Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Kesho kwenye ukumbi huo huo, Rais Kikwete atazungumza na wazee wa jiji hilo hilo la Dar kuelezea yale yaliyojiri Dodoma. Natumaini ataweka mguu wake ardhini na kusema ni nini hakiwezekani. Ni matumaini yangu waandishi badala ya kukaa na kuangalia kama walivyofanya akiwaambia baraza la mawaziri watauliza maswali haya yasiyokaribishwa.

Waandishi wetu wajifunze kurusha maswali wasingoje hadi waambie basi kuna maswali. Waulize tu hata kwa kurusha hata kama hayatajibiwa.

Juzi Dodoma walikuwa na nafasi kubwa ya kumuuliza maswali lakini wakamuacha anaondoka huku wao (waandishi) wakikusanya vijinotebook vyao kuwahi kuripoti..

"Mhe. Rais, kulikuwa na tetesi kuwa ulikuwa unafanya jitihada za kuwashirikisha wapinzani kuna ukweli wowote"?

"Mhe. Rais kama itatokea Mhe. Chenge akaonekana kuhusika na kashfa ya EPA utakubali wakati huo ajiuzulu au hakuna chochote kumhusu Chenge kitakachokufanya umtoe ndani ya baraza lako"?

"Mhe. Rais ulishiriki namna gani kuhakikisha kuwa Richmond haipewi mkataba, hasa tukikumbuka kuwa uliwaambia waandishi kuwa hukutaka walipwe kwanza"

"Mhe. Rais Kabla ya Waziri Mkuu kutangaza kujiuzulu ulikuwa na taarifa ya kitendo chake hicho au na wewe kama Watanzania wengine ulikisikia/kukiona kwenye radio na luninga"?

n.k n.k
 
Viongozi wetu wanakosea sana!

Kuondoa Azimio la Arusha haikuwa ruhusa ya watu kutafuta mali kwa njia za halali; haikusema watu waanze ufisadi, na mengine mengi tunayoona sasa hivi. Hata huko ambapo ubepari umekomaa tunaona mafisadi na wala rushwa wanashughulikiwa na sheria.

Hadi pale tutakapokubali kufanya kazi na kuacha ndoto za mafanikio ya haraka bila kuweka jitihada za kweli itakuwa ndoto kwa watanzania kupiga hatua ya maendeleo.
 
Jamani:

Twendeni na wakati. Azimio la Arusha na Zanzibar ni matokeo ya mfumo wa chama kimoja. Na maagizo ya chama yalikuwa sheria za nchi.

Sasa hivi nchi ni ya vyama vingi na kunawengine hatuna mpango na ujamaa wala vyama vya kijamaa. Kitu kitakachotufanya tuwe pamoja ni sheria za nchi.

Bepari ana haki ya kuwa kiongozi na afuate sheria za nchi. Na masikini na naye haki ya kuwa kiongozi kama vile bepari.
 
Bin Marium,

Point yako nzito sana na ndio maana kila siku nalia na dira ya Kitaifa kuwa nchi hii inaongozwa bila dira...
Kwanza dira ni muhimu kisha Sheria zinajengwa kulinda dira ya Taifa na sio swala la chama kimoja ama matakwa ya rais fulani...Maazimio yote yaliyopita ni maazimio ya chama kimoja na hayawezi kuwa ya Kitafa hata kidogo.

Bila hivyo tutaendelea kuwafuga mafisadi nchini ktk kila sekta na haitawezekana kabisa kuwaondoa kwani bila dira ni sawa na msafiri jangwani asokuwa na navigator (dira). No matter how good you are mpango wa kutegemea kusoma nyota tutaishia kubaya...

Dira ya nchi haihitaji kuwa ni ya Kijamaa ama Kibepari, kwani Dira sio sera wala mrengo wa chama... Tujaribu kutofautisha vitu hivi. Na hapo ndipo tunapoweka maazimio yetu kulingana na wakati mfano sasa hivi tunahitaji Kuondoa Umaskini... Hili ni Azimio la Kitaifa na halina Kiongozi wala mwananchi....

