SueIsmael
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 932
- 1,281
*ASKOFU KAKOBE AJIPE MUDA KUTAFAKARI .
Nimesoma mitandaoni maneno anayosadikiwa kuyasema kiongozi mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) lililopo Mwenge, Askofu Zakaria Kakobe akimsakama Rais Magufuli kwa maneno mazito na kumtaka atubu. Lahaula!
Nimebaki nikijiuliza kati ya Rais Magufuli na Askofu Kakobe nani anatakiwa atubu?!. *Askofu Kakobe anatakiwa aanze kutubu yeye* kwa sababu:-
1. Mwaka 1995 aliwaaminisha Watu kuwa Augustine Mrema atashinda urais na kuingia Ikulu. Kakobe alidai amepewa maono hayo lakini mwisho wa siku Mrema aliangushwa vibaya na Benjamin Mkapa akashinda urais. Kakobe ulishatubu juu ya hili?
2. Kakobe huyu huyu akaibuka tena 2015 akasema Mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa atashinda urais lakini akaishia kupata aibu nyingine ya Mgombea wake huyo kushindwa urais. Kakobe hakuwahi kutubu dhambi hii ya kuwadanganya Watanzania.
3. Kakobe aliwahi kuwaambia waumini wake umeme uliopita juu ya kanisa lake hautakaa ufanye kazi. Mpaka kesho umeme huo unafanya kazi. Kakobe alitakiwa aendelee kutubu tu kwa dhambi hii ya kuwadanganya mpaka waumini wake.
4. Kakobe huyu anayemvaa na kumrarua Rais Magufuli kwa maneno makali anatakiwa kuanza kutubu yeye maana ameshindwa kuheshimu mamlaka ya hapa Duniani wakati kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Mwenyezi Mungu amewaagiza Wanadamu kuheshimu mamlaka za hapa Duniani na za Mbinguni lakini huyu anayejiita Askofu Kakobe ameshindwa kulitambua na kuheshimu hili. Kakobe nenda katubu kabisa kwa kushindwa hata kuheshimu mamlaka, kuitii Biblia na kuheshimu agizo la Mwenyezi Mungu.
5. Kakobe huyu huyu anatakiwa atubu kabisa kwa kuanza kuhubiri siasa kanisani tena Madhabahuni (sehemu takatifu) badala ya kuhubiri neno la Mungu, kuhubiri Biblia inasemaje na kumuhubiri Mwenyezi Mungu. Kitendo cha kutelekeza neno la Mungu na kuvaa uanasiasa si tu kuwagawa Waumini wake bali pia ni kutikisa misingi ya amani ambayo imejengwa kwa gharama kubwa za jasho, mateso na kujitoa kwingi kwa Waasisi wetu. Kakobe nenda katubu kwa uchochezi huu.
Askofu Kakobe alitakiwa ajipe muda wa kutosha wa kufikiri juu ya matendo yake na kauli zake kabla ya kuzitoa madhabauni. Alipaswa kujifunza faida na hasara zake.
Askofu Kakobe alitakiwa aendelee kujifunza juu ya mwelekeo wa Tanzania Mpya na mwelekeo wake Mpya kwa sasa. Tanzania mpya ya sasa inayoongozwa na Rais Magufuli haina muda wa siasa za chini ya Mwembe tena.
Kwa Wahubiri wanasiasa kama Kakobe watamuona Magufuli ni tatizo ila kwa Watanzania Wazalendo tunamuona Rais Magufuli ni Mkombozi kwa Taifa letu. Tunamuona Rais Magufuli ndiye Mussa wa Watanzania wetu kwa sasa anayetutoa Misri kwenye mateso, anatuvusha bahari ya Shamu na kutupeleka Kaanani, nchi ya Maziwa na Asali. Daima sisi Watanzania wanyonge tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli siku zote, nyakati zote.
Utter bullshit! Tujifunze kutokuwa na double standards! Tutafuta mchawi mpaka kesho kutwa Ila tunajiloga wenyewe kwa kauli za kinafki kama hizi. Hata kama mtazamo wa Kakobe siukubali, Ila hii kauli haipangui hoja yake, ndio kwanza inadhihirisha mapungufu ya mwandishi.