Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Ambao wameishadadia hiyo hoja ni wapinzani au CCM?

Hebu jaribu kupima thread zinazofunguliwa mfulululizo kutaka kumjibu Kakobe

Swali ninalojiuliza ni kuwa aliyeambiwa atubu amekaa kimya, wapambe ndiyo mnakanyagana na kuumizana!

Kulikoni??

Ngoja aliyeambiwa atubu tumsikie ajitokeze hadharani na kusema aidha anakubali kufanya toba hiyo au amekaidi - OVA
 
Askofu Zakaria Kakobe leo akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, amenukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu" amenukuliwa akisema Kakobe.[/QUOT
Ngoja niache kukujibu ili nikupuize
 
Nyie ndo mnaua upinzani huku mkijifanya wapinzani, hivi kweli kuna haja yoyote Upinzani ku-relax na kuona kama Kakobe kamaliza mchezo? Wa ajabu kwelikweli.
Kakobe katumia nafasi yake kama anavyopaswa kufanya, mbona mnahangaika naye sana kama hana impact?
Upinzani ume relax?? Ni vyema ukajua kuwa kimya kingi kina mshindo, ndio maana siku likitolewa tamko moja tu lumumba nzima na kule ferry mnachanganyikiwa na kupanic...
 
kweli Tanzania hakuna haki, kama naona maneno wanayo ongea kina Kakobe ndio ingekuwa Shekh Ponda kasema rumande tu mwaka bado kesi. hawa jamaa wanajiamini wanasema tu hakuna cha kushikwa wala nini? wale mashekh wa Zanzibar tu kusema hawataki muungano ndani mpaka leo kimyaa. Kakobe anashambulia kote muungano mpaka Rais lakini wanamjibu tu katika media. leo nimeamini Tanzania hakuna haki na waislamu wamejishusha wenyewe na njaa zao hawana misimamo. Respect kwa wenzetu.
 
Anamkosoa mtukufu rais! atakuwa anatumiwa huyo, itabid achunguzwe.
Hujakosea kabisa Nyaroka_Jr huyu Askofu Kakobe anatumiwa na Mungu alietoa agizo kuwa mtawala akikosea na ajulishwe makosa yake.... akishajulishwa makosa yake maana yake na [HASHTAG]#ATUBU[/HASHTAG]. huo ndio uchunguzi uliopo hakuna muda wala uchunguzi mwingine utakaofanywa ulete majibu tofauti na haya. [HASHTAG]#ATUBU[/HASHTAG]
 
Askofu kakobe amesikika kanisani kwake akiwaambia waumini wake kua, "kama rais au waziri wamekosea ni lazima kuambiwa ni wajibu wangu mimi kumwambia rais au waziri kua hapa umekosea".

Kisha akasema tena "mimi sina haja ya kunywa chai ya ikulu, chai n ile ile tu, na siogopi serikali maana hata mimi nna pesa kuliko serikali, kwani wenyewe si mnaona mambo ni haya pesa hizi, ndio, hata mawaziri wakiwa wana shida waje hapa mimi ntawakopesha".

NB: nna shindwa kuiweka hapa hio video ya askofu huyu. (ila unaweza kuipata kwenye ule mtandao wa youtube kwa ku search "kakobe amkemea tena rais").
 
Ubaya wa siasa za kudandia. Leo ukidandia kwa huyu kwa vile kaisema serikali vibaya na amekukosha, kesho akiisema vizuri kwa kuwa huna ajenda utamwita msaliti. Mwisho wa siku haueleweki na hauaminiki. Wanachama wakiondoka unasema wamenunuliwa!

Ziko wapi siasa zenje Sera mujarabu na mikakati maridhawa?

Siasa za kumkimbilia Wema Sepetu kwa vile kakorofishana na chama chake bado hazijatufunza tu?

Upinzani kama taasisi uanzishe mwendo na sio kudandia gari lisilojulikana uelekeo wake.

Safari ya Gwajima imeishia wapi? Safari ya Manji, safari ya Clouds, safari ya Nape! Kote huko hakuna fundisho lililopatikana? Au akili ndio imefikia mwisho?
 
Huyu Anajulikana tu, alianza kutabir mrema staingia ikulu hadi Leo hana jipya
We mbwa hata angetabiri maalim Seif kuwa rais bado angeonekana muongo maana ccm hawakubarik wapo kwa hisani ya vyombo vya dola......labda km vyombo vya dola vitageuka na kuanza kutumia akili zao baadae km walivofanya zimbabwe
 
Back
Top Bottom