Kiongozi kutokuwa mfanyabiashara haiwezi kuwa ni sababu ya Ujamaa wala Ubepari isipokuwa ni ilani inayoambatana na matakwa ya malengo ya dira yenyewe. Labda niweke sawa hapa kwa kusema pamoja na kuwa wapo madereva wazuri mara zote unahitaji dira ya kule unakokwenda iwe kichwani, imechorwa ama kifaa kinachokuelekeza lakini tusianze kubishana kwa nini sheria za kuendesha zinasema dereva haruhusiwi kuyafanya yale yalnayoruhusiwa kwa abiria mfano kula akiendesha ama kusikiliza simu...
Sheria kama hizi hazitazami kwanza unaelekea wapi na upo ktk njia gani bali ni sheria zinazojaribu kupunguza kama sio kuondoa ajali na pengine kupotea, hivyo basi madereva wetu wanaweza kabisa kubanwa na sheria ktk kufikia maazimio ya Kitaifa...

Hayo ni mawazo yangu na nadhani Azimio la Arusha lilikuwa na malengo ya kitaifa bila kujali kuwa sisi ni Wajamaa ama Mabepari.. isipokuwa sheria ndizo zingeweza badilishwa kurahisisha dira hiyo ya Kitaifa....

Azimio la Zanzibar liklikuwa kutupotosha sote, kwani kabla hatujafika tunakotaka kwenda amri nyingine inatolewa sio kutuambia ni wapi tunakotakiwa kwenda bali kumpa ruksa dereva kuendesha gari akiwa amelewa...

Azimo la Zanzibar halina mabadiliko yoyote kwa wananchi isipokuwa vifungu vyote vinawahusu viongozi!... That's a crap, huwezi kuweka Azimio linalowahusu watu wachache badala ya Taifa zima.
 
tatizo la azimio la arusha lilikuwa nini? ni watendaji au azimio lenyewe? kuna haja ya kulirudisha ili kupambana na ufisadi. kama hukuwahi kulisoma kwa kina hili hapa na wewe lipitie
 
tatizo la azimio la arusha lilikuwa nini? ni watendaji au azimio lenyewe? kuna haja ya kulirudisha ili kupambana na ufisadi. kama hukuwahi kulisoma kwa kina hili hapa na wewe lipitie

Mkuu unaongelea Azimio la Arusha au Mwongozo? Kama ni Mwongozo hakika inabidi urudi ili kudhibiti ufisadi katika uongozi! Ila kama ni Azimio la Ujamaa na Kujitegemea je uko tayari tutaifishe mali yako kwa ajili ya Taifa? Je, uko tayari kuona kuwa njia kuu za uchumi ziko chini ya wakulima na wafanyakazi badala ya wafanyabiashara na wanasiasa? Uko tayari kutomiliki mali binafsi?

Kama kweli uko tayari tuwasiliane zaidi tuone ni jinsi gani tutalirudisha Azimio!
 
There is no way...lazima litekelezwe sasa. watake wasitake.

Haiwezekani, haitekelezeki sasa kwa sababu mazingira ya wakati ni tofauti sana na wakati ule ilipotungwa. Walitakiwa waitekeleze tangu wakati ule huku wakiifanyia mabadiliko ambayo yangeenedana na mabadiliko mengine ya kimfumo wa uchumi duniani. Walichofanya ni 'kuiua' kiaina kwa kubadili msingi wake kutoka kwenye ujamaa kwenda kwenye ubapari
 
