ATM za UmojaSwitch

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Hello wanaJF, heshima kwenu

Kama una swali lolote kuhusu huduma za ATM za umojaswitch tuulize kwenye twitter uswegelm au @Linassamson mara zote tumia hashtag #UmojaSwitch

  1. tuambie kuhusu experience yako ya ATM za umoja
  2. Tupe mapendekezo ya maeneo gani ungependa tuboreshe.
  3. tuulize kama uko na swali lolote kuhusu ATM za Umoja.
  4. Tufikie wakati wowote utapohitaji kufanya hivyo kuhusu huduma zetu za ATM
 
Wewe/ninyi ni kama nani hapa!
 
Wewe/ninyi ni kama nani hapa!

Sisi UmojaSwitch, mtandao unaomilikiwa na mabenki, ambapo kwa pamoja (haya mabenki) wanamiliki ATM zilizoenea nchi nzima, naamini umeshawahi kuona ATM zetu.
 
Sisi UmojaSwitch, mtandao unaomilikiwa na mabenki, ambapo kwa pamoja (haya mabenki) wanamiliki ATM zilizoenea nchi nzima, naamini umeshawahi kuona ATM zetu.
Nina wasiwasi na wewe,Ebu funguka zaidi na ikiwezekana weka na some more informations ili watu wasikutilie shaka,otherwise u must be nigerian swindler/trickster!
 
Nina wasiwasi na wewe,Ebu funguka zaidi na ikiwezekana weka na some more informations ili watu wasikutilie shaka,otherwise u must be nigerian swindler/trickster!

kitu gani specific ungependa nifunguke. ukisoma maelezo unaona ninakaribisha maoni na ninasema tuko tayari kutoa maelezo kama wateja wetu wanayahitaji, kama mimi ndio natoa taarifa zetu na sio nakuomba wewe unipe taarifa zako ni vipi utapeliwe?

katika hayo maelezo yangu hakuna namna mtu anaweza kutapeliwa, tunajaribu tu kuwa karibu na wateja wetu, sio tu humu lakini ktk twitter na soon katika facebook, kwenye official website yetu ambayo currently na vyombo vingine vya habari.

lengo letu ni wateja wa UmojaSwitch waweze kupata huduma na habari kwa urahisi.

Kitu gani specific kwa mfano ungependa nifunguke au kinakupa wasiwasi?

Hello wanaJF, heshima kwenu

Kama una swali lolote kuhusu huduma za ATM za umojaswitch tuulize kwenye twitter uswegelm au @Linassamson mara zote tumia hashtag #UmojaSwitch

  1. tuambie kuhusu experience yako ya ATM za umoja
  2. Tupe mapendekezo ya maeneo gani ungependa tuboreshe.
  3. tuulize kama uko na swali lolote kuhusu ATM za Umoja.
  4. Tufikie wakati wowote utapohitaji kufanya hivyo kuhusu huduma zetu za ATM

"Your financial institution is unavailable" What the ef does this msg mean?
 
"Your financial institution is unavailable" What the ef does this msg mean?

Tripo,

  1. Asante kwa kufunguka, nitakujibu hili na pia tutaweka maswali ninayopata hapa kwenye FQA (Frequent Asked Questions) kwenye website yetu.
  2. Hiyo msg inatokea wakati server zinazoendesha ATM zinashindwa kuona server ya benki yako, taarifa za mteja zinakaa kwenye benki yako, unapoingiza kadi server ya ATM inawasiliana na server ya benki kupata kupata taarifa zako mfano balance ya account.

    Inapotokea benki yako, kwa sababu zozote, hawapo hewani, labda wanafanya matengenezo, au wana-run COB (wanafunga siku), basi utapata hiyo msg.

    ziko njia nyingine za kutatua hilo tatizo, benki nyingi zinatumia lakini baadhi ya benki hazifanyi kwa sababu report zinawaambia si mara nyingi watu wanashindwa kupata huduma kwa sababu hii, lakini kama itakua inaleta usumbufu sana tofauti na hizi benki zimekua zikiamini, (ambapo watu wa kutumbia ni ninyi wateja), basi UmojaSwitch itaongea na benki husika kuhakikisha wote wanadeploy stand-in.

Nimejibu swali lako tripo?

And I have 1

vizuri, so utapotaka kujua kitu chochote wakati wowote, tupate kwenye hizo twitter account mbili, remember hashtag #UmojaSwitch au kwenye facebook page, sasa hivi huduma kwa wateja ziko kwa kila benki, wakati tunaanza mwaka 2007 tulikua benki 6 sasa hivi benki ziko 23, sasa tunalazimika kufikiri tofauti, ndio maana tunafunguka zaidi hata kwenye mitandao ya kijamii na pia Plans are underway to have centralized call centre.

Kwanini ATM zenu zinatoa ela chafu sana?kuna siku nilitoa pesa zilikuwa chakavu kupitiliza na baadhi zilikuwa zimelika kama zimeliwa na panya?
 
