tunatakiwa kukazania utawala wa kuheshimu sheria, sio mambo ya maadili ya Azimio, sasa mnapotaka ku-promote Azimio now, mtakuwa mna promote over mgongo wa sheria zetu,

- Azimio lenu halisemi kiongozi akiwa na nyumba zaidi ya mbili which is kinyume na Azimio afanywe nini, lakini sheria yetu iko wazi kama nyumba mbili ni za wizi anatakiwa kufungwa mara moja!

- Ndio maana ninasema ya maadili ya Azimio yamepitwa, sasa tuna vyama vingi vya siasa hilo Azimio lilikuwa intended on utawala wa chama kimoja na hayo mambo ya Azimio yanatakiwa kuwahusu viongozi wa CCM tu, sasa unaya-promote vipi na kwa vyama vingine kama Chadema?

Ndio maana ninasema ku-promote Azimio now, ni kukubali CCM itawale milele!

Respect.

FMEs!
 
Zakumi hiyo Katiba unayodai kuwa ndio inatuunganisha nalo ni zao la Azimio la Arusha alilolifia Seti Benjamini Mpinga. Azimio lilitamkwa 1967 na Katiba ikatungwa 1977. Katiba inalikubali Azimio la Arusha kama toleo hili la mwaka 1977 linavyosema:

LENGO NA MADHUMUNI YA KATIBA HII NI UHURU, HAKI, UDUGU NA AMANI, MAMBO AMBAYO MISINGI YAKE NI HII IFUATAYO-
...

B. KWAMBA Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

...
 
Azimio la arusha Phillemon Mikael
user_online.gif
Yesterday, 10:31 AM
5 February 1967
The Arusha Declaration

Written: for Tanganyika African National Union by Julius Nyerere, 1967;

The Arusha Declaration and TANU’s Policy on Socialism and Self-Reliance

Mkuu wa idara FMES,

Wewe ndio unaniachaga hoi kabisaa, yaani kila kitu kumlaumu mwalimu tuu, kwani unafikiria Azimio la Arusha (AA) liliandaliwa na mwalimu peke yake?

Hii tabia ya kumlaumu mwalimu kwa kila kitu itaisha lini jamani? Unaijua hadithi ya Karumekenge ambaye hakutaka kwenda shule na akawa anausingizia umande!

Amani.

- Mkuu naona usome tena hapo juu, ni quote mbili moja ya Mkulu PM, ambayo inasema wazi the author wa Azimio ni nani, halafu soma pumba zako hapo chini,

- Azimio lingekuwa sio la Mwalimu, basi walioshirkiana naye kuliweka wangejitokeza lilipokuwa likivunjwa kule Zanzibar, au lingekuwepo mpaka leo tatizo ni wewe na chuki zako binafsi na hoja zangu ambazo huwa zinakubana sana mbavu, umejaribu sana kubadili IDs, lakini inapokuja kwenye context umeshindwa ni lazima uonyeshe chuki zako na siku zote huwa ni bila hoja,

- Kuna mazuri ya Mwalimu huwa ninayakubali, lakini un-fortunately mengi ya Mwalimu pamoja na kwamba ninakubali kwamba alikuwa ni the greatest ever huwa ni mabaya sana na ndiyo yanayotutesa hili taifa mpaka leo, Mwalimu alitakiwa kusimamia sheria kwa taifa kwanza sio haya mambo ya Azimio na CCM. Mwalimu alikuwa na one best skill nayo ni alikuwa ana-command respect ya wananchi na viongozi wote aliowachagua, lakini akashindwa kuitumia kukazania utawala wa kuheshimu sheria,

- Ndio matokeo ikawa maazimio mengi yasiyotekelezeka, badala ya simply kusimamia sheria, taifa letu leo linateketea kutokana na kukosa kuheshimu sheria sio kukosekana kwa maazimio ya CCM. Sasa tumeruhusu NEC ya CCM kuamua kama Lowassa na mafisadi wenzake wana makosa kisheria au hawana, badala ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kuamua through mahakama,

- anytime unapo-promote Azimio, unali-promote over mgongo wa sheria zetu za jamhuri, huwezi kufanikiwa ndio maana Mwalimu alikwama nalo hilo Azimio, sasa love me or hate me huu ni ukweli huwezi kuubadili, simamia sheria utaona kama kuna atakayekumbuka ya Azimio, punguza obssession na FMES mkuu, imeshakufikisha pabaya tayari, jaribu kutoa hoja za kulisaidia taifa, mimi nilishaamuka siku nyingi sihitaji kuamushwa na wewe!

Respect.

FMEs!
 
FMES,
Lakini mkuu wangu huwezi kutunga sheriua kama hakuna ustaarabu fulani uunaotangulia hizo sheria. Kwa mfano huwezi weka sheria za madereva wabaya ikiwa hakuna utaratibu wa kuendesha magari hayo, hakuna alama za barabani, hakuna sheria za vyeti kwa madereva na kadhalika.

Kinachoombwa hapa ni kama vile leo hii Tanzania nzima inaendeshwa na amri ya Lowassa kuruhusu magari kwenda upande mmoja kulingana na traffic iliyopo (Azimio la Zanzibar)..Hali ambayo imesababisha kuvunjika kwa sheria zote za barabarani na huwezi kuzi apply hata kidogo..Imefikia kiasi kwamba kila kona inatakiwa askari kuongoza magari badala ya taa za traffic au alama za barabani bado wewe unajaribu kutueleza ni lazima hizo alama zitumike tu kwa sababu ni sheria hali uendeshaji wa magari wenyewe haufuati sheria hizo tena..

Msongmano huu wa kiuchumi ni sababu kubwa ya Ufisadi, hata kama madai yako yanasema Nyerere alishindwa kulisimamia Azimio la Arusha hiyo sii hoja tena..Binafsi naamini kabisa aliweza isipokuwa tatizo ni wananchi wenyewe kufuata sheria hizo..hata huku Ulaya kwenye sheria za barabani watu wanakiuka kila siku haina maana sheria zinawashiinda viongozi..