Ndani ya Azimio la Arusha kuna mengi mazuri yanayotufaa hadi leo. Mfano, 'equal distribution of the national cake' pato la taifa' haya bado ni mambo mazuri sana. Ukiangalia kwa sasa kuna tofauti kubwa sana ya maendeleo miongoni mwa mikoa yetu mingine ikiwa na maendeleo sana na mingine ikiwa imeachwa nyuma kabisa. Ninachokiona mimi, lifanyiwe marekebisho ili liende sanjari na hali tuliyonayo sasa. Dhima nzima ya azimio la Arusha lilikuwa nzuri, ukiangalia kuna baadhi ya nchi za Scandinavia zinataka kuwa na mfumo ambao umelezwa ndani ya Azimio la Arusha na mambo ya ni bomba, Sweden ni mfano mojawapo. Kwa upande mwingine kama likizingatiwa suala la ufisadi kwa kiasi linaweza kupungua. Lakini bado wasi wasi upo nani ataruhusu liwepo kama si hao mafisadi wenyewe. Labda semeni na nyie.
 
Mkuu unaongelea Azimio la Arusha au Mwongozo? Kama ni Mwongozo hakika inabidi urudi ili kudhibiti ufisadi katika uongozi! Ila kama ni Azimio la Ujamaa na Kujitegemea je uko tayari tutaifishe mali yako kwa ajili ya Taifa? Je, uko tayari kuona kuwa njia kuu za uchumi ziko chini ya wakulima na wafanyakazi badala ya wafanyabiashara na wanasiasa? Uko tayari kutomiliki mali binafsi?

Kama kweli uko tayari tuwasiliane zaidi tuone ni jinsi gani tutalirudisha Azimio!

Umesoma wapi ndani ya Azimio au nani aliyekwambia kwamba Azimio la Arusha linawataka watu wasimiliki mali binafsi? Miiko ya Uongozi ndani ya Azimio la Arusha ina mantiki hadi leo. Lisingeuwawa Azimio la Arusha tungelikuwa na watu wanaotafuta uongozi ili kutumikia wananchi na si kutafuta uongozi kwa udi na uvumba kwa ajili ya kutaka kuyatumia madaraka yao kujilimbikizia mali! Hivi sasa uongozi umekuwa dili kwa sababu hakuna sheria yoyote ambayo inawadhibiti ipasavyo watu wenye mali ambazo hazina maelezo ya namna walivyozipata wasiruhusiwe kuutafuta ama kupewa uongozi.
 
Jamani mmewekewa hilo andiko la azimio la arusha, lisomeni kabla ya kuendelea kujadili
 
Nilipokuwa mdogo wakati wa mvutano wa kifikra, niliona na kuamini kuwa Azimio la Arusha lilikuwa baya na ndilo lililozuia Tanzania kuwa Matajiri.

Nimejiliza maswali baadaye na mpaka leo kama kweli Watanzania walilisoma Azimio na kulielewa au ilikuwa ni mapokezi ya hadithi za kijiweni kuwa Azimio ni baya.

Majuzi wakati Mzee Munanka alipofariki, tuliambiwa kuwa Marehemu Munanka alikuwa fisadi wa Kwanza. Nakumbuka kina Mzee Rupia, Marealle na wengine wengi matajiri Watanzania wawe ni wabantu, wahindi au waarabu, walikuwa ni matajiri.

Je hawa Azimio liliwapita vipi? liliwaepuka vipi kina Nimrod Mkono, Reginald Mengi, Khatar Singh, Khambaita, SK. George, Somaiya, Rajani. Abdul Haji, Iddi Simba, Anthony Diallo na wengine wengi?

Azimio halikuzuia biashara, lilipiga vita Unyonyaji. Tafsiri ya Unyonyaji si na haiendani na Ubepari kama mfumo wa kiuchumi.

Tulichokosea sisi ni kuoanisha hasira za kumchukia Mkoloni na mdfumowake wa kinyonyaji kutumia Ubepari kutudhulumu na kutunyanyasa. Tukaamua kuita Ubepari kuwa ni Unyonyaji.

Lenin aliposema Capitalism is leech and moribund to society, tulipokelea kuwa Ubepari ni mbaya bila kuangalia kuwa ni vipi Ubepari unaweza kutumika kujenga mhimili wa mtaji kwa Taifa.

