Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 59,802
- 104,747
Hautakiwi kuashughulikia walioshinda tenda inabidi ushughulikie waliotoa tenda. Mtu mpaka anapata tenda serikalini kuna watu kibao wameshaipitisha na wana gawio kubwa kuliko hao waliopata tenda. Kuwatesa walioshinda tenda ni kazi bure maana waliofanikisha ubadhirifu wa mali na fedha za umma wapo na wanakula maisha. Kuna watu wamepewa dhamana ya kulinda mali ya umma. Hawa ndio JPM alitakiwa awafilisi na awape tabu. Mwishowe nchi hii wale waliokuwa na influence kubwa kipindi cha Kikwete bado waliendelea kipindi cha JPM. Ukimuangalia Rostam na Home Shopping Centre. Unahangaika na wafanyabiashara baada ya kuhangaika na TRA. Unahangaika na Migodi badala ya kuhangaika na mawaziri waliokubali hio mikataba. Ndio maana tulishindwa kesi zote hizo. JPM alikuwa ni Rais wa wajinga na wavivu kufikiri
Uko sahihi kabisa, nilikuwa nikiuliza sana, mbona wafanyabiashara tu ndio walikuwa wanakomolewa, lakini viongozi waandamizi wa ccm na serekali hawakamatwi kwa kushirikiana na hao wezi?