Makosa ya Nyerere yapo pale alipoongeza sheria zisizofungamana na Azimio hilo kama vile kupiga marufuku, magari madogo ya usafiri kuwa ni anasa, TV, na mengineyo mengi, hivyo badala ya kujenga Taifa lenye kufahamu kinachoendelea nchi za nje ikwa anajenga Taifa la wafungwa. Kifupi nyerere aliongoza nchi kama gereza la Ukonga hivyo sheria za nidhamu zinakuwa zinazidi mpaka wa uungwana kwani ktk fikra zake Nyerere hakumuamini mtu.. sisi sote tulikuwa kama wafungwa vile kesho tunaweza toroka..

Kifupi Azikmio la Arusha lina vipengele vingi vya kufanyiwa marekebisho hasa pale panapohusu chama kimoja lakini mfumo huo unaweza kuwa dira ya taifa zima.. mahala ambapo kunasema CCM ibadilike kuwa kiongozi yeyote wa Taifa, maswala ya Uchumi na biashara yatazamwe upya kuwapa Wawekezaji nafasi ndani ya uzalishaji na umiliki wa mali hizo..Kuna vifungu vingi muhimu sana ambavyo havitaki changes zozote na vinafit ktk serikali yoyote ile kwani mambo mengi yaliyozungumzwa ktk Azimio hilo yanakubalika hata katika Constitution ya Marekani, Uingereza, Canada na hata China.

Hili swala la kusema Azimio la Aeusha liliandikwa na mwalimu Nyerere, mkuu wangu siii hoja kabisa kwani hakuna Azimio lolote la utawala ambalo halikuandikjwa na mtu mmoja. hata hizo Consitituion.. Kwa mfano hiyo yenu ya Marekani ilitungwa na James Madison ambaye alikuwa rais wa nne wa Marekani..na hata yeye hiyo constitution ilimshinda kutimiza yote ikawa inafanyiwa marekebisho kulingana na wakati..

Mkuu wangu lisome vizuri Azimio la Arusha kisha changanua pumba toka mchele kulingana na walaji (lWATU na MAZINGIRA) upate vibaba tosha vya kuwalisha hawa Wadanganyika waliokaa na njaa kubwa..
Biafsi naaamini kabisa inawezekana, Azimio liwe ndio DIRA ya Taifa tumnalotaka kujenga..Mkuu wangu hatuwezi kabisa kusimamisha nguzo za nyumba pasipo kuwa nauelewa wa jengo gani linakusudiwa kujengwa. Ndio mahesabu ya Wadanganyika (Miafrika)..kufikiria kujenga wakati huna plan ya mjengo zaidi ya kutazama kwanza mfuko wako. Ndivyo tunavyoijenga Tanzania ya leo, kiholela habisa.

Siku zote unapojenga nyumba fuata ramani na agiza mali kulingana na ujenzi laa sivyo kila siku utaibiwa simenti, mabati, mchanga, mbao na kadhalika kwa sababu mwenye mali hufahamu anataka kujenga nyumba ya aina gani na ni vitu gani vinahitajika. Ile kufikiria tu unajenga nyumba na kuanza kufyatua matofali haitoshi kabisa mkuu wangu ktk Ujenzi wa Taifa ndani ya mfumo huu..mababu zetu walifanya hivyo kulingana na wakati ule wakimiki ardhi kubwa na vifaa vilikuwa vya asili pia... sii leo walijaribu kufyatua matofali tu pasipo plan, wengi hadi leo baada ya miaka 20 hadi 40 bado hawajajenga kitu, matokeo yake wameuza hata hivyo viwanja..Na ndiko Tanzania tunakoelekea.
Mkuu Priorities hujenga na Malengo ambayo ndio AZIMIO tunalozungumzia.
Hivi kweli mkuu wangu unaweza nambia sababu haswa ya nchi yetu kukosa UMEME na MAJI kisha kila siku tunaenda nchi za nje kuwavuta wawekezaji!.. Does it make sense!
 
Mkuu wa idara ZAKUMI,

Nadhani sasa wewe ndio unaeongea crap! hakuna anayesema Azimio ndio substitute ya utawala wa sheria! bali tunachosema Azimio ni muhimu kwa kuwa nchi inakuwa na malengo yanayoeleweka sio kama sasa hivi ambapo hatuna mwelekeo wowote ule. Hata hayo mataifa ya mabepari wakubwa bado wana maazimio yao ambayo daima yanawaongoza.

Halafu unanishangaza unavyowasema wachina huoni kuwa bila ya maazimio yao wasingekuwa hapa walipo leo?? walichofanya ni kurekebisha zile sehemu ambazo haziendi na wakati na sio kuachana na maazimio yao kabisa na matokeo unaona mda mfupi ujao wao ndio watakuwa the world next biggest superpower!
Amani.

Azimio la Arusha ni pure crap. Matatizo yako ni kuwa ujalisoma mpaka mwisho na kuelewa implications zake katika maisha yako.

Kutokana na viongozi wengi kukiuka maadili ya uongozi, watu wanaona kuwa Azimio la Arusha ni silaha ya kuweka sawa maadili ya uongozi. Lakini ukweli wa mambo, Azimio linagusa mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ambayo hayatumii principal za uchumi. Hivyo basi kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayokabili jamii za kiAfrika, utakuwa na machaguo mawili tu. Utumie sehemu ya azimio hilo au tafuta something new.

Ngoja nikupe mifano. Kwa maneno ya Chifu Kunambi. Anasema kuwa safari ya Nyerere UNO ilichangiwa na wananchi. Na kabla ya safari pesa zilikuwa hazitoshi. Rupia ikabidi akate pesa na akaonekana shujaa.

Azimio la Arusha lilipotangazwa, mmoja wa watu wa mwanzo kuona athari zake alikuwa Rupia kwa sababu mali zake zilikuwa tayari ni unyonyaji.

Mwamwindi tayari alikuwa ni mwekezaji mzawa ambao kwa sasa hivi watu kama hao tunawatafuta kuwekeza kwenye kilimo.