Azimio lilipiga vita unyonyaji na viongozi kutumia nafasi zao kujineemesha, ndio maana wale wote wanaodai leo kuwa Azimio lilikuwa bovu, ndio vinara wa Ufisadi!

Nimewaomba sana watu wakae chini na walisome Azimio la Arusha walielewe na ndipo tuanze mazungumzo kutathmini mapungufu yake na hata kuyaboresha, lakini kila siku watu wanapiga chenga na kuendelea kusema Azimio ni baya, limetuletea umasikini!

Je uhuru mpya wa Kibepari baada ya Azimio kufa mwaka 1992 vimetuletea neema na utajiri kama Taifa na Jamii?
 
Naomba niwakilishe nukuu kutoka wikipedia kuhusu tathmini ya Azimio la Arusha.

Arusha Declaration

From Wikipedia, the free encyclopedia


Jump to: navigation, search
The Arusha Declaration was made by Tanzanian President Julius Nyerere on 5 February 1967, outlining the principles of Ujamaa (Nyerere's vision of socialism) to develop the nation's economy. The declaration called for an overhaul of the economic system, through African socialism and self-reliance in locally administered villages through a villagization program.
The villagization program, implemented in 1973-76, sought to transform the pattern of rural settlement by congregating the rural population-which previously had been resident predominantly on dispersed family smallholdings-in nucleated villages of sufficient size to be efficient (in bureaucratic terms) units for the delivery of services. Involved in this plan was the idea that the new villages could also become the basis for a socialist system of production.
One important element in the evaluation of the Arusha vision depends on interpretation of the degree of consistency between policies implemented and intentions, as stated in the declaration. Particularly in the period beginning in 1972, policies were implemented that arguably were inconsistent with the positions developed in the Arusha Declaration. The formulation of the Basic Industrial Strategy involved a definite shift from the priority given to rural development in the declaration. There was increasing centralization of economic authority and urgency in the implementation of programs. The attempt to enforce the villagization ("Ujamaa Villages") program over two years, the abolition of cooperatives and local government, and the commitment to achieve universal primary education in two years all reflected an impatience to achieve political goals swiftly, even if it meant the loss of the principle of decentralized participatory rural development associated with the Arusha Declaration rhetoric and downplaying realism in the implementation of policies. At the same time, the emphasis on the ascendancy of politics-and politicians-over the bureaucracy and workers' participation in the management of state enterprise seemed to incorporate a heightened political radicalism, although at the expense of weakening the self-confidence and role of technocrats.
It is ironic that the regional commissioners charged with collectivization of the farms, for "egalitarian" purposes, following the Arusha Declaration enriched themselves at the farmers expense.
Politically and socially the declaration was hugely unpopular. In 1974 Operation Dodoma forced collectivization of farming with the use of the military. Following the murder of Klerru, a regional commission who sezied all of a Mr's Mwanwindi's land in 1975 and the public attention to the trial the collectivism of the Arusho Declaration finally ended. It was a complete failure and only plunged Tanzania into further debt, a crisis in its balance of payments deficits and worsened relations with international donors.

