Azifichaye dhambi zake hatofanikiwa

Gerald Robert

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
337
219
AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA... mithali 28:13

Kuna Mchungaji mmoja hivi aliingia Bar na kuagiza Kilimanjaro baridiii,

Wakati mhudumu anaekekea kaunta kuchukua kinywaji alichoagizwa na yule mchungaji, akaanza kujiuliza maswali kama ifuatavyo

Hivi mchungaji kaniagiza Kilimanjaro, au nimemuelewa vibaya?

Mchungaji anywe pombe kweli!!

Hata, ngoja niludi nikamuulize vizuri, huenda nimemuelewa vibaya.

Yule Muhudumu akaludi tenapaka mezani pale alipoketi mchungaji,

akamuuliza tena,

hivi Mtumishi, Umeniagiza nikuletee Kilimanjaro baridi, au nimeekewa vibaya?

Mchungaji alipofahamu kwamba amegundulika kuwa yeye ni Mtumishi, ikabidi palepale abadilishe lugha,

akasema, nikweli binti umenielewa vibaya, yawezekana haujasikia vizuri.

Yaani mimi Mtumishi wa Mungu niagize pombe, kweli?

Mimi nimekuagiza uniletee Kilimanjaro Maji, sio pombe. Ila nahitaji yawe yabaridi sana.

Yule binti (muhudumu) akauliza kwa kuhoji, lakini Mchungaji, mimi sioni sababu ya wewe kuja hapa Bar kununua maji ya kilimanjaro wakati hata kwenye maduka ya kawaida maji hayi yanapatikana!

Mchungaji nae baada ya kuona anafahamika mpaka kihuduma kwamba yeye ni Mchungaji, ikabidi naye ahoji kwa upole,

Kwani wachungaji hawaruhusiwi kunywa maji yanayouzwa Bar?

Binti ambaye ni muhudumu akajibu,

Hapana mtumishi, wanaruhusiwa, ngoja nikakuletee.

Maji yalipoletwa, mchungaji akalipa hela, baada ya hapo akaondoka fasta hata maji yenyewe akayasahau palepale maana halikuwa hitaji lake.

Huo ndio ulikuwa ni mwisho na nwanzo wa mchungaji kunywa pombe.

Note: kila ulitendalo sirini ipo siku Mungu ataliweka hadharani.

UWE NA SIKU NJEMA.
 
Mmmh imani bila matendo ni batili tu.Ishi maisha yako,tenda mema na mengine utajaaliwa.
 
Barikiwa mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom