Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kuna mambo kadhaa ambayo yanakinyoshea kidole serikali kuhusika na utekaji wa Ulimboka. Maoni yangu hapa yanatokana na kitu tunachoita "profiling" ya mazingira ya incident ili ku-identify nani kahusika;
1. Utumiaji wa assault riffles - hizi bunduki za kivita zinapatikana kirahisi katika vyombo vya usalama vya serikali tu. Si rahisi watu binafsi wafanye mpango wa kumteka Ulimboka na watumie assault riffles. Kwanza hili nalo linaondoa kabisa dhana kwamba waliomteka ni ndugu wa walioathirika na mgomo wa madaktari.
2. Maswali aliyoulizwa "nani wako nyuma ya mgomo huu". Hili bila shaka ni swali kutoka ma-agent wa serikali ya CCM tu. Haiwezekani kikundi binafsi kikamteka na kuuliza swali kama hili. Kikundi binafsi kingekuwa kinatoa lawama kwa kusababisha vifo vya ndugu zao, sio kuuliza "nani yuko nyuma ya mgomo wenu". Kikundi binafsi kingekuwa kinamwagia Ulimboka shutuma za hasira, kama vile "ngoja na wewe tukukomeshe uone uchungu wa kuumwa", sio kuuliza maswali.
3. Kujiamini katika kumteka. Ulimboka ametekwa katika mazingira ya watu wenye kujiamini sana. Hawa ni professionals ambao inaonyesha wazi wamepitia mafunzo ya kikachero. Na pia "choreography" iliyofanyika hadi kumteka ni dhahiri watu wenye mafunzo ya ki-intelligence walihusika, na kwamba kulikuwa na "synchronised and orchestrated plan".
4. Kujiamini kuendesha gari isiyo na namba. Ina maana hawa watu walijua kwamba hata wangesimamishwa njiani na polisi walikuwa na uhakika wa kujieleza pamoja na vitambulisho. Mtu ambaye hahusiki na vyombo vy taifa vya usalama angetumia namba "feki" sio kuondoa namba za gari kabisa. Na watekaji binafsi wasingetaka kuendesha gari lisilo na namba muda mrefu hadi kule msituni. Na vyombo vya usalama vinapendelea magari meusi kwa operation za usiku.
5. Uteseji wa Ulimboka ambao ni wa ki-professional. Ulimboka alikuwa akiteswa kwa namna ambayo ingefanya aumie muda mrefu bila kufa. Mtu anayekupiga kwa kitako cha bunduki na anajua wapi akupige uli usife mapema kabla hajapata taarifa anayotaka, huyo ni mtu aliyefundishwa namna ya kutesa ili kupata habari - na huyo sana sana ni ofisa wa usalama wa taifa, wala sio polisi. Hata polisi hawana utaalamu huu, mara nyingi wakitesa mtu kwa ajili ya kupata habari wanaishia kuua, kwa sababu hawajui utaalamu wa kutesa bila kuua.
6. Utumiaji wa "safe house". Ulimboka alipelekwa kwenye "safe house" fulani kabla hajapelekwa msituni. Matumizi ya "safe house" ni ya vyombo vya usalama wa taifa, na ni kweli kwamba ni standard procedure kumfunika mtu uso wakati wanampeleka "safe house". Kwa mtekaji mwingine yeyote, si rahisi wateke mtu halafu kwanza wampeke "nyumbani", nyumba ambayo ni ya makazi binafsi. Uwezekano mkubwa ni kwamba walitaka ku-"minimize" muda wa kuwa na Ulimboka kule msituni na ilibidi watumie "safe house" ili kupata habari. Na pia ningependa kujua extent ya mateso aliyopata Ulimboka kabla ya kufikishwa "safehouse". Hilo litakuambia uamuzi wa kumuua ulifanyika wakati gani.
Kwa hiyo bwana, hata iweje, au muulize mtu yeyote aliyebobea mambo ya intelligence, atakuambia hii incident ya Ulimboka ina footprint kubwa sana ya chombo rasmi cha usalama cha serikali. In fact, kiongozi yeyote wa usalama aliyeidhinisha hili hakutumia busara, kwani suala zima limeacha footprint kwamba watu wa usalama wamehusika, na liko wazi kwa mtu yeyote yule anayejua mambo ya intelligence na counter intelligence.
Ni wazi kabisa kilichomwokoa Ulimboka ni watekaji kudhani alikuwa amekufa. Na hata ungeniambiaje hapa, uwezekano kwamba utekaji ulifanywa na watu professionals walioko serikalini ni zaidi ya asilimia 95%.
Labda JK anachohitaji kusema ni kwamba Ikulu haikuhusika, kwamba watu wa Usalama wa Taifa walifanya hivi on their own initiative.
Na pia, uwezekano kwamba hili lilifanywa na Usalama wa Taifa ni asilimia 90%, na kwamba lilifanywa na Polisi ni asilimia 60%. Uwezekano kwamba Polisi walishirikiana na Usalama wa Taifa ni asilimia 99%.
In fact, inaonekana hata Polisi Bunju waliona kila dalili ya kwamba chombo cha serikali kilihusika na huu utekaji, na kosa lilifanyika kumwacha hai wakidhani amekufa. Ninahisi kwamba kumwacha Ulimboka muda mrefu pale kituoni bila matibabu ilikuwa ni kujaribu kuona kama angekufa kabla hajapata msaada.