[edit] Excerpt From the Arusha Declaration

“It is particularly important that we should now understand the connection between freedom, development, and discipline, because our national policy of creating socialist villages throughout the rural areas depends upon it. For we have known for a very long time that development had to go on in the rural areas, and that this required co-operative activities by the people.… When we tried to promote rural development in the past, we sometimes spent huge sums of money on establishing a Settlement, and supplying it with modern equipment, and social services, as well as often providing it with a management hierarchy.… All too often, we persuaded people to go into new settlements by promising them that they could quickly grow rich there, or that Government would give them services and equipment which they could not hope to receive either in the towns or in their traditional farming places. In very few cases was any ideology involved; we thought and talked in terms of greatly increased output, and of things being provided for the settlers.
What we were doing, in fact, was thinking of development in terms of things, and not of people … As a result, there have been very many cases where heavy capital investment has resulted in no increase in output where the investment has been wasted. And in most of the officially sponsored or supported schemes, the majority of people who went to settle lost their enthusiasm, and either left the scheme altogether, or failed to carry out the orders of the outsiders who were put in charge — and who were not themselves involved in the success or failure of the project.
It is important, therefore, to realize that the policy of ujamaa Vijijini is not intended to be merely a revival of the old settlement schemes under another name. The Ujamaa village is a new conception, based on the post Arusha Declaration understanding that what we need to develop is people, not things, and that people can only develop themselves.…
Ujamaa villages are intended to be socialist organizations created by the people, and governed by those who live and work in them. They cannot be created from outside, nor governed from outside. No one can be forced into an Ujamaa village, and no official — at any level — can go and tell the members of an Ujamaa village what they should do together, and what they should continue to do as individual farmers.…
It is important that these things should be thoroughly understood. It is also important that the people should not be persuaded to start an Ujamaa village by promises of the things which will be given to them if they do so. A group of people must decide to start an Ujamaa village because they have understood that only through this method can they live and develop in dignity and freedom, receiving the full benefits of their co-operative endeavour.…
Unless the purpose and socialist ideology of an Ujamaa village is understood by the members from the beginning — at least to some extent it will not survive the early difficulties. For no-one can guarantee that there will not be a crop failure in the first or second year — there might be a drought or floods. And the greater self-discipline which is necessary when working in a community will only be forthcoming if the people understand what they are doing and why.
”
—Arusha Declaration, [1]
 
Mchungaji Kishoka anasema: “Nilipokuwa mdogo wakati wa mvutano wa kifikra, niliona na kuamini kuwa Azimio la Arusha lilikuwa baya na ndilo lililozuia Tanzania kuwa na Matajiri. Nimejiuliza maswali baadaye na mpaka leo kama kweli Watanzania walilisoma Azimio na kulielewa au ilikuwa ni mapokezi ya hadithi za kijiweni kuwa Azimio ni baya

Maelezo Kuhusu Azimio:
Azimio la Arusha lina sehemu TANO. Sehemu ya kwanza inazungumzia Imani ya TANU ambayo ni CCM kwa sasa. Tukiamini kwamba kila Mwana-TANU/CCM alikuwa anatakiwa kujua ama kuelezwa akaelewa chama alichojiunga kina amini nini ama kina imani gani na kupaswa kuwa muumini wa kweli wa imani ya chama alichojiunga.

Kama utakavyoona kwenye Sehemu hiyo ya kwanza, kuna vipendele (a) – (i).
Kwamba Binadamu wote ni sawa; (Je Mzungu, Mhindi, Mwarabu ama Mwafrika Fisadi ni binadamu zaidi kuliko wewe?) Kwamba kila mtu anastahili heshima; kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya Mikoa hadi Serikali Kuu. Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;…… Kipengele cha mwisho (i) kinasema kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa.

Ukisoma vyote (a) - (i) kimoja baada ya kingine, lazima utaona vifungu vyote ni muhimu, vina mantiki, na bila shaka utaviwekea tiki. Imani ya Chama chochote chenye kujali haki za wananchi na mustakabali wa Taifa na watu wake inapaswa kuwa na vipengele kama hivyo.

Pia katika sehemu hiyo yapo madhumuni ya TANU. Chama kinajiwekea mambo ya kutekeleza kuhakikisha kwamba Cha kinahakikisha Serikali inachukua hatua zanazowalinda wananchi na nchi yao kwa ujumla.

Sehemu ya Pili ya Azimio la Arusha inahusu Siasa ya Ujamaa. Chama cha TANU kilipaswa kuamua na kutamka ni itikadi ama siasa gani ambayo kitafuata. Itikadi ambayo itakuwa ina misingi ya nadharia za mfumo wa kisiasa na uchumi. Itikadi ya TANU ikawa Ujamaa na Kujitegemea.

