Azam TV wanatuuzia vifurushi (package) bei ghali ukilinganisha na majirani zetu

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,064
13,732
Habari za midaa hii wajumbe!

Moja kwa moja kwenye mada. AzamTv wanachotufanyia sisi watanzania hakikubaliki. Azam tv ni yetu na ni ya mtanzania mwenzetu lakini wanatunyonya! Watwambie tatizo liko wapi, kama ni serikali tujue, kama ni TCRA tujue, kama ni TOZO tujue, kama ni kodi tujue.

Just imagine kifurushi cha Tsh 25,000/= Uganda wanalipia Ush 13,000/= ambayo ni sawa na Tsh 8,000 hivi na ushee.

Yaaani kutoka kwenye Tsh 25,000/= mpaka 8,000/= what a gape?

Zifuatazo ni link za vifurushi kutoka Azam Tv kwa nchi mbalimbali, ingia linganisha afu twambie kwanini sisi Watanzania kwanini tunatozwa hela nyingi kiasi hiki.

Tanzania


Kenya


Uganda



Screenshot_20230921-210042_Chrome.jpg
 
Uhitaji (Demand) wa Azam Tv hapa Tanzania ni mkubwa zaidi kuliko hizo nchi nyingine ndio maana ni bei sana hapa kwetu,

1. Azam Tv ina channel nyingi za kitanzania, huku kwetu utabadili channel kwa raha zako, ni tofauti na Kenya na Uganda kuna channel chache za nchi zao.

2. Mpira wa Tanzania una fatiliwa sana, kuna watu wamelipia azam kwajili ya mpira tu, huko nchi nyingine hata vibanda vya kuonyeshea mpira hawanaga habari na ligi zao wanaonyesha mpira wa ulaya tu.

3. Azam kawekeza zaidi Tanzania, ni mamia ya mabilioni yamewekezwa, hii ligi ya mpira tu azam kaweka bilioni 250 na kila timu unayoiona kwenye ligi kuu inapewa milioni 50 kila mwezi ndio mana huwezi kusikia sikuhizi team imekosa usafiri au malazi, hizi channels za kiswahili zimewekewa mabilioni kwajili ya mishahara ya wanaoendesha vipindi, camera za bei ghali, usafiri, kutafsiri muvi, n.k.

Bei zipo fair kabisa wala tusilalamike,
 
Habari za midaa hii wajumbe!!

Moja kwa moja kwenye mada. AzamTv wanachotufanyia sisi watanzania hakikubaliki. Azam tv ni yetu na ni ya mtanzania mwenzetu lakini wanatunyonya! Watwambie tatizo liko wapi, kama ni serikali tujue, kama ni TCRA tujue, kama ni TOZO tujue, kama ni kodi tujue!!
Watapunguza endapo tu ushabiki wa simba na yanga utakoma na ule wa tamthilia za kutafsiriwa.
 
Back
Top Bottom