Heri yako Maganjwa maana umetuletea uzi wenye maana katika wakati tukitafakari namna ya kuikomboa Tanzania kutoka katika umagharibi, pengine niseme kuwa azimio la Arusha ndiyo mwongozo bora wa kutupeleka pahala sahihi kama tutalisimamia bila ya kuhujumu mazuri yote yaliyomo, lilitamuka wazi kuwa Tanzania ni nchi ya ujamaa na kujitegemea. nimeyapigia mstari haya maneno mawili kwasababu ndiyo nguzo ya kutuwezesha kupambana na sera mbaya za benki ya dunia na shirika la fedha la umoja wa mataifa ambazo msingi wake ni ubepari unaoelekea kukomaa hapa kwetu ili uwe ubeberu, hii ni hatari kabisa maana hakutakuwa na nafasi ya Tanzania kuendelea kama taifa bali mtu mmojammoja sasa wapi tuna kwenda? Azimio tena la Arusha litasaisia kuondoa unyonyaji, uonevu ,ukandamizaji, uporaji na mambo mengine yanayofanana na hayo kwahiyo , tukaze jamani tukaze, tujifunge mikanda tuweze kurejesha Azimio la Arusha ili uzalendo na maadili ya WATANZANIA KWA TANZANIA yarudi.