Sehemu hii nayo ina vipengele vyake vinavyoelezea Siasa ya Ujamaa, ambayo TANU imeamua kuifuata, ni nini. Kuna kipengele kuhusu Unyonyaji, kwamba Siasa ya Ujamaa hairuhusu unyonyaji; kwamba njia kuu za uchumi sharti ziwe chini ya wakulima na wafanyakazi; kwamba kuna demokrasia; na kipengele cha mwisho ni kwamba Ujamaa wenyewe ni IMANI ambayo wana-TANU ambao ndio waumini wa itikadi hiyo lazima wawe nayo.

Sehemu ya Tatu inahusu KUJITEGEMEA. Kipengele hicho wala hakina mjadala. Mtu mzima usipoweza kujitegemea ni fedheha kwako na familia yako. Taifa lisiloweza kujitegemea nalo ni fedheha tupu maana litakuwa ombaomba na mwisho kutawaliwa na kuamuliwa mambo na mataifa ambayo Taifa linayategemea. Sehemu hii inaeleza jinsi ambavyo Mikopo na misaada kutoka nje inavyoweza kuhatarisha Uhuru wa Taifa. Katika sehemu hiyo ya Kujitegemea, Azimio linasema “Tumjali zaidi Mkulima wa Vijijini”. Kilimo kitiliwe mkazo kwa sababu Kilimo ndicho kilikuwa kikitegemewa kuleta Maendeleo. Hadi sasa ukweli ndio huo, kilimo ndiyo ‘ajira’ ya walio wengi nchini. Mwisho wa sehemu hiyo kuna maelezo kwamba Masharti ya Maendeleo ni Juhudi na Maarifa. Azimio linabainisha kwamba ili maendeleo yapatikane, mkazo uwe katika Watu, Ardhi, Siasa safi, na Uongozi Bora.

Sehemu ya Nne ya Azimio la Arusha inahusu umuhimu wa Wanachama wa TANU kuijua itikadi yao kikamilifu. Kipengele hiki nitakizungumzia baadaye.

Sehemu ya TANO ya Azimio la Arusha ndiyo sehemu ‘nyeti’ ambayo iligusa zaidi mustakabali wa viongozi ndani ya TANU. Mniwie radhi, Nita-copy na ku-paste sehemu hii ambayo ndiyo haswa iliyokuwa ikiwabana viongozi na ndiyo sababu ya kuzaliwa kwa Azimio la Zanzibar ambalo wengi tunaamini kwamba ndilo liliua Azimio la Arusha.

“SEHEMU YA TANO
AZIMIO LA ARUSHA

Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka 29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-
A. VIONGOZI
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanya kazi, na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari na kikabaila.
2. Asiwe na hisa katika makampuni mawili au zaidi.
3. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
4. Viongozi tunaofikiria hapa ni Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana na kifungu chochote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe.)”


Sehemu hii ya Azimio iliwekwa makusudi kuwadhibiti na kuwapima viongozi wote waliotaka kugombea uongozi. Walikuwa wanaambiwa: kama mtu anataka uongozi, basi awe tayari kukubaliana na masharti haya. Vinginevyo ruksa kuendelea kuwa mfanyabiashara kama alivyoamua Mzee Bokhe Munanka (RIP) na wengine ambao waliona kuwa matajiri ni bora zaidi kuliko kuwatumikia wananchi na kubaki maskini ka walivyokuwa wananchi wengine.

Kama ilivyo kwa ‘Mchungaji Kishoka’, wapo wengi kama yeye ambao walizaliwa miaka mingi baada ya Uhuru au hata wale ambao walikuwa wameshazaliwa, ama walikuwa mashuleni wakati huo, na wengine walikuwa watu wazima. Lakini katika makundi yote hayo, wapo wanaolizungumzia vibaya Azimio la Arusha bila kuelewa Azimio lenyewe lina nini ndani yake. Hata wale walioweza kunufaika na utekelezaji wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ama utekelezaji wa Azimio la Arusha, wapo ambao hawakumbuki tena kwamba siasa hiyo ama Azimio liliwasaidia, bila siasa ya Ujamaa na Azimio la Arusha, huenda maisha ya baadhi yao na uzao wao yasingelikuwa hivyo yalivyo hivi sasa! Si kusimangana ila ukweli ndio huo.

