Azam FC mtoeni Dube kama mlivyomchukua Fei

Hakuna timu iliyomtaka, yeye kama yeye ndio alivunja mkataba
Sio kweli kuwa hakuna timu iliyomtaka, Fei hakuwa na 140m za kuvunja mkataba, alipewa. Wengi tulipiha kelele humu juu ya mlango ule uliofunguliwa kumpitisha Fei kutoka Yangà kwenda Azam. Ni mlango huohuo utumike kwa Dube pia ambae anasema Hana furaha Azam. Mlango ule haupaswi kufungwā tena na wala haufungiki tena.
 
What Goes Around.... Comes Around
Dube Kasema hataki kucheza Azam, unamwambia alipe 700,000,000 ili aondoke. Hivi Kuna mchezaji wa sh. 700m pale Azam? Hivi kama Fei angeuzwa kwa ,700m SI angeendelea kubaki Yanga hata kama hapendi kubaki Yanga? Hiyo bei ya 700,000,000 Haina uhalisia, ni kumfanya mchezaji acheze Azam hata kama hataki (mtumwa).
 
Unaona unavyojichanganya unampomsaini mchezaji unaweka thamani yake kubwa ili kusitokee uhuni kama huu wa dube, sasa wewe fei ulimwekea eti thamani yake ni m 100 kwa nini asilipe na kusepa. Sasa dube nae kama anayo hiyo hela analipa na kusepa
 
Kwani Azam wamekataa kumtoa?

Wamesema atoe hicho kiasi ambacho kimeelezwa kwenye termination of contract.

Yanga kumbuka walirudisha ile pesa ya Feisal ya kuvunja mkataba maana yake hawakutaka.

Azam wako tayari na kinachosubiriwa ni mchezaji kutoa hicho kiasi then akatafute maisha mengine.
release clause ya huo mkataba haisemi dola laki tatu,dube anawapa kiasi kilichoandikwa na hawataki,dube anaenda china
 
Fei hakufata utaratibu wa kuhama lakini alihamishwa, bei ya fei haikuwa 100m lakini aliondoka.

Azam inaiandama yanga haijulikani kwanini, au pengine Azam inaisaidia Simba kwenye mambo yake.
Azam imehusika na masakata ya yanga kama vile Obre Chirwa, Donald Ngoma, kavumbagu, Ngasa, Sure Boy, Fei, Litombo na wengine wengi kwa lengi ya kuihujumu na kuidhoofisha Yanga. Dube atapata shida kuondoka pale kama akibainika anataka kwenda Yanga. Hii ndio inayosababisha Azam kuboronga kwenye kandanda pamoja na uwekezaji wake mkubwa.

Tobo alilopitishiwa Fei kwenda Azam "lazima" litumike kumpitisha Dube kwenda anakotaka kwenda, maana scenarios zao zinafanana, wote hawana raha kwenye timu zao.
 
Tobo alilopitia Fei bado lipo, aonyeshwe tobo apite. ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa upanga. Tulionya kuhusu kutengeneza tobo kwaajili ya mchezaji mmoja tu ambalo halizibiki.
 
Mchezaji Hana furaha kucheza Azam, wale wachambuzi, mawakala na wanasheria waliokuwa wanamtetea Fei wako wapi kwenye hili? maana yanafanana kabisa. Vinginevyo mchezaji atakaa na kulipwa kwa misimu 2 bila kucheza.
Sasa si ndo mumchangie hiyo hela ailipe Azam aondoke?
 
Sio kweli kuwa hakuna timu iliyomtaka, Fei hakuwa na 140m za kuvunja mkataba, alipewa. Wengi tulipiha kelele humu juu ya mlango ule uliofunguliwa kumpitisha Fei kutoka Yangà kwenda Azam. Ni mlango huohuo utumike kwa Dube pia ambae anasema Hana furaha Azam. Mlango ule haupaswi kufungwā tena na wala haufungiki tena.
Bahati mbaya yako ni kwamba Azam haina wanasheria vilaza kama walioko utopolo.
 
Atacheza chini ya kiwango na kutumia kila wakati na kuumwa kila siku utamfanya nn? Hivi unajua Donald ngoma mzimbabwe mwenzake alikwendaje Azam kutoka Yangà?
Kucheza chini ya kiwango kwa makusudi ni kuihujumu timu.

Inapothibitika kwa hakika kuwa umeihujumu timu lazima uchukuliwe hatua katika mamlaka za soka.
 
