ATM za UmojaSwitch

mkuu ni mara mbili nimeshapata tatizo la Pesa kugoma kutoka kwenye ATM Machine, nilipita kwenye ATM za PBZ hapa Malindi Zanzibar, siku ya kwanza rlinasa 10,000 baada ya wiki 3 ikanasa 40,000, ATM machine ile ile nikaingia mpaka ndani ya Bank sikupata maelezo ya kuridhisha nikawapigia Azania Bank Dar ikawa hakuna maelezo ya kutosha sikuridhika, kwanini ikitokea tatizo kama hii hamuwezi kulishughulikia? Mbona CRDB nilipata tatizo nilipata huduma within 10 Minutes? Inabidi muangalie hayo mabenki mnayoshirikiana nao sio wastaarabu

Pole sana manyanza,
  1. Ulifanikiwa kutatuliwa tatizo lako? kama hapana niandikie kwenye uswege.mwaipyana@umojaswitch.co.tz nitalifatilia
  2. Tumekusikia na tunajitajidi sasa kuondosha kero kwa wateja wetu, ikitokea unapata shida siku ingine, kama umewasiliana na benki na bado hujaridhika, tafadhali wasiliana na sisi
 
Uswege utalipia matangazo hapa au bure!hongera kutaka kujua matatizo ya atm zenu ili mziboreshe,biashara ushindani jitahidini sana kuboresha huduma zenu,kama mtaweza washaurini equity bank nao wajiunge na atm zenu!!!!!
 
kwa kweli nimefarijika leo kukuta hii mada;
Nilifungua akaunt benki ya posta kwa matumaini ya umoja switch,lakini ni shida tu hapa Moshi,karibu matawi yenu yote hapa ni matatizo,hakuna mtandao kila mara na sasa sitaki hata kuweka fedha kwenye akaunt ya posta kwa ni usumbufu mwingine wakati fedha ni zako lakini zinakutesa
 
Wakati utapofika support yangu kwa JF utaiona tu.

Noted, Equity tutawakaribisha kwenye mtandao wetu.

Nashukuru pia kwa pongezi zako, ni lengo letu kwamba mteja asipate shida na inapotokea kakutana na tatizo basi isichukue muda kupata huduma.

kwa kweli nimefarijika leo kukuta hii mada;
Nilifungua akaunt benki ya posta kwa matumaini ya umoja switch,lakini ni shida tu hapa Moshi,karibu matawi yenu yote hapa ni matatizo,hakuna mtandao kila mara na sasa sitaki hata kuweka fedha kwenye akaunt ya posta kwa ni usumbufu mwingine wakati fedha ni zako lakini zinakutesa

Pole kwa Usumbufu Chief Mgalula, Ni ATM gani hapo moshi ambazo network zinasumbua? tunaboresha Network kwenye ATM zetu zote lakini kama kuna sehemu pana tatizo zaidi basi tutatoa kipaumbele kwa eneo hilo

Kwanini umoja switch hamuweki features za ku-support visa na master card, ili tusio wateja wa bank zilizopo under umoja switch tuwezw kutumia ATM zenu?
Lingine nikufahamishe kama hujawahi kulisikia, kipindi cha nyuma sera ya BOT ilikuwa ni kuwekeza kwenye National Switch moja kwa mabenki yote Tanzania. Na lengo ilikuwa ni kupunguza transaction costs, lakini nasikia baadhi ya banks ....hasa kubwa zilipinga sana suala hili!
 
Kwanini umoja switch hamuweki features za ku-support visa na master card, ili tusio wateja wa bank zilizopo under umoja switch tuwezw kutumia ATM zenu?
Lingine nikufahamishe kama hujawahi kulisikia, kipindi cha nyuma sera ya BOT ilikuwa ni kuwekeza kwenye ATM Switch moja kwa mabenki yote Tanzania. Na lengo ilikuwa ni kupunguza transaction costs, lakini nasikia baadhi ya banks ....hasa kubwa zilipinga sana suala hili!

Rich Dad,
Visa na MasterCard zipo kwenye mipango yetu, bahati mbaya sio kwenye mipango ya hivi karibuni, it is safe to say, at least not this year. Kila kitu ni project na sasa tunelekeza nguvu kwenye mobile channel, cardless na interbank transactions, hizi zote zitakua live kufika mwezi wa 11 mwaka huu.