Kwa maoni yangu, mgogoro mzima wa kuliona Azimio la Arusha lilikuwa baya ni Sehemu ya Pili ya Siasa ya Ujamaa. Wengi wanaamini kwamba Siasa ya Ujamaa ndiyo sababu ya Taifa letu kushindwa kupata maendeleo. Baadhi ya watu ambao wamekuwa wakisema kwamba Siasa ya Ujamaa tuliyoamua kufuata ndiyo sababu ya nchi kutokupata maendeleo, ukiwaambia waielezee siasa hiyo na kwa nini wanadhani ilishindwa kuleta maendeleo wanashindwa kukupa jibu la kuridhisha kwamba kweli siasa hiyo ilikuwa haifai.

Tatizo kubwa liko kwenye kipengele (d) Ujamaa ni Imani:
Kinasema: “Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani Ujamaa ni imani. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini na kufuata kanuni zake….. Wajibu wa kwanza wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU ni kutii kanuni hizi za Ujamaa hasa katika maisha yake mwenyewe. Na hasa mwana-TANU kiongozi hataishi kwa jasho la mtu mwingine au kufanya jambo lolote ambalo ni la kibepari au kikabaila

Kipengele hicho kinamalizia na: “Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinazofuatana na siasa ya Ujamaa unategemea sana viongozi kwa sababu Ujamaa ni imani na ni vigumu kwa viongozi kujenga siasa ya Ujamaa ikiwa hawaikubali imani hiyo

Viongozi wengi hawakuwa waumini wa dhati ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Walikuwa wanafiki na wabinafsi. Hawakulipenda Azimio la Arusha tangu mwanzo kwa sababu waliona linawabana. Pia wapo wengine ambao walikuwa ni bendera tu yafuata upepo. Hao ndio wale ambao hawakuweza hata kujifunza Siasa ya Ujamaa maana yake ni nini. Kwa hiyo, hawakuweza hata kuwafundisha ama kuwaeleza wananchi kinaganaga juu ya manufaa ya Siasa ambayo Chama chao kilikuwa kikifuata.

Wapo wengine ambao walikuwa na imani kubwa na Mwalimu Nyerere kutokana na msimamo aliokuwanao wa kujali sana maslahi ya wanyonge. Wapo pia ambao kwa kutokuwa na elimu ya kutosha na uelewa mdogo wa mambo ya Siasa, walikuwa wakifuata tu alichosema Mwalimu Nyerere bila kuelewa yale kiongozi wao aliyokuwa akiyasimamia. Hawa ndio wale waliokuwa wakiimba kama kasuku “Zidumu Fikra …..” Ukiwauliza ni fikra gani hawajui, hawana cha kueleza.

Lakini kuna kundi lingine ambalo walimchukia Mwalimu kwa kuwa aliwazidi kwa akili na kuwa na upeo mkubwa wa kufikiri na kuelewa mambo. Wengine walikuwa na chuki binafsi kwa kuwa pengine Mwalimu katika kutekeleza kazi zake za uongozi aliwahi kuwachukulia hatua kali ama kuwaumiza wao au jamaa zao. Kundi hili kwa chuki tu, liliweza kubeza na kupinga hata yale mazuri Mwalimu aliyoyasimamia. Wapo na wengine ambao walijiona kwamba hata wao walikuwa na mawazo mazuri kuzidi ya Mwalimu, lakini Mwalimu hakuyatilia maanani ama aliyapinga na akayajengea hoja ya kwake yeye, na kuibuka mshindi wa hoja; ama kwa sababu ndiye aliyeshika rungu la uongozi, kulazimisha yake aliyoyaamini yeye.