Moja ya matunda ya ujamaa ni benki za umma. Nyerere alikopa pesa kujenga nyumba yake ya Msasani. Na kwa maneno yake mwenyewe alishindwa kulipa. Kama rais wa nchi anashindwa kutumia Azimio la nchi kujiendeleza ni nani anayeweza ?
 
Mkuu wangu maelezo yako yote yanashambulia Azimio la Arusha pasipo kufikiria kwamba SHERIA inatakiwa kusimama vile vile.. Huwezi weka sheria mahala pasipo kuwa na AZIMIO na huwezi kutekeleza Azimio kama hakuna SHERIA..
Hivyo sote kutubaliane kwamba Nyerere aliweka Azimio lakini alishindwa kusimamisha Sheria.Hilo tumejifunza toka kwake, Leo hii tunaitaka Sheria mahala pasipokuwa na Azimio ambalo ni Malengo yetu Kitaifa. Pia HAIWEZEKANI tume/tutashindwa vile vile.
Wasomi kama nyie ni watu ambao mnatakiwa kutazama kwa undani makosa yaliyowahi tokea na kuweka kitu safi ambacho kinaweza fanya kazi.. Kwanza ni lazima tuwe na Azimio ambalo kwa kufupisha kazi wachangiaji wengi wamekubaliana na mengi mazuri ktk Miiko na maadili ya Viongozi.. Hakuna mtu aliyepongeza Azimio la Arusha sehemu ya kusimamia Uchumi wetu...
 
Azimio la Arusha ni pure crap. Matatizo yako ni kuwa ujalisoma mpaka mwisho na kuelewa implications zake katika maisha yako.
Pure Crap? Pengine ni kwa akina Zakumi! Umelisoma lakini hukuelewa yaani umesoma kama kasuku.

Kutokana na viongozi wengi kukiuka maadili ya uongozi, watu wanaona kuwa Azimio la Arusha ni silaha ya kuweka sawa maadili ya uongozi. Lakini ukweli wa mambo, Azimio linagusa mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ambayo hayatumii principal za uchumi. Hivyo basi kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayokabili jamii za kiAfrika, utakuwa na machaguo mawili tu. Utumie sehemu ya azimio hilo au tafuta something new.

Hakuna nchi ulimwenguni ambayo inaendeshwa kwa misheni town, hizo nchi za dunia ya kwanza zina maazimio yao tatizo lako upeo mdogo wa kuelewa mambo yanavyokwenda kwenye karne hii ya 21st bado uko kwenye 16th
 
Ngoja nikupe mifano. Kwa maneno ya Chifu Kunambi. Anasema kuwa safari ya Nyerere UNO ilichangiwa na wananchi. Na kabla ya safari pesa zilikuwa hazitoshi. Rupia ikabidi akate pesa na akaonekana shujaa.
Azimio la Arusha lilipotangazwa, mmoja wa watu wa mwanzo kuona athari zake alikuwa Rupia kwa sababu mali zake zilikuwa tayari ni unyonyaji.
 
Tafsiri zilizopitwa na wakati nani alikwambia matajiri walikuwa ni wanyonyaji? Beggars' belief, matajiri wanachotakiwa ni kulipa kodi yao jinsi wanavyochuma, angalia kina RA, EL, JK, et al hawawezi kukuonyesha kodi wanazolipa na hivyo kulitia hasara taifa kwenye hazina yake. Uko radhi muuza madafu alipe kodi then JK na kundi lake la mafisadi wasilipe kodi ingawa wanachuma zaidi kuliko muuza madafu - pumbaf kabisa.
 
Mwamwindi tayari alikuwa ni mwekezaji mzawa ambao kwa sasa hivi watu kama hao tunawatafuta kuwekeza kwenye kilimo.
 
Angalia vizuri historia usipotoshe ukweli Mwamwindi alikuwa ni mkulima na wapo wengi sana kama yeye mkoani Iringa, au hufahamu maana ya the big 4? Klerlu alikuwa anakula mkewe ndio sababu akala shaba acha hizi alinacha za Pwagu na Pwaguzi,

Moja ya matunda ya ujamaa ni benki za umma. Nyerere alikopa pesa kujenga nyumba yake ya Msasani. Na kwa maneno yake mwenyewe alishindwa kulipa. Kama rais wa nchi anashindwa kutumia Azimio la nchi kujiendeleza ni nani anayeweza ?

Hivi unafahamu Mwalimu alikuwa anachukua mshahara kiasi gani? Naona kati ya watu sifuri wewe ni mojawapo au ni kuwadi wa Mafisadi.
 
FMES,
Lakini mkuu wangu huwezi kutunga sheriua kama hakuna ustaarabu fulani uunaotangulia hizo sheria. Kwa mfano huwezi weka sheria za madereva wabaya ikiwa hakuna utaratibu wa kuendesha magari hayo, hakuna alama za barabani, hakuna sheria za vyeti kwa madereva na kadhalika.

Kinachoombwa hapa ni kama vile leo hii Tanzania nzima inaendeshwa na amri ya Lowassa kuruhusu magari kwenda upande mmoja kulingana na traffic iliyopo (Azimio la Zanzibar)..Hali ambayo imesababisha kuvunjika kwa sheria zote za barabarani na huwezi kuzi apply hata kidogo..Imefikia kiasi kwamba kila kona inatakiwa askari kuongoza magari badala ya taa za traffic au alama za barabani bado wewe unajaribu kutueleza ni lazima hizo alama zitumike tu kwa sababu ni sheria hali uendeshaji wa magari wenyewe haufuati sheria hizo tena..

Msongmano huu wa kiuchumi ni sababu kubwa ya Ufisadi, hata kama madai yako yanasema Nyerere alishindwa kulisimamia Azimio la Arusha hiyo sii hoja tena..Binafsi naamini kabisa aliweza isipokuwa tatizo ni wananchi wenyewe kufuata sheria hizo..hata huku Ulaya kwenye sheria za barabani watu wanakiuka kila siku haina maana sheria zinawashiinda viongozi..