Sasa si ndo mumchangie hiyo hela ailipe Azam aondoke?
hana bei hiyo, wacha akalime matikitiki kwanza kama mlivyomfanyia Obre Chirwa, au wacha aende hijja kwanza kama mlivyomfanya Fei Toto wakati akisubiri hatima yake. Azam mtapata hasara kwakuwa mtaendelea kumlipa bila kucheza kwa miaka 2. Donald Ngoma alikuwa anasema anaumwa kila siku na kukataa kucheza sasa ni zamu yenu kwa dube.
 
Bahati mbaya yako ni kwamba Azam haina wanasheria vilaza kama walioko utopolo.
hachezi sasa mfanyeni mnavyotaka na kumlipa mtamlipa tu. huwezi kumlazimisha punda kunywa maji hata ukiweza kumlazimisha kwenda mtoni. The white elephant in the room, endelea kumlipa wakati unaendelea kusubiri 700m. Ni wanasheria matope kabisa hao.
 
Fei hakufata utaratibu wa kuhama lakini alihamishwa, bei ya fei haikuwa 100m lakini aliondoka.

Azam inaiandama yanga haijulikani kwanini, au pengine Azam inaisaidia Simba kwenye mambo yake.
Azam imehusika na masakata ya yanga kama vile Obre Chirwa, Donald Ngoma, kavumbagu, Ngasa, Sure Boy, Fei, Litombo na wengine wengi kwa lengi ya kuihujumu na kuidhoofisha Yanga. Dube atapata shida kuondoka pale kama akibainika anataka kwenda Yanga. Hii ndio inayosababisha Azam kuboronga kwenye kandanda pamoja na uwekezaji wake mkubwa.

Tobo alilopitishiwa Fei kwenda Azam "lazima" litumike kumpitisha Dube kwenda anakotaka kwenda, maana scenarios zao zinafanana, wote hawana raha kwenye timu zao.
Daah!! kumbe ushabiki umekujaa, hebu jiondoe kwenye ushabiki kwanza mwanangu narudia " unapomsaini mchezaji unakuwepo mkataba wenye kuonesha mambo mengi tu, mshahara, nyumba, bima, kama ni mchezaji wa kigeni ndio basi tena mtaenda mpaka dakika za kucheza uwanjani nk nk lkn kuna kuwepo kipengere cha kuvunja mkataba, hakuna mkataba usiovunjwa, katika mkataba lazima mweke thamani ya mchezaji na mchezaji mwenyewe aijue mfano mdogo pacome kwa sasa ana bei gani kama timu ikitaka kumchukua unaweza kukuta ni dola laki moja, sasa kama ni hivyo inategemea na msimu mfano sasa hivi dirisha limefungwa hakuna timu inaruhusiwa kuongea na mchezaji ili kuhama kinachofanyika ni timu x inampa mchezaji hiyo hela ya thamani yake + mishahara ya miezi 3 mbele mchezaji analipa club yake anasepa na hutasikia ameenda timu fulani mpaka dirisha la usajili kwa sababu kukwepa rungu la FIFA hiki ndicho kilichotokea kwa fei yaan fei alikuwa na thamani ndogo yaan m 100 sasa azam thamani ya dube ni dola laki 3 kama anayo alipe asepe hapo ndio mtiti 😅 na kama kuna timu nyuma ya pazia inamuhitaji imsaidie dola laki 3 kimya kimya asubiri dirisha ajiunge nao.
 
Kwani Azam wamekataa kumtoa?

Wamesema atoe hicho kiasi ambacho kimeelezwa kwenye termination of contract.

Yanga kumbuka walirudisha ile pesa ya Feisal ya kuvunja mkataba maana yake hawakutaka.

Azam wako tayari na kinachosubiriwa ni mchezaji kutoa hicho kiasi then akatafute maisha mengine.
najiuliza, kweli thamani ya Prince M Dube ni USD 300,000 ( TZS 765 Milioni)?

Hii imepimwaje?

Mwenye ufahamu anijuze
 
Iyo ni janja tu ya Azam kutisha watu kwakua Dube anaujua ukweli na Tff wanajua ukweli.

Tff Wana nakala za mikataba ya wachezji wote na wanahifadhi wao.
Wanao mtaka prince pia wamesha usoma mkataba wote na kwasasa Wana angalia mchezo unavyokwenda.
 
Nimekusoma 👍🏾
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom