Azam TV yazindua full dozi

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
7,593
6,934
Azam TV yazindua full dozi

IMG_3884-1.jpg



Kituo cha Azam TV kimezindua promosheni ya Full Dozi Kutwa Mara Tatu ambapo ni fursa kwa mteja mpya atapewa king’amuzi bure, dishi bure na vifaa vingine ikiwa ni pamoja na kufungiwa king’amuzi hicho bure ikiwa mteja atalipia kifurushi cha kikubwa cha Azam Play kwa mwaka mzima.

shaffihdauda.co.tz ikataka kujua kwa upande wa mteja mpya ambaye anataka kununua king’amuzi cha Azam TV kwa ajili ya kuangalia ligi kuu Tanzania bara pekee, atafaidikaje na promosheni hii ya Full Dozi. Haya ndio yalikuwa majibu ya Yayha Mohammed: “Mpira sasahivi tumeweka katika package zote pamoja na plus, kwahiyo mpira upo pote, mtumiaji wa king’amuzi cha Azam TV akitaka kuangalia mpira pekee anaweza kufanya hivyo lakini haimnyimi nafasi ya kuchagua kuona huduma nyinginezo.”

Kwahiyo anaweza kuendelea kupata huduma hizi pana, lakini pia akaendelea kupata maudhui ya mpira ambayo ambayo inapendwa na mashabiki wengi wa soka. Mpira ni kijisehemu cha eneo pana katika huduma hii ambayo mtanzania anaweza akaipata kutoka katika promosheni hii.”

Azam inavifurushi vitatu vya mwezi ambavyo ni Azam Pure 15,000, Azam Plus 23,000 na kifurushi kikubwa kabisa cha Azam Play 28,000 ambacho ndiyo kinahusishwa kwenye kwenye promosheni hiyo ambapo gharama zake kwa miezi 12 ni shilingi 336,000 yaani shilingi 28,000 kila mwezi.

Septemba 20,2016
 
Hakuna poa kwani hao wamewaza mbali kwangu mie ni kawaida sababu naipenda Azam sababu ni LA LIGA tu Na naweza pata la liga kwa 15000/=
 
Hawa Azam wahuni tu, nimelipia full package ya 28000/= wamefungua zote ila zile za NTV Kenya, nk bado haziwaki, si mzitoe basi kuliko kutulingishia! Nina mpango bora niiwashe decorder yangu ya DSTV.
Japo bei ya dstv sio rafiki
 
Back
Top Bottom