Makosa ya Nyerere yapo pale alipoongeza sheria zisizofungamana na Azimio hilo kama vile kupiga marufuku, magari madogo ya usafiri kuwa ni anasa, TV, na mengineyo mengi, hivyo badala ya kujenga Taifa lenye kufahamu kinachoendelea nchi za nje ikwa anajenga Taifa la wafungwa. Kifupi nyerere aliongoza nchi kama gereza la Ukonga hivyo sheria za nidhamu zinakuwa zinazidi mpaka wa uungwana kwani ktk fikra zake Nyerere hakumuamini mtu.. sisi sote tulikuwa kama wafungwa vile kesho tunaweza toroka..

Kifupi Azikmio la Arusha lina vipengele vingi vya kufanyiwa marekebisho hasa pale panapohusu chama kimoja lakini mfumo huo unaweza kuwa dira ya taifa zima.. mahala ambapo kunasema CCM ibadilike kuwa kiongozi yeyote wa Taifa, maswala ya Uchumi na biashara yatazamwe upya kuwapa Wawekezaji nafasi ndani ya uzalishaji na umiliki wa mali hizo..Kuna vifungu vingi muhimu sana ambavyo havitaki changes zozote na vinafit ktk serikali yoyote ile kwani mambo mengi yaliyozungumzwa ktk Azimio hilo yanakubalika hata katika Constitution ya Marekani, Uingereza, Canada na hata China.

Hili swala la kusema Azimio la Aeusha liliandikwa na mwalimu Nyerere, mkuu wangu siii hoja kabisa kwani hakuna Azimio lolote la utawala ambalo halikuandikjwa na mtu mmoja. hata hizo Consitituion.. Kwa mfano hiyo yenu ya Marekani ilitungwa na James Madison ambaye alikuwa rais wa nne wa Marekani..na hata yeye hiyo constitution ilimshinda kutimiza yote ikawa inafanyiwa marekebisho kulingana na wakati..

Mkuu wangu lisome vizuri Azimio la Arusha kisha changanua pumba toka mchele kulingana na walaji (lWATU na MAZINGIRA) upate vibaba tosha vya kuwalisha hawa Wadanganyika waliokaa na njaa kubwa..
Biafsi naaamini kabisa inawezekana, Azimio liwe ndio DIRA ya Taifa tumnalotaka kujenga..Mkuu wangu hatuwezi kabisa kusimamisha nguzo za nyumba pasipo kuwa nauelewa wa jengo gani linakusudiwa kujengwa. Ndio mahesabu ya Wadanganyika (Miafrika)..kufikiria kujenga wakati huna plan ya mjengo zaidi ya kutazama kwanza mfuko wako. Ndivyo tunavyoijenga Tanzania ya leo, kiholela habisa.

Siku zote unapojenga nyumba fuata ramani na agiza mali kulingana na ujenzi laa sivyo kila siku utaibiwa simenti, mabati, mchanga, mbao na kadhalika kwa sababu mwenye mali hufahamu anataka kujenga nyumba ya aina gani na ni vitu gani vinahitajika. Ile kufikiria tu unajenga nyumba na kuanza kufyatua matofali haitoshi kabisa mkuu wangu ktk Ujenzi wa Taifa ndani ya mfumo huu..mababu zetu walifanya hivyo kulingana na wakati ule wakimiki ardhi kubwa na vifaa vilikuwa vya asili pia... sii leo walijaribu kufyatua matofali tu pasipo plan, wengi hadi leo baada ya miaka 20 hadi 40 bado hawajajenga kitu, matokeo yake wameuza hata hivyo viwanja..Na ndiko Tanzania tunakoelekea.
Mkuu Priorities hujenga na Malengo ambayo ndio AZIMIO tunalozungumzia.
Hivi kweli mkuu wangu unaweza nambia sababu haswa ya nchi yetu kukosa UMEME na MAJI kisha kila siku tunaenda nchi za nje kuwavuta wawekezaji!.. Does it make sense!

- Bob, ninakusikia sana mkuu, isipokuwa ni kwamba naona mimi na wewe hapa tuna tofautiana na one ishu, mimi ni muumini mkubwa sana na a strong beliver wa respect kwa rule of law na ubepari, siamini kitu chochote kingine zaidi ya utawala unaoheshimu sheria, siamini US au UK, wamefikia hapo walipo kimaendeleo kwa kutumia maazimio, labda maazimio ya kisheria, lakini sio ya kichama through siasa.

- Sipendi haya maneno ya kurudisha maazimio ya CCM, kwa sababu in the first place ndiyo yametufikisha hapa tulipo as a nation yaani tumekwama, waziri ni mwizi ameiba na inafahamika kuanzia na wananchi hata authorities, lakini anaitwa kwenye chama na kuambiwa amevunja ibara ya 10 ya Azimio la Arusha, kwa hiyo anahamishiwa kuwa RC Lindi, garademiti haya ndiyo yametufikisha tulipo mkuu, huyu waziri alitakiwa afikishwe kwenye mkono wa sheria na kula mvua za kumpeleka Segerea.

- Bob, ninasema tupiganie utwala unaoheshimu sheria za jamhuri, sio kurekebisha maazimio ya Arusha, ni waste of our time na hatuwezi kabisa kuendelea na hiyo mentality ya maazimio maazimio, kwanza hayo yalikuwa intended kwa chama cha CCM, sio taifa sasa taifa tuna vyama vingi vya siasa, how do we promote maazimio ya chama kimoja over ya vyama vingine, maana hapo sasa itabidi ukubali maazimio ya vyama vingine pia vya siasa,

- Tanzania, tunahitaji heshima kwa utawala wa sheria, sio heshima kwa Azimio la Arusha, ule wakati ulishapita sasa huwezi kataza viongozi wasiwe na mishahara miwili tena, au wasiwe na nyumba mbili are you kidding me or what? Ukifuatilia kwa makini sana hilo Azimio, viongozi kama Mbowe, Ndesamburo hawatakiwi kuwa kwenye uongozi wa taifa kutokana na utajiri mkubwa wa binafsi walionao tayari hata kabla ya kuwa viongozi wa siasa, hatuwezi kuendesha nchi namna hiyo, Azimio lilikuwa na lengo moja tu nalo ni kuhakikisha kwamba umasikini ni kigezo muhimu cha kuwa kiongozi wa taifa, that by-itself is insanity kwa sababu huwezi weka hizo taratibu za umasikini na uongozi leo mwaka 2009!

- Bob, I am a strong believer of Ubepari na katika ubepari serikali inakaa nyuma na kuruhusu individualism ku-shine to the full end, huku ikihakikisha kwamba the field is levelled kwa kila individual kula kwa skills zake, serikali ni ku-regulate sheria na kukusanya kodi, sio ku-impose maazimio nje ya sheria za jamhuri.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu wangu maelezo yako yote yanashambulia Azimio la Arusha pasipo kufikiria kwamba SHERIA inatakiwa kusimama vile vile.. Huwezi weka sheria mahala pasipo kuwa na AZIMIO na huwezi kutekeleza Azimio kama hakuna SHERIA..
Hivyo sote kutubaliane kwamba Nyerere aliweka Azimio lakini alishindwa kusimamisha Sheria.Hilo tumejifunza toka kwake, Leo hii tunaitaka Sheria mahala pasipokuwa na Azimio ambalo ni Malengo yetu Kitaifa. Pia HAIWEZEKANI tume/tutashindwa vile vile.
Wasomi kama nyie ni watu ambao mnatakiwa kutazama kwa undani makosa yaliyowahi tokea na kuweka kitu safi ambacho kinaweza fanya kazi.. Kwanza ni lazima tuwe na Azimio ambalo kwa kufupisha kazi wachangiaji wengi wamekubaliana na mengi mazuri ktk Miiko na maadili ya Viongozi.. Hakuna mtu aliyepongeza Azimio la Arusha sehemu ya kusimamia Uchumi wetu...

Mkandara:

Mimi si msomi ni mbeba mabokisi tu. Lakini pamoja na hayo naelewa kuwa kuna leadership and ethics vacuum in Tanzania. Na hii ina lazimisha watu kuwa na selective nolstagia ya Azimio la Arusha.

Watu wakisoma miiko ya viongozi, tayari wanapandwa mori kuwa tungekuwa na Azimio la Arusha basi EPA, Richmond, Kiwira na longolongo zingine zisingetokea.

Longolongo zinatokea sio kwa sababu ya ukosefu wa Azimio la Arusha. Zinatokea kwa sababu system ya utawala sio transparent, haina check and balance. Na mbaya zaidi hata yale mazuri yaliokuwepo, watu wamehamua kutoyafuata.
 
Pure Crap? Pengine ni kwa akina Zakumi! Umelisoma lakini hukuelewa yaani umesoma kama kasuku.

Hakuna nchi ulimwenguni ambayo inaendeshwa kwa misheni town, hizo nchi za dunia ya kwanza zina maazimio yao tatizo lako upeo mdogo wa kuelewa mambo yanavyokwenda kwenye karne hii ya 21st bado uko kwenye 16th

Tafsiri zilizopitwa na wakati nani alikwambia matajiri walikuwa ni wanyonyaji? Beggars' belief, matajiri wanachotakiwa ni kulipa kodi yao jinsi wanavyochuma, angalia kina RA, EL, JK, et al hawawezi kukuonyesha kodi wanazolipa na hivyo kulitia hasara taifa kwenye hazina yake. Uko radhi muuza madafu alipe kodi then JK na kundi lake la mafisadi wasilipe kodi ingawa wanachuma zaidi kuliko muuza madafu - pumbaf kabisa.
 
Angalia vizuri historia usipotoshe ukweli Mwamwindi alikuwa ni mkulima na wapo wengi sana kama yeye mkoani Iringa, au hufahamu maana ya the big 4? Klerlu alikuwa anakula mkewe ndio sababu akala shaba acha hizi alinacha za Pwagu na Pwaguzi,

Hivi unafahamu Mwalimu alikuwa anachukua mshahara kiasi gani? Naona kati ya watu sifuri wewe ni mojawapo au ni kuwadi wa Mafisadi.

Wacha:

Ngoja nirudie tena: AZIMIO LA ARUSHA WAS PURE CRAP. Vilevile katika posti yako hakuna kipya cha maana zaidi ya kujaribu ku-debate kwa kutumia emotions.

Kwanza unatakiwa kuelewa kuwa Azimio la Arusha ni Party Creed. Ilikuwa ni misimamo ya TANU na baadaye kurithiwa na CCM.

Hivyo basi chama chochote cha kisiasa hakiwezi kuwa juu ya nchi la kulazimisha imani zake kwa raia wote.

Sasa hivi nchi ya vyama vingi. Hivyo basi kuna mistari ya uendeshaji wa chama na uendeshaji serikali. Na kwa mtaji huu, imani ya chama cha siasa sio lazima iwe sera za nchi.

Mimi sio mwanachama wa CCM and I don't give a damn kuhusiana na chama hicho. Ninachofanya ni kile mkristo anachoweza kusema kuhusu kuwa Muhamad sio mtume. Na vilevile mwislamu kusema kuwa Yesu sio Mungu.
 
- Bob, ninakusikia sana mkuu, isipokuwa ni kwamba naona mimi na wewe hapa tuna tofautiana na one ishu, mimi ni muumini mkubwa sana na a strong beliver wa respect kwa rule of law na ubepari, siamini kitu chochote kingine zaidi ya utawala unaoheshimu sheria, siamini US au UK, wamefikia hapo walipo kimaendeleo kwa kutumia maazimio, labda maazimio ya kisheria, lakini sio ya kichama through siasa.

- Sipendi haya maneno ya kurudisha maazimio ya CCM, kwa sababu in the first place ndiyo yametufikisha hapa tulipo as a nation yaani tumekwama, waziri ni mwizi ameiba na inafahamika kuanzia na wananchi hata authorities, lakini anaitwa kwenye chama na kuambiwa amevunja ibara ya 10 ya Azimio la Arusha, kwa hiyo anahamishiwa kuwa RC Lindi, garademiti haya ndiyo yametufikisha tulipo mkuu, huyu waziri alitakiwa afikishwe kwenye mkono wa sheria na kula mvua za kumpeleka Segerea.

