Avunja ndoa ya miaka 20 kwa tabia ya mkewe kupakulia majirani chakula

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,492
2,164

Image: MARGARET WANJIRU

Mwanamume mmoja nchini Zambia amewaacha watu kwa mshangao kubwa baada ya kumpa mkewe talaka kwa sababu ya kuwa na mazoea ya kuwapakulia majirani chakula.

George Phiri mwenye umri wa miaka 49 aliamua kumuacha mkewe Tanta Zulu mwenye umri wa miaka 34 ambaye walidumu naye kwa ndoa ya miaka 20, tovuti ya Zambian Observer iliripoti.

Phiri aliamua kumshtaki mkewe mwishoni mwa juma katika mahakama ya Matero, akidai anatabia ya kugawa chakula, akiongeza kuwa amekuwa akiwapatia na watoto wa hao majirani.

Akijitetea, Zulu aliiambia mahakama kuwa mumewe alikuwa ni bahili na mkali hadi anafikia hatua ya kupima chakula kilichopo ndani ya nyumba kabla ya kwenda kazini, tovuti hiyo ilisema.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi Harriet Mulenga, alibainisha kuwa sababu za kuachana kwa wanandoa hao hazina msingi, lakini kwa sababu mlalamikaji alisisitiza kwamba hataki mke wake, mahakama ilikubali talaka.

Itakumbukwa tena nchini humo miezi kadhaa nyuma mwanamke mmoja alishangaza mahakama baada ya kudai kuwa alitaka kumuacha mumewe kwa sababu ya kumpata amenyoa sehemu nyeti bila kumtaarifu.

Katika taarifa hiyo ya kushangaza ambayo ilichapishwa na vyombo vya habari nchini humo, mwanamke huyo alisema kuwa alikuwa anataka talaka kwa sababu aligundua mumewe ana mwanamke wa pili na yeye hangeweza kuvumilia ndoa ya wake wawili.

Akiulizwa alijuaje kuwa mumewe ana mke wa pili, mwanamke huyo kwa jina Karen Chungu alisema kuwa siku moja alitaka kufanya mapenzi na mumewe lakini akapigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa alikuwa amenyoa nywele za sehemu za siri.


Credit Radiojambo
 
Watu wakishachokana huwa wanatafutiana vijisababu ilimradi tu wapate kuachana.

Hapo wote Mke na Mume kila mmoja alishamchoka mwenzie.
Jamaa yuko sawa kabisa nyinyi wanawake mna tabia ya kutothamini jasho la waume zenu.

Yaani mtu unajitutumua unanunua kidumu cha lita 5 cha mafuta ya kula kg 50 za mchele na unga, sukari kg 10 ili angalau upoze bajeti ya mwezi mzima ,lakini unakuja kushangaa hata wiki mbili havimalizi ukija kuchunguza unakuta mkeo alikuwa anavigawa gawa hovyo kwa mashost wake ambao na wao wana waume zao nyumbani.

Kiufupi mimi mwanamke mwenye akili za kipuuzi kama huyo nikimuonya akashindwa kujilekebisha namtimua mapema sana haiwezekani mashost wako wawe na thamani kuliko jasho langu.
 
Back
Top Bottom