Point of correction, BOT walikua wanaongea kuhusu national switch na sio ATM switch, ndio nimewahi kusikia, Labda itakua ni busara zaidi kwa wao kuiendeleza UmojaSwitch (zaidi ya 50% ya mabenki yote tanzania ni wanachama wa umojaswitch) kuliko kuanza switch mpya
 
safi sana mnajitahidi kutoa huduma nzuri,mi ni mmojawapo wa watumiaji wa huduma zenu,boresheni tu tatizo la networks baadhi ya sehemu other wise keep it up!
 
Ninashukuru Michese
 
Asante mkuu kwa kunisahihisha! Ngoja ni-edit post yangu hapo juu ili nisi wa misled watu.
Rich Dad,
Visa na MasterCard zipo kwenye mipango yetu, bahati mbaya sio kwenye mipango ya hivi karibuni, it is safe to say, at least not this year. Kila kitu ni project na sasa tunelekeza nguvu kwenye mobile channel, cardless na interbank transactions, hizi zote zitakua live kufika mwezi wa 11 mwaka huu.

Point of correction, BOT walikua wanaongea kuhusu national switch na sio ATM switch, ndio nimewahi kusikia, Labda itakua ni busara zaidi kwa wao kuiendeleza UmojaSwitch (zaidi ya 50% ya mabenki yote tanzania ni wanachama wa umojaswitch) kuliko kuanza switch mpya
 
discussion hii nzuri, ANGALIZO wana jf msije kujadiliana kuhusu PIN hiyo nenda personally kwenye tawi lako.

Mgeni hufanya vizuri kuja lakini hukaribishwa sebuleni tu.
 
Iswege,
Kama nimepoteza atm card yangu pamoja na simu, na kwenye simu kuna password (PIN), nitafanyaje haraka aliyeeiba asichukue fedha kwenye akaunti yangu ?
 
PIN huwa hatujadili, sio tu hapa hata kwenye tawi la benki, PIN ni siri ya mteja, hatakiwi mtu mwingine, hata ofisa wa benki yako, kujua PIN yako
 
Iswege,
Kama nimepoteza atm card yangu pamoja na simu, na kwenye simu kuna password (PIN), nitafanyaje haraka aliyeeiba asichukue fedha kwenye akaunti yangu ?

Kama unajua namba ya customer service ya benki yako wapigie wai-block, hii ni step ya kwanza halafu taratibu nyingine zitafata ambazo ni kutoa taarifa polisi na kuitaarifu benki yako kimaandishi (barua)
 
Pole sana manyanza,
  1. Ulifanikiwa kutatuliwa tatizo lako? kama hapana niandikie kwenye uswege.mwaipyana@umojaswitch.co.tz nitalifatilia
  2. Tumekusikia na tunajitajidi sasa kuondosha kero kwa wateja wetu, ikitokea unapata shida siku ingine, kama umewasiliana na benki na bado hujaridhika, tafadhali wasiliana na sisi

asante mkuu, sikuwepo humu jamvini baada ya kula BAN, hiyo ya tsh 40,000 nilipata solution, hiyo 10,000 sikupata solution maana niliona ni usumbufu nikaamua kuachana nayo, if possible unaweza kunisaidia mkuu..
 
ndio inawezekana, nitumie details za hiyo transaction kwenye email yangu.

1. ATM uliyotumia
2. Tarehe uliyoenda
3. Namba ya card (siyo PIN) ila namba hiyo imeandikwa juu ya kadi yako
 
ATM za Mabenki mengine yote ktk umoja Swtch ni nzuri but ATM zilizo ktk umiliki wa Bank ya Posta ni za ovyo na Mbovu na Muda mwingi hazifanyikazi, Pili Kadi ikitumbukia kwenye Mashine isiyo ya benki yako inachukua Wiki zaidi ya 5, why? Mwisho ATM za Akiba Na BOA zinakata fedha kwenye ac lakini hela haitoki kwenye mashine na wanachelewa kuirejesha kwenye ac,
 
ndio inawezekana, nitumie details za hiyo transaction kwenye email yangu.

1. ATM uliyotumia
2. Tarehe uliyoenda
3. Namba ya card (siyo PIN) ila namba hiyo imeandikwa juu ya kadi yako

Mkuu asante kwa msaada wako kweli sikumbuki tarehe lakini ilikuwa mwezi wa kumi mwaka jana next tym nikipata tatizo nitakushitua halafu kila kitu nilibadilisha ATM card pia nili renew kwa hiyo nahisi hata namba za kadi zilibadilishwa na mbaya zaidi tarehe niliuofanya yransactipn siikumbuki tena
 
Back
Top Bottom