Kwanini ATM zenu zinatoa ela chafu sana?kuna siku nilitoa pesa zilikuwa chakavu kupitiliza na baadhi zilikuwa zimelika kama zimeliwa na panya?

Hello Dully,

Pole kama umewahi kukutana na hilo tatizo, kuna wakati haikua kati ya vitu tunavyovifatilia kwa karibu, lakini tukagundua kuna tatizo kwenye ubora wa noti, moja kati ya vitu tunaviwekea mkazo sana sasa hivi ni ubora wa noti zinazowekwa kwenye machine.

Lakini naomba ieleweke kwamba pamoja na kwamba UmojaSwitch inasimamia uendeshwaji wa ATM na ubora wa huduma, tunategemea sana taarifa kutoka kwa wateja wetu ili kuboresha huduma.

kama utapata tatizo lolote, ikiwa ni pamoja na noti mbovu, tafadhali wasiliana nasi kupitia hizo twitter account zetu, au kupitia email address yetu au kupitia simu nambari 022-2775371 tuambie ni ATM gani kwa mfano kuna pesa mbovu sisi tutawasiliana na mhusika anayehudumia hiyo ATM kwa ajili ya kutatua hilo tatizo
 
Kwanini ATM zenu zinatoa ela chafu sana?kuna siku nilitoa pesa zilikuwa chakavu kupitiliza na baadhi zilikuwa zimelika kama zimeliwa na panya?

hili ni kweli kabisa,mimi nilishakutana nalo kwenye ATM ya pale manzese darajani karibu na ofic ya tigo
 
Nilitaka kujua viwango vya makato ambavyo mteja anakatwa pindi kuchukua pesa tafadhari
 
Hello wanaJF, heshima kwenu

Kama una swali lolote kuhusu huduma za ATM za umojaswitch tuulize kwenye twitter uswegelm au @Linassamson mara zote tumia hashtag #UmojaSwitch

  1. tuambie kuhusu experience yako ya ATM za umoja
  2. Tupe mapendekezo ya maeneo gani ungependa tuboreshe.
  3. tuulize kama uko na swali lolote kuhusu ATM za Umoja.
  4. Tufikie wakati wowote utapohitaji kufanya hivyo kuhusu huduma zetu za ATM

........Uswege,Mimi ni mtumiaji wa hizo ATM,tatizo hasa ilea pale bamaga petro station hakuna network kila Mara.Ile ya mwenge adjacent nanjeshini karibu na BRU haifanyi kazi kabisa.................naomba unifahamishe locations za ATM jijini Mwanza.
mwenzetu
 
Nilitaka kujua viwango vya makato ambavyo mteja anakatwa pindi kuchukua pesa tafadhari

Unapotoa Pesa
Unapotoa Pesa kwenye ATM unachajiwa - Tsh 550
Unapohamisha pesa kwenye kwenye account yako mwenyewe kwenye benki hiyohiyo - Tsh 550

Kuanzia mwezi wa nane kutakua na huduma nyingine
Kuhamisha pesa kwenda Account kwa mtu mwingine, benki hiyohiyo au benki nyingine mwanachama wa umoja - Tsh 550
Kumtumia mtu mwingine asiye na account wala kadi ya ATM (Cardless) - Tsh 550

Nimejibu swali lako Lidaku?
 
........Uswege,Mimi ni mtumiaji wa hizo ATM,tatizo hasa ilea pale bamaga petro station hakuna network kila Mara.Ile ya mwenge adjacent nanjeshini karibu na BRU haifanyi kazi kabisa.................naomba unifahamishe locations za ATM jijini Mwanza.
mwenzetu

Asante Mwenzetu,

  1. Tumesikia kuhusu ATM ya Bamaga, Mwenge kama ni ile ilikua karibu maduka ya vifaa vya ujenzi, imehamishiwa sehemu nyingine, lakini kuna ATM nyingine pale kwenye branch ya AZANIA opposite na soko la matunda mwenge.

  2. ATM zilizoko Mwanza
    • Mwaloni kwenye branch ya AZANIA
    • Kenyatta Road kwenye branch ya CBA
    • Nyerere Road kwenye branch ya AZANIA
    • PPF Plaza
    • Liberty Street kwenye branch ya Twiga Bancorp

....................asante sana kwa taarifa,.................
Mwenzetu
 
mkuu ni mara mbili nimeshapata tatizo la Pesa kugoma kutoka kwenye ATM Machine, nilipita kwenye ATM za PBZ hapa Malindi Zanzibar, siku ya kwanza rlinasa 10,000 baada ya wiki 3 ikanasa 40,000, ATM machine ile ile nikaingia mpaka ndani ya Bank sikupata maelezo ya kuridhisha nikawapigia Azania Bank Dar ikawa hakuna maelezo ya kutosha sikuridhika, kwanini ikitokea tatizo kama hii hamuwezi kulishughulikia? Mbona CRDB nilipata tatizo nilipata huduma within 10 Minutes? Inabidi muangalie hayo mabenki mnayoshirikiana nao sio wastaarabu
 
Back
Top Bottom