Avatar ipi mnaipenda?

Ni Avatar gani Mwanakijiji aitumie?

  • Napenda ya mzee mwenye Jembe (ya zamani)

    Votes: 52 59.1%
  • Napenda ya mzee mwenye mkwaju (mpya)

    Votes: 35 39.8%
  • Asitumie Avatar yoyote

    Votes: 1 1.1%

  • Total voters
    88
Hebu support art kwa kuitumia ile ya mzee aliyechorwa. Inapendeza kuitazama nainaleta hisia za uanakijiji mkuu.
 
Mwanakijiji;

Irudishe basi ya babu mwenye Mkwaju. Huyu Mvuta bangi mtoe.

Ya Mkwaju ni nzuri zaidi na inapendeza. Usifuate upepo, yatakuwa yale yale kama ya kuchagua CCM simply kwa kuwa ni Brand Name lakini hamna kitu.

Shauri yako Mwaya!
 
Ya babu mwenye mkwaju. Maana kuna ukweli kabisa katika maneno ulyiyoyasema pale mwanzo kuwa ".....sasa ni kutembeza mkwaju tu!"

Lile jembe limekuwa butu. Halitifui tena si ardhi wala si kiburi cha mafisadi.

Hayo ya "kilimo kwanza" tumuachie Mh Rais.
 
Naona kuupgrade avatar yangu kumewakwaza wengine kidogo; wapo wanapenda niendelee na ile ya jembe la mkulima (black and white) na wengine wanapenda hii mpya ya mkwaju (ya rangi). Sasa sijui wapiga kura mnasema niendelee na hii mpya watu wataizoea au nirudie ile ya zamani ambayo kama mmoja alivyosema ni "brand image"..
mara nyingine huwa nadhani huyu jamaa ni imposter hau ndie mkulima mwenyewe rudisha mkuu. Yule jamaa ana endana na kauli zako.
 
jamani mwanakijiji una shamba la bangi?hii mbaya haina mvuto


karibu watu wote wanayoiangalia hiyo picha (ya kweli) huwaza bangi kwanza.. tangu nilipoiweka mara ya kwanza 2006 watu walikuwa wananiuliza nasokota nini.. jamani shamba la mahindi hilo..
 
karibu watu wote wanayoiangalia hiyo picha (ya kweli) huwaza bangi kwanza.. tangu nilipoiweka mara ya kwanza 2006 watu walikuwa wananiuliza nasokota nini.. jamani shamba la mahindi hilo..
Wakulima wa mahindi pamoja na magumu yote ya shambani, huwa wanaonyesha kujijali kidogo. Hii inaonekana kama mtu kajizira hivi, ndio maana wadau wazo la kwanza wanalolipata ni mtuamiaji wa kuleeeeeeeee.......kwa marehemu bob. Kwa nadharia ya kijijini kupata ushauri ni upendo wa wanakijiji wenzako kwako.
Ingawa bado, ushauri ni suala moja na kuuchukua au kuukataa ni suala jingine, but think twice.
 
karibu watu wote wanayoiangalia hiyo picha (ya kweli) huwaza bangi kwanza.. tangu nilipoiweka mara ya kwanza 2006 watu walikuwa wananiuliza nasokota nini.. jamani shamba la mahindi hilo..

Kama hii ni ya 2006 , hebu update " upige" ya 2010 maana naamini kutakuwa na mabadiliko na hasa kama unashiriki kwenye kilimo kwanza... (kidding!)

On a serious note picha hii inaonyesha hali halisi ya wakulima wengi huko vijijini - hali inasikitisha sana..pengine kama resources zitawafikia na kuwasaidia kuboresha kilimo kutoka jembe la mkono ( linalowachakaza na kuwafanya waonekane kama wamevuta.....) na kuwapatia angalau vitendea kazi na pembejeo vya kuwaondolea suluba labda afya na hali za wakulima wa kizazi kipya zitabadilika.

Having said that, binafsi naona uweke avatar inayowakilisha kile unachoamini... kama ni mkulima halisi wa Tz basi hii uliyoweka inafaa.
 
Mwanakijiji!

Ile ya zamani imekaa ki-SISIM. Hii mpya ni poa kabisa na tafadhali ISAJILI ili iwe official NEMBO.
 
Back
Top Bottom