madabadaba
JF-Expert Member
- Jan 12, 2017
- 288
- 178
Mbona hujampa like mwenye mapovu?Povu
Mbona hujampa like mwenye mapovu?Povu
It is schadenfreude when thieves cannot provide offering to their brain masters.Dick rider
Nonsense nuisance!Povu
viumbe wajinga kila anayejiita askofu mnamuaminiKwani askofu alimtaja raisi wetu? Au mmeshindwa kutafsiri mafumbo ya askofu wetu kakobe? Alichoongea askofu ni ukweli mtupu, hata hizo chaguzi unazozisema, alikaa na aliona kila chaguzi masisiemu hayakosi kuiba kura, na hakuna chaguzi isiyoibiwa kura tz, hata kitongoji kura zinaibiwa labda huishi bongo!
Acheni sindano za maaskofu zizame na sio kuleta visingizio vya kufanya siasa madhabahuni, soon tutaskia kaanza kufuatwa na nisani patrol8))
Okay hypothetically tuseme huyo bwana ametumwa au anatafuta kiki, vyovyote vile au sadaka but it is indeed what he claims is a somewhat naked truth only retards will repudiate that..It is schadenfreude when thieves cannot provide offering to their brain masters.
Naona sikukuu haikuwapa nafasi ya kula pesa za wizi maana hii siyo hasira ya kawaida. Sadaka pia zimepungua.
Nawe uko kwa Kakobe unasubili upatiwe uzazi, mimba?
Hii siyo dunia ya kusubili neema kanisani wakati mbele yenu kuna mtu aliyeshindwa ajira zingine.
Pengo na shekh wa bakwata dar wao kazi yao ni kuisifu tu serikali hao mbona hamsemi wanachanganya dini na siasa?Nimesoma mitandaoni maneno anayosadikiwa kuyasema kiongozi mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) lililopo Mwenge, Askofu Zakaria Kakobe akimsakama Rais Magufuli kwa maneno mazito na kumtaka atubu. Lahaula!
Nimebaki nikijiuliza kati ya Rais Magufuli na Askofu Kakobe nani anatakiwa atubu?!. *Askofu Kakobe anatakiwa aanze kutubu yeye* kwa sababu:-
1. Mwaka 1995 aliwaaminisha Watu kuwa Augustine Mrema atashinda urais na kuingia Ikulu. Kakobe alidai amepewa maono hayo lakini mwisho wa siku Mrema aliangushwa vibaya na Benjamin Mkapa akashinda urais. Kakobe ulishatubu juu ya hili?
2. Kakobe huyu huyu akaibuka tena 2015 akasema Mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa atashinda urais lakini akaishia kupata aibu nyingine ya Mgombea wake huyo kushindwa urais. Kakobe hakuwahi kutubu dhambi hii ya kuwadanganya Watanzania.
3. Kakobe aliwahi kuwaambia waumini wake umeme uliopita juu ya kanisa lake hautakaa ufanye kazi. Mpaka kesho umeme huo unafanya kazi. Kakobe alitakiwa aendelee kutubu tu kwa dhambi hii ya kuwadanganya mpaka waumini wake.
4. Kakobe huyu anayemvaa na kumrarua Rais Magufuli kwa maneno makali anatakiwa kuanza kutubu yeye maana ameshindwa kuheshimu mamlaka ya hapa Duniani wakati kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Mwenyezi Mungu amewaagiza Wanadamu kuheshimu mamlaka za hapa Duniani na za Mbinguni lakini huyu anayejiita Askofu Kakobe ameshindwa kulitambua na kuheshimu hili. Kakobe nenda katubu kabisa kwa kushindwa hata kuheshimu mamlaka, kuitii Biblia na kuheshimu agizo la Mwenyezi Mungu.
5. Kakobe huyu huyu anatakiwa atubu kabisa kwa kuanza kuhubiri siasa kanisani tena Madhabahuni (sehemu takatifu) badala ya kuhubiri neno la Mungu, kuhubiri Biblia inasemaje na kumuhubiri Mwenyezi Mungu. Kitendo cha kutelekeza neno la Mungu na kuvaa uanasiasa si tu kuwagawa Waumini wake bali pia ni kutikisa misingi ya amani ambayo imejengwa kwa gharama kubwa za jasho, mateso na kujitoa kwingi kwa Waasisi wetu. Kakobe nenda katubu kwa uchochezi huu.
Askofu Kakobe alitakiwa ajipe muda wa kutosha wa kufikiri juu ya matendo yake na kauli zake kabla ya kuzitoa madhabauni. Alipaswa kujifunza faida na hasara zake.
Askofu Kakobe alitakiwa aendelee kujifunza juu ya mwelekeo wa Tanzania Mpya na mwelekeo wake Mpya kwa sasa. Tanzania mpya ya sasa inayoongozwa na Rais Magufuli haina muda wa siasa za chini ya Mwembe tena.
Kwa Wahubiri wanasiasa kama Kakobe watamuona Magufuli ni tatizo ila kwa Watanzania Wazalendo tunamuona Rais Magufuli ni Mkombozi kwa Taifa letu. Tunamuona Rais Magufuli ndiye Mussa wa Watanzania wetu kwa sasa anayetutoa Misri kwenye mateso, anatuvusha bahari ya Shamu na kutupeleka Kaanani, nchi ya Maziwa na Asali. Daima sisi Watanzania wanyonge tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli siku zote, nyakati zote.
Naona wameamua kumjibu kakobe.
Source
Breaking news swahili.