Aunty Ezekiel: Wema anatutoa shimoni

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,458
7,837
Msanii wa filamu bongo Aunty Ezekiel, amejivunia kitendo cha msanii mwenzake ambaye pia ni rafiki yake mkubwa Wema Sepetu, kuzindua filamu ya Heaven Sent kwa aina ya kipekee, na kusema huenda likawa tumaini jipya kwa bongo movie.

01-9_0.jpg

Akizungumza kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa sinema jijini Dar es salaam, Aunty Ezekiel amesema anaamini Wema amekuja kubadilisha tasnia ya filamu na kuwatoa shimoni wasanii hao, ambao walikuwa wanaanza kupotea kwa kukaa kimya kwa muda mrefu bila kazi mpya sokoni.

"Nimekuja kumuunga mkono Wema Sepetu ambaye amekuja na filamu mpya, naamini amekuja kuibadilisha tasnia ya filamu, labda amekuja kututoa tulipo shimoni na kutuleta juu", alisema Aunty Ezekiel.

Aunty Ezekiel aliendelea kwa kusema ...."kwa njia moja au nyingine imeleta 'bongo movie' mpya, kwa muda mrefu hakujawahi kutokea kitu kama hiki, unapoingia tu hapa unaona kabisa tasnia ya filamu inaenda kubadilika, kwa hiyo ni kitu ambacho kinanipa faraja kama msanii", aliseme muigizaji huyo.

Siku ya Jumamosi tar 26 Agosti 2017, Wema Sepetu amezindua filamu yake ya 'Heaven Sent' ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu mbalimbli, wakiwemo waigizaji wa filamu za bongo na wa muziki pia.
 
Kawatoaje sasa maana uzinduzi tu tumeambulia maonyesho ya mavazi no movie trailer au wahusika wengine wa movie hio zaidi ya wema na magauni yake

Ukiingia mtandaon unakutana na sifa za make up,magauni ya wema na wengineo na sio cover wala uhusika wa kwenye hio movie.

Bongo movie bado sana
 
Wema ni chadema lazima apate washauri wazuri awezi kukurupuka tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umaarufu wa bongo movie wa kike hivi sasa ni UMALAYA kuliko kucheza movie..
Wanajiuza na kufanya ngono ovyo kwenye kichaka/kivuli cha bongo movie.
 
Kawatoaje sasa maana uzinduzi tu tumeambulia maonyesho ya mavazi no movie trailer au wahusika wengine wa movie hio zaidi ya wema na magauni yake

Ukiingia mtandaon unakutana na sifa za make up,magauni ya wema na wengineo na sio cover wala uhusika wa kwenye hio movie.

Bongo movie bado sana
Ndio hapo nami najiuliza na kukariri kwake magauni ya mtindo mmoja
 
..Nilikuwa nasubiria kwa hamu nione japo TRAILER ya hiyo Movie matokeo yake sijaona hata kwenye Page yake INSTAGRAM...Hata kwenye page za mitandao mingine hamna,,
Matokeo yake picha nakutana alivyovaa na kubadilisha gaurni mara 2. Hapo naona attention yote ilikuwa kwake yeye tu.
 
Mhhh! Kumbe Untie muhenga aisee! na make up zote bado uhunga umeshindwa kujificha? Basi acha watoke huko shimoni tu hakuna namna.
 
Niliangalia Nirvana ya wiki iliyopita ikiwaonesha mamiss wazamani walivyoungana na kufanya kazi pamoja yupo Mke wa Nyalandu na Nancy Sumari.

Niliipenda ile wale sahizi hawaoneshi maisha yao ila kazi zao.

Ila hawa wengine sijui walikosea wapi maskini, Tunayajua maisha yao kuliko kazi zao.
 
Back
Top Bottom