Matokeo yake, katika kujadili kushindwa kwa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na Azimio la Arusha, wakawepo watu ambao bila kujua kwa undani madhumuni ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliyozaa Azimio la Arusha, ama kwa sababu nyingine yoyote waliamua kwamba Siasa hiyo ndiyo iliyoliletea umaskini nchini, na Azimio halikuwa muhimu wala halikuwa na manufaa kwa Taifa.

Hivi sasa, viongozi wa vyama vya Siasa, wasomi na wananchi wasioridhika na jinsi Serikali ya CCM inavyoendesha shughuli za nchi, hususan kwenye masuala ya ufisadi na matabaka yaliyojitokeza dhahiri ya Matajiri wa kutupa na Maskini wasiojua kesho watakula nini na watoto wao, na kadhalika, wamegundua kwamba kumbe Azimio la Arusha lilikuwa na mantiki. Pia, wapo wanaogundua kwamba Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea haikuwa na ubaya wowote, isipokuwa viongozi wa TANU na CCM waliopaswa kuwa mstari wa mbele katika kuijua, kuitetea na kuitekeleza hawakufanya hivyo kwa dhati. Kutokana na ubinafsi wao, hawakuwa na waumini wa kweli wa Itikadi waliyoamua wenyewe kuifuata!
 
Jamani mmewekewa hilo andiko la azimio la arusha, lisomeni kabla ya kuendelea kujadili

MN, Nimelisoma haraka haraka na kwa maoni yangu more than 85% percent ya yaliyomo bado tunayahitaji leo hii katika kuendesha nchi yetu. Sioni sababu zozote za msingi za kuachana na Azimio la Arusha.
 
I like this

A. VIONGOZI
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au
mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au
kikabaila.
2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya
34
Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha
Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye
vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe
).

Mume Kiongozi mke anamiliki kampuni au kinyume chake
 
Sehemu ya TANO ya Azimio la Arusha ndiyo sehemu ‘nyeti’ ambayo iligusa zaidi mustakabali wa viongozi ndani ya TANU. Mniwie radhi, Nita-copy na ku-paste sehemu hii ambayo ndiyo haswa iliyokuwa ikiwabana viongozi na ndiyo sababu ya kuzaliwa kwa Azimio la Zanzibar ambalo wengi tunaamini kwamba ndilo liliua Azimio la Arusha.

“SEHEMU YA TANO
AZIMIO LA ARUSHA

Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka 29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-
A. VIONGOZI
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanya kazi, na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari na kikabaila.
2. Asiwe na hisa katika makampuni mawili au zaidi.
3. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
4. Viongozi tunaofikiria hapa ni Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana na kifungu chochote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe.)”

Bibi Ntilie,

Mbona unasulubu namna hiyo bila hata kupaka mafuta ya kupuliza maumivu!

Yule Babu yetu angefurahi kweli kweli kutusoma!

Azimio la Arusha pamoja na siasa yake ya Ujamaa, lilitambua kuwepo kwa ubepari na ukabaila katika jamii. Hicho kipengele nilichokikazia kwa wino mwekundu ni ushahidi tosha kuonyesha ni upotokaji wa hali ya juu uliofanyika kuamini kuwa Azimio la Arusha ndiyo shina la Umasikini.

Zaidi, Azimio linaonyesha wazi kuwa lilikuwa na maono ya mfumo wa kibepari, ndio maana katika kipengele cha pili hapo juu, kinadhibiti nafasi ya viongozi kujipatia mali kwa kuwekeza mitaji au kuwa na hisa katika makampuni.

Ikiwa Azimio lilitambua kuwa jamii ni lazima iwe na Mabepari na Makabaila na zaidi kutambua kuwa kuna kujiwekea akiba na kujipatia kipato kwa kutumia hisa za makampuni, basi ni lazima tukubali Azimio la Arusha lilikuwa na mwamko wa kiuchumi na bora kuliko zile program za kijamaa za China, Cuba, Urusi, Korea Kaskazini na kwingineko.
 
Back
Top Bottom