AZAM TV imeniuzi kifurushi cha Access Denied!

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,675
22,265
Mods isomeke "mmeniuzia"

AZAM Tv wanatuibia wateja, nimekua nikinunua kifurushi cha Azam Tv kwa shiling 8,000/= kikiwa na chaneli muhimu kwangu, lakini kifurushi hicho kimepandishwa bei na kuwa shilingi 10,000/= hili si tatizo, tatizo ni pale wameondoa chaneli nyingi na kutuachia maganda matupu! Azam Tv hii ni dhuluma, hayo maganda matupu mnatuachia tuyafanye nini au mnataka ionekane kifurushi kina chaneli nyingi huku hazina kitu!
Azam Tv mnatuuzia vifurushi ndani ya magunia kwani hamtujulishi ndani ya kifurushi mna nini, huu ni utapeli.
 
Pamoja ni tatizo la vifurushi tatizo lao kubwa ni kununua ving'amuzi na madishi ya bei rahisi kisha wanatuuzia kwa bei kubwa, matokeo yake wanalazimika kutufanyia matengenezo kila siku vinginevyo hawatakuwa na watazamaji.
 
Back
Top Bottom