Azim Dewji: Lissu amuombe radhi Biteko; Matamshi wanayotoa wapinzani hayapaswi kuumiza watu wengine

Nilichokielewa kikubwa kabisa ni...

Kama mh Tundu lisu siku awe kiongozi, angependa kuitwa majina ya hovyo kama anavyowaita viongozi wengine, Je angependa tumdharau kama anavyoonyesha kuwadharau viongozi wengine?

Dewj kaongea point

..Lissu ni kiongozi tayari.

..Ni anavumilia matusi ya kila aina toka kwa wana-Ccm.

..Wako vijana wa Ccm wanambeza Lissu kwa ulemavu alioupata kutokana na kushambuliwa na serikali.

..Kwenye siasa lazima mhusika awe na ngozi ngumu.
 
Duh, yaani hili tukio ndo Limetrend Zaidi kuliko Maandamano Yenyewe.

Bila hili tukio,Wengi wasingejua Kama Kulikuwa na Maandamano Yamefanyika..!
 
huyu mwamba awamu hii yupo oya oya sana,
hawa ndio wenyewe wanaoendesha gari kwa rimoti, wamefurahi kweli kweli tu avyoteseka!

bandari, wanyama, mafuta na hili la umeme hawa ndio wanufaika namba 1.......piga sana pesa hawa awamu hii, wanafidia
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Nchi hii haina mnyaturu mhindi.
Hiki ni kiwango kikubwa sana cha kutuona watanzania hatunazo.
Huyu mhindi baada ya kutuibia kwa mda mrefu kwa usaidizi wa watawala sasa amevimbiwa anaanza kututoboa macho kwa kidole.
Hawa watu ni wale wale
Rostamu - Tabora
Deuji - singida nk
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Chawa huyoo
Kwani Biteko hakujua hiyo njia ikuwa kwenye maandamano? Hapo ni nani wa kuomba radhi? Biteko ndie ali ingilia maandamano ya Chadema.
Ati serikali ikizuia maandamano. Kwamba Dewji ana ona maandamano ni fadhila na sio takwa la kikatiba. Huu ni upuuzi.
 
We gabachori kaa kwa kutulia ,unajua kwamba biteko ndiyo amevunja sheria?
Ataijulia wapi hiyo sheria, labda siku wakimtia jamba jamba na mambo ya kuficha sukari ndio atamuelewa huyo Mnyanturu Mwenzake...
Ilikuwa bahati sana waandamanji hawakumkamata huyo Biteko na kumchinja pale pale barabarani, ile ilikuwa provocation ya hali ya juu sana, kwa kitendo kile alichofanya, kutaka kukatiza katikati ya maandamano, na yeye kama NPM, ni kwamba hatoshi katika nafasi yake. Watu wana hasira na umeme, na yeye ndio mwenye dhamana, halafu anakwenda kuwasanifu na kuwapitiliza bila hata kutoa neno la faraja kwao...

Polisi nao wajitafakari, siku nyingine wasichanganye maandamano na hii misafara ya viongozi, ni hatari tupu ikiwa waandamanaji watageuka Mbogo na polisi kutumia risasi za moto kuwatawanya. Itakuwa maafa makubwa sana, na polisi ndio wa kwanza kulaumiwa... Hili liwe funzo kwa siku zijazo. Provocation haitakiwi kwa wenye hasira na maisha ya kuunga unga- umeme tabu tupu, sukari hata kijiko kimoja ni anasa, dollar hazipo za kutosha, nchi kama nchi tumekuwa Matonya (RIP) huko duniani, mashirika ya kutuma fedha kama world remit sasa wanakataa kufanya muamala kwa cash, na tunako elekea, Mungu anapajua... Ingawaje mwenye shibe hamjui mwenye njaa, tunawahitaji wenye shibe na watawala wasikie kilio cha wenye njaa na watoe suluhisho kabla mambo hayajawa mambo, ni hayo tu. Mwenye kusikia na asikie.
 
Kabisa ,viongozi wa msafara wa biteko walifanya kosa kubwa sana ,ni risk sana wasije kufanya tena upuuzi kama ule ,chadema ni wastaarabu ,wangeakuta waandamanaji wengine wangeichoma moto zile V8.
 
Nilichokielewa kikubwa kabisa ni...

Kama mh Tundu lisu siku awe kiongozi, angependa kuitwa majina ya hovyo kama anavyowaita viongozi wengine, Je angependa tumdharau kama anavyoonyesha kuwadharau viongozi wengine?

Dewj kaongea point
Ni jina gani baya Lisu hajaitwa? Au mtu akiwa kiongozi unamuona kama Mungu? Kiongozi unakwenda kupita kwenye maandamano ya watu wasiokubaliana na itikadi zako unategemea Nini?
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Dewji Kazeeka Mwili na akili , Yaani Lissu amuombe radhi Biteko !
 
Mimi ni Ofisa wa Serikali mstaafu na si shabiki wa chama cho chote wala Simba au Yanga. Nashangaa ofisa gani Mwandamizi wa Serikali anaweza kumpitisha Kiongozi ye yote wa kitaifa katikati ya halaiki ya maandamano ambayo ni rasmi, achilia mbali ya kiongozi mwenyewe kuafiki huo utaratibu. Ni aibu tupu kwa Tanzania kuwa hatuko chini katika viwango vya elimu tu lakini hata katika viwango vya utawala na uongozi!! Jambo hilo si la kutetewa hata kidogo. Rais mwenyewe anatakiwa alikemee jaribio hilo kwa sababu misiba inayoweza kuzuiliwa kabla ya kutokea mchezo huo ukienda kombo!
Naunga mkono.
Aliyempitisha Naibu Waziri Mkuu kwenye Barabara iliyoruhusiwa Maandamano achukuliwe hatua za kinidhamu na Wananchi tupewe taarifa
 
Back
Top Bottom