- Bob, ninasema tupiganie utwala unaoheshimu sheria za jamhuri, sio kurekebisha maazimio ya Arusha, ni waste of our time na hatuwezi kabisa kuendelea na hiyo mentality ya maazimio maazimio, kwanza hayo yalikuwa intended kwa chama cha CCM, sio taifa sasa taifa tuna vyama vingi vya siasa, how do we promote maazimio ya chama kimoja over ya vyama vingine, maana hapo sasa itabidi ukubali maazimio ya vyama vingine pia vya siasa,

- Tanzania, tunahitaji heshima kwa utawala wa sheria, sio heshima kwa Azimio la Arusha, ule wakati ulishapita sasa huwezi kataza viongozi wasiwe na mishahara miwili tena, au wasiwe na nyumba mbili are you kidding me or what? Ukifuatilia kwa makini sana hilo Azimio, viongozi kama Mbowe, Ndesamburo hawatakiwi kuwa kwenye uongozi wa taifa kutokana na utajiri mkubwa wa binafsi walionao tayari hata kabla ya kuwa viongozi wa siasa, hatuwezi kuendesha nchi namna hiyo, Azimio lilikuwa na lengo moja tu nalo ni kuhakikisha kwamba umasikini ni kigezo muhimu cha kuwa kiongozi wa taifa, that by-itself is insanity kwa sababu huwezi weka hizo taratibu za umasikini na uongozi leo mwaka 2009!

- Bob, I am a strong believer of Ubepari na katika ubepari serikali inakaa nyuma na kuruhusu individualism ku-shine to the full end, huku ikihakikisha kwamba the field is levelled kwa kila individual kula kwa skills zake, serikali ni ku-regulate sheria na kukusanya kodi, sio ku-impose maazimio nje ya sheria za jamhuri.

Respect.

FMEs!

FMES:

Maneno mazito unayozungumza. Tanzania ina tabia mbili kunapotokea matatizo. Kuunda kamati za uchunguzi au kupitisha maazimio.Toka nimezaliwa maazimio na kamati lukuki za uchunguzi zimeundwa na sioni cha maana kinachoendelea. Hivyo inanifanya kuamini kuwa, watu wanakwepa kuwajibika.
 
Zakumi hiyo Katiba unayodai kuwa ndio inatuunganisha nalo ni zao la Azimio la Arusha alilolifia Seti Benjamini Mpinga. Azimio lilitamkwa 1967 na Katiba ikatungwa 1977. Katiba inalikubali Azimio la Arusha kama toleo hili la mwaka 1977 linavyosema:

LENGO NA MADHUMUNI YA KATIBA HII NI UHURU, HAKI, UDUGU NA AMANI, MAMBO AMBAYO MISINGI YAKE NI HII IFUATAYO-
...

B. KWAMBA Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

...

Hivi nikikuuliza Ujamaa ni nini? na kujitegemea ni nini? Je unaweza kupata tafsiri ya kuonyesha kujenga jamii ya watu walio sawa na huru?

Au wakati mwingine tunakubali maneno ya watu bila kufikiri?
 
Nani aliua Azimio la Arusha? Ikiwa Azimio la Arusha lilikufa wakati Muasisi mwenyewe bado yu hai)Nyerere kwa nini tusikubali kuwa lilishindwa na Azimio lingine bora zaidi lingekuja??

Kwa tabia ya watanzania ilivyo na jinsi tunavyokwepa kuwajibika, hata Azimio lingekuwa la kuzimu au Peponi lingevunjwa tu;

Sijajua wala siamini MANENO MATAMU YA AZIMIO LA ARUSHA YAMEZIKWA NA SITAKI KUAMINI KUWA WATU WAONE KUWA NDIO MSINGI WA TATIZO,

Naomba kuwasilisha kuwa watanzania tuna Tatizo lingine ambalo kamwe Azimio la Arusha hata kama lingekuwa hai hii leo lisingefanya lolote!

Nyerere alishawahi kusema lolote baada ya kifo cha hili Azimio??

Kumbuka miaka hiyo kweusi, globalisation bado haijaanza,Aazimio llishakufa leo hii si ndio hata kujadiliwa lisingejadiliwa??
 
Jamani eeh...........na hebu tuchambue basi ni mambo yepi hayatufai na yepi yanatufaa katika hilo Azimio la Arusha..............na sio kushuka na general conclusions tu..........au nimemuelewa vibaya muanzisha mada?..........
 
5 February 1967
The Arusha Declaration

Written: for Tanganyika African National Union by Julius Nyerere, 1967;

The Declaration was discussed and then published in Swahili. This revised English Translation clarifies ambiguities which existed in the translation originally issued.
The Arusha Declaration and TANU’s Policy on Socialism and Self-Reliance

PART ONE
The TANU Creed

The policy of TANU is to build a socialist state. The principles of socialism are laid down in the TANU Constitution and they are as follows:
WHEREAS TANU believes:

Nyerere Archive

- Sasa Mkulu Ogah, hebu nisaidie hapa tu kwa kuanza tunajadili nini hasa cha kuweza kutusadia hili taifa, I mean haya maneno ya Socialism yalishapitwa na wakati,

- Nia na madhumuni ilikuwa ni kujenga taifa la ki-Socialism ambalo sasa sio tena, sasa please help me unajadili nini hasa hapo worthy kwa taifa letu la leo?

Respect.

FMEs!
 
FMES,
Mkuu nakusikia sana na pengine bado hujaelewa kiini cha maelezo yangu. Nitajaribu kwa uwezo wangu kukufahamisha zaidi undani ya maelezo yangu pengine unaweza toka nje ya hilo kabati la gubu dhidi ya Ujamaa na Nyerere..Mkuu hata mimi naamini Ubepari ktk maendeleo ya Kiuchumi lakini ktk mfumo uliokuwa na miiko na maadili ya viongozi wake.(Azimio la Arusha)
Labda nikurudishe ktk kitu aambacho unakielewa vizuri zaidi..kuna vitu viwili Miiko na maadili ya Viongozi (Azimio la Arusha) na pili Sheria (Constitution)..

Kwanza kabisa kuhusu Ujamaa na Umaskini, mkuu wewe ni muumini wa dini, hivi kweli Yesu au mitume wote wangeangalia kwanza maisha yetu ktk mzani wa Masikini na Tajiri ili kuhubiri neno la Mungu ingewezekana?.
Na sidhani kama hata hizo sheria za dini iwe Ten commandament kama zingekuwepo ikiwa Moses hakuwa na mwongozo kwake kama kiongozi..Miiko na maadili ya uongozi wao iwe Moses, Yesu au mtume yeyote yule ilikuwa nje ya sheria za kuabudu kama vile Ten Commandament ambazo ni kwa waumini au binadamu wote. As leaders walitakiwa kutofanya baadhi ya mambo ambayo wewe na mimi tunaweza kabisa kuyafanya na isiwe tumevunja sheria..

Mkuu wangu, Ili Yesu aweze kuitangaza dini au kuwaongoza wakristu alikuwa na majukumu tofauti kabisa na waumini wake, Azimio la Arusha tunalozungumzia sisi halina maana kila Mtanzania anatakiwa kuwa Mjamaa, ila ili uwe kiongozi unatakiwa uwe mtu wa aina gani...Na itachekesha sana ikiwa sisi tutategemea Kiongozi awe mtu wa aina fulani pasipo yeye kufahamu miiko na maadili ya uongozi wake..Huwezi kutumia sheria za Uraia au niseme waumini sawa na mtu ambaye ana madaraka tayari ukashindwa kuweka vigezo vya Kiongozi..Yaani unataka hata Mapadre wafuate sheria kama zetu lakini ktk Upadre wao pasiwepo na sheria zinazowaongoza wao kama Mapadre!..Sijui kama umenielewa upana wa mawazo yangu ktk kutofautisha vitru hivi..

Kwa hiyo ukisoma Azimio la Arusha, utakuta kuna vipengele vingi sana vimo katika Maazimio ya viongozi wa nchi tajiri na Mabepari, tatizo letu sisi tumehalalisha hata haramu hizo kwa viongozi. Yes, Mbowe ni tajiri, Ndesamburo ni tajiri lakini siku akitaka kushika madaraka ofisi ya serikali basi hana budi kuachia ngazi biashara zake. Ni muhimu sana tutofautishe mali ulokuwa nayo kiongozi na kiongozi huyo kuendesha biashara. huwezi kuweka sheria ya kuzuia Conflict of interest ikiwa kiongozi huyo anaruhusiwa kuwa na interest sehemu mbili au tatu..Ndio maana nikasema Ubepari tumeuvamia pasipo kuelewa unafanya kazi vipi..ni matumizi ya common sense tu mkuu wangu haina Ujamaa wala Ubepari..
Ni kama vile mtu aliyeamua kuoa mke inambidi aache vimada alokuwa nao kabla ya ndoa hata kama alikuwa nao 10, maadam kaamua kuoa mke basi mchezo wake alokuwa nao Ukapela ndio umetoka. Lakini Azimio hilo halimkatazi kapela (wasiokuwa viongozi) kuendelea kupuyanga..Hivyo kama viongozi, kina Mbowe hawataki au hawawezi basi waache kuoa.
 
Hivi nikikuuliza Ujamaa ni nini? na kujitegemea ni nini? Je unaweza kupata tafsiri ya kuonyesha kujenga jamii ya watu walio sawa na huru?

Au wakati mwingine tunakubali maneno ya watu bila kufikiri?

Hilo swali nimeshakujibu mara kadhaa. Rejea mjadala wa Nguzo 5 za Ujamaa. Kama huzikumbuki hizi hapa:
Sunday, July 5, 2009

UNAZIKUMBUKA NGUZO TANO ZA UJAMAA?

Katika kipindi hiki ambapo jamii mbalimbali duniani zinapigania haki na usawa hasa ule wa kumiliki rasilimali ambazo zimepokwa na zinazidi kunyakuliwa na waumini wa itikidi ya uliberali mamboleo ni vyema tukajikumbusha Nguzo Tano za Ujamaa hasa nguzo ya nne inayogusia rasilimali kuu ya ardhi:

NGUZO TANO ZA UJAMAA - KWA MUJIBU WA MWALIMU JULIUS K. NYERERE, SABA SABA 1970

1. 'WATU WOTE NI SAWA'

"...Kama hukubali hilo, yaani kama unadhani watu wengine ni miungu wengine, malaika, wengine nusu-nyani, basi hukubali ujamaa. Ujamaa kwako hauna maana, kwa sababu ujamaa unahusu usawa wa watu: hapo ndipo unapoanza...Sisemi usawa wa urefu wala ufupi; kwa urefu namzidi Kawawa, sana tena. Sisemi maguvu, hata; nasema utu, watu, na ubinadamu wao. Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe? Kama huliamini hilo, utakuwa mjamaa? Hilo la kwanza... mkaliulize-ulize, mlielewe maana yake. Na mtu anayepinga ujamaa naye ajiulize kama anapinga hilo nalo. Mtu mpingaji ujamaa aseme, 'Hilo nalo, usawa wa watu, napinga; kwamba binadamu wote hivi si sawa'" - Mwalimu Julius K. Nyerere

2. 'LAZIMA MTU AFANYE KAZI'

"...Binadamu hao unaotuona hapa, na hao waliosambaa dunia nzima wanaishi kwa kazi. Hawana namna nyingine ya kuishi. Wakiacha kufanya kazi watakufa; hawana namna nyingine; kuishi kwao, na kuendelea kuishi, lazima wafanye kazi...Lakini binadamu haishi kama farasi. Binadamu haridhiki kuishi kama farasi au punda; binadamu ana kitu anakiita maendeleo; lazima aendelee...Wakati mwingine ili kusudi maendeleo haya yaje wana shughuli za kupigana misasa akili, wanapanuana mawazo tu, nayo ni kazi...nendeni mkaulizane...kama kazi si kitu cha lazima, kama binadamu anaweza kujikalia tu hafanyi kazi, akaishi, na maendeleo yakaja bila kazi. Na huyo anayepinga ujamaa naye ajiulize kama hilo analipinga? Na hilo la kufanya kazi analipinga au kuna jingine analopinga?" - Julius K. Nyerere

3. 'HAKUNA MTU KUMNYONYA MTU'

"...Kama binadamu ni sawa, tunalikubali hilo...Pili tunasema kitu kazi ni jambo la lazima kwa kila mtu, hakuna aliyesamehewa kazi. Basi siwezi kukufanyia kazi. Kukufanyia kazi maana yake ni kwamba wewe unasamehewa kazi! Siwezi kukufanyia kazi. Wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya. Sio mimi nifanye, wewe hufanyi; lazima ufanye kazi. Kwa hiyo wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya kazi; kila mtu atafanya kazi. Yaani namna ya kulitamka hilo ni kwamba kunyonyana hakuna. Hakuna mtu kumnyonya mtu; sasa tena msingi wa kumnyonya unatoka wapi? Tumesema watu sawa; na mtu ili aishi hana budi afanye kazi, na kazi ndio msingi wa maendeleo. Sasa mwanachama... ajiulize kama anaweza kuwa mjamaa na huku ananyonya! Unamnyonya mkeo; mkeo anakwenda kufanya kazi wewe unakwenda kupiga chibuku; hivi kweli mjamaa wewe? Tunasema kazi jambo la lazima, lakini wewe hufanyi kazi, unamnyonya mkeo. Wewe mjamaa? Nasema na hilo mjiulize...Unaweza kuwa mjamaa na huku unanyonya? Na anayepinga ujamaa ajiulize hilo nalo analipinga, kwamba yeye anaona kunyonya ni sawa tu! Sawa yeye kunyonya mwingine au wengine kumnyonya yeye, huyu anayesema kunyonya ni sawa. Kama kunyonya ni sawa baba, sasa tuanze kunyonya, au mkuki kwa nguruwe?" - Julius K. Nyerere

4. 'VYOMBO MUHIMU VIMILIKIWE PAMOJA'

"...Kama watu ni sawa; binadamu wote ni sawa; kazi ni jambo la lazima kabisa; kunyonya ni haramu; la nne linafuata: Vyombo vyote vya lazima, vinavyohitajika kwa maisha ya binadamu kwa kufanyia kazi lazima vimilikiwe kwa jumla. Ardhi lazima imilikiwe kwa jumla maana tusipoimiliki ardhi kwa jumla tutamwachia Rashidi Kawawa na Sheikh Karume wao wawe ndio wenye ardhi, na ardhi ni kitu cha lazima kwa maisha, hebu tuone kwanza usawa utakuwaje. Itakuwa lazima twende kwa Rashidi na kwa Karume, 'tafadhali bwana nataka ardhi'. Umekwishamwita 'Bwana' huyu; usawa umekwisha. Lakini vilevile kama Sheikh Kawawa ana ardhi, na Sheikh Karume ana ardhi, hawa hawalazimiki kufanya kazi. Kwa nini wafanye kazi? Hawawezi kufanya kazi. Tumesema kazi ni kitu cha lazima kwa kila mtu, lakini hawa hawawezi kufanya kazi, watakaa tu wanatutoza kodi kwa ardhi yao. Ndiyo wanatunyonya hivyo tena. Mimi nafanya kazi; mimi nalima. Halafu Rashidi anasema, 'Ukishalima mahindi ukapata magunia matano, moja langu'. Ndio ananyonya hivyo. Anavunja kanuni ya usawa; anavunja kanuni ya kazi; anavunja kanuni ya kutonyonya. Kwa nini? Kwa sababu tumemruhusu amiliki yeye vitu ambavyo vinastahili viwe vya wote. Mtu ambaye yeye ana ardhi; umemkabidhi viwanda, ukishakuwa umemkabidhi majambo mengine haya, umemwongezea nguvu zake, yeye utu wake umeongezeka-ongezeka na wangu mimi umeupunguza-punguza. Kwa hiyo vitu vilivyo vya lazima kwa kila mtu, kama ardhi ambayo ni ya lazima kwa kila mtu, lazima vimilikiwe na wote. Sasa...mjiulize kama unaweza kuwa mjamaa kweli huku unajidai ardhi yangu? Na wanaopinga wanatakaje? Hao wanaosema ujamaa mbaya. 'Eti vitu vyote viwe vya ujumla'; wengine waongo, 'Eti wanasema hata wakina mama wawe wa jumla'. Tunasema ardhi, hatusemi kina mama, tunasema ardhi viwanda, madini: kwa nini mtu mmoja anakwenda kuvinyakua vikawa vyake hivi!" - Julius K. Nyerere

5. 'KUUNDA NCHI BILA MATABAKA'

"..Kama tunakubali kuwa watu wote ni sawa; na watu wote ni lazima wafanye kazi, mtu asimnyonye mtu; na mali, mali kubwa, sikusema shati langu liwe la Rashidi: misingi ya uchumi kama mabasi yale yanapita iwe kwamba tunasema mabasi yetu, asiweko mheshimiwa mmoja pale anasema 'Basi langu lile!' Basi lako! Yupo dereva mle anaendesha, anasema dereva wake! 'Dereva wangu' - dereva wako, wewe unaweza kuwa na dereva? Dereva anaweza kuwa dereva wa umma, sio dereva wako. Dereva ni sawa sawa na mwalimu; mwalimu wa umma, daktari wa umma, dereva wa umma. Huyu anakuwaje 'wako'? Hata askari siku moja utasema wako. Kama tunakubali watu wote ni sawa; watu wote lazima wafanye kazi, hakuna kunyonyana; mali,vitu vyote vile vya jumla lazima viwe vya umma; maana yake ndio kusema tunataka kuunda nchi ambayo haina tabaka: hakuna mabwana na watwana." - Julius K. Nyerere

NUKUU ZIMETOKA KWENYE UJAMAA NI IMANI: MOYO KABLA YA SILAHA, 1973: EAPH KINACHOPATIKANA KATIKA MAKTABA YA MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP)
 
Back
Top Bottom