#COVID19 Awamu ya Tano ilituaminisha kuwa Mungu kaondoa Uviko-19 ili tufarijike

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,723
Kiukweli uviko 19 au corona ilitikisa dunia na kufikia kupoteza watu wengi.

Kipindi cha mwendazake kutuambia mungu kaondoa uviko 19 baada ya kuomba mimi kwangu nililipa asilimia 2%.

Uviko 19 nchi zilizokumbwa ulivua nguo sekta za afya nyingi tena hizi za serikali.

Kuna mda mwengine tulikubari kudanganya au kudanganywa ili kupunguza ukweli kwenye sekta ya afya.

Hakuna sekta ya afya tena kwa nchi zetu hizi maskini ikapokea kwa mkupuo wagonjwa wa kupelekwa ICU 300 kwa wakati mmoja.

Hakuna sekta ya afya itakayoweza kuwa na vifaa kwa wakati mmoja kama vya kupumulia.

Lazima ingeleta simanzi na hasira kwa kila mtu anayetaka kumpambania ndugu yake au mtu wa karibu.

Huduma za afya zisingeweza kumudu idadi kubwa kama ingekuwa wazi na ndio maana ilikuwa siri kueleza takwimu ya wagonjwa.

Leo nimeona kueleza ili baada ya wenzetu wakirumbana kuhusu sekta za afya zilivoshindwa japo kuwa na mauwezo kuliko sisi.
 
Huo ugonjwa mpaka Leo bado hauna Solution na Mpaka Sasa bado siyo tishio Kama inavyotangazwa.

Hivyo hapakuwa na ulazima wa Watu Wengi kulazwa Wala mashine ya kupumulia kutumika. Maneno yote aliyosema mkemia Magufuli ndiyo yanayofuatwa na dunia nzima. Corona tutaishi nayo Kama magonjwa mengine.
 
Sawa ebu nieleze we ulitaka afanye nini....

JamiiForums1421820019.jpg
 
Mlikejeli barakoa za vitambaa mwamba akasema barakoa ni barakoa tu kitu kikasambaa dunia nzima, tukajifukiza,no lockdown wala bibi yake lockup,level siti tukatupilia kule,chanjo tumepuuza hadi wa leo zinadoda tu huko vituoni. Tukaongeza mauzo ya vitunguu swaumu,limao,tangawizi, pilipili manga.

Ila wajane wa bulldozer mkimmiss tu fasta mnamuanzisha uzi. Acheni Jiwe aitwe Jiwe. jamaa alijua kutetemesha balaa

R.I.P Shujaa JPM
 
Aibu kweli kweli.
Wakubwa wanavuana nguo kuhusu uongo wao, mkuu umeshupaza shingo na usiyoyajua!

Tuliochanja ndio tuko kwenye hatari na wasiwasi wa kutojua ni nini haswa wamedumbukiza kwenye hii miili.
Mlikurupukia chanjo za dezo dezo Kaka.

Pole, ila Mungu atawaponya kwa uwezo wake.

Eti chanjo! For whaaat!
 
Kiukweli uviko 19 au corona ilitikisa dunia na kufikia kupoteza watu wengi.

Kipindi cha mwendazake kutuambia mungu kaondoa uviko 19 baada ya kuomba mimi kwangu nililipa asilimia 2%.

Uviko 19 nchi zilizokumbwa ulivua nguo sekta za afya nyingi tena hizi za serikali.

Kuna mda mwengine tulikubari kudanganya au kudanganywa ili kupunguza ukweli kwenye sekta ya afya.

Hakuna sekta ya afya tena kwa nchi zetu hizi maskini ikapokea kwa mkupuo wagonjwa wa kupelekwa ICU 300 kwa wakati mmoja.

Hakuna sekta ya afya itakayoweza kuwa na vifaa kwa wakati mmoja kama vya kupumulia.

Lazima ingeleta simanzi na hasira kwa kila mtu anayetaka kumpambania ndugu yake au mtu wa karibu.

Huduma za afya zisingeweza kumudu idadi kubwa kama ingekuwa wazi na ndio maana ilikuwa siri kueleza takwimu ya wagonjwa.

Leo nimeona kueleza ili baada ya wenzetu wakirumbana kuhusu sekta za afya zilivoshindwa japo kuwa na mauwezo kuliko sisi.
Na ungemaliza kwakusema iliishaje .
 
Back
Top Bottom