Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Nimesoma mitandaoni maneno anayosadikiwa kuyasema kiongozi mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) lililopo Mwenge, Askofu Zakaria Kakobe akimsakama Rais Magufuli kwa maneno mazito na kumtaka atubu. Lahaula!

Nimebaki nikijiuliza kati ya Rais Magufuli na Askofu Kakobe nani anatakiwa atubu?!. *Askofu Kakobe anatakiwa aanze kutubu yeye* kwa sababu:-

1. Mwaka 1995 aliwaaminisha Watu kuwa Augustine Mrema atashinda urais na kuingia Ikulu. Kakobe alidai amepewa maono hayo lakini mwisho wa siku Mrema aliangushwa vibaya na Benjamin Mkapa akashinda urais. Kakobe ulishatubu juu ya hili?

2. Kakobe huyu huyu akaibuka tena 2015 akasema Mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa atashinda urais lakini akaishia kupata aibu nyingine ya Mgombea wake huyo kushindwa urais. Kakobe hakuwahi kutubu dhambi hii ya kuwadanganya Watanzania.

3. Kakobe aliwahi kuwaambia waumini wake umeme uliopita juu ya kanisa lake hautakaa ufanye kazi. Mpaka kesho umeme huo unafanya kazi. Kakobe alitakiwa aendelee kutubu tu kwa dhambi hii ya kuwadanganya mpaka waumini wake.

4. Kakobe huyu anayemvaa na kumrarua Rais Magufuli kwa maneno makali anatakiwa kuanza kutubu yeye maana ameshindwa kuheshimu mamlaka ya hapa Duniani wakati kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Mwenyezi Mungu amewaagiza Wanadamu kuheshimu mamlaka za hapa Duniani na za Mbinguni lakini huyu anayejiita Askofu Kakobe ameshindwa kulitambua na kuheshimu hili. Kakobe nenda katubu kabisa kwa kushindwa hata kuheshimu mamlaka, kuitii Biblia na kuheshimu agizo la Mwenyezi Mungu.

5. Kakobe huyu huyu anatakiwa atubu kabisa kwa kuanza kuhubiri siasa kanisani tena Madhabahuni (sehemu takatifu) badala ya kuhubiri neno la Mungu, kuhubiri Biblia inasemaje na kumuhubiri Mwenyezi Mungu. Kitendo cha kutelekeza neno la Mungu na kuvaa uanasiasa si tu kuwagawa Waumini wake bali pia ni kutikisa misingi ya amani ambayo imejengwa kwa gharama kubwa za jasho, mateso na kujitoa kwingi kwa Waasisi wetu. Kakobe nenda katubu kwa uchochezi huu.

Askofu Kakobe alitakiwa ajipe muda wa kutosha wa kufikiri juu ya matendo yake na kauli zake kabla ya kuzitoa madhabauni. Alipaswa kujifunza faida na hasara zake.

Askofu Kakobe alitakiwa aendelee kujifunza juu ya mwelekeo wa Tanzania Mpya na mwelekeo wake Mpya kwa sasa. Tanzania mpya ya sasa inayoongozwa na Rais Magufuli haina muda wa siasa za chini ya Mwembe tena.

Kwa Wahubiri wanasiasa kama Kakobe watamuona Magufuli ni tatizo ila kwa Watanzania Wazalendo tunamuona Rais Magufuli ni Mkombozi kwa Taifa letu. Tunamuona Rais Magufuli ndiye Mussa wa Watanzania wetu kwa sasa anayetutoa Misri kwenye mateso, anatuvusha bahari ya Shamu na kutupeleka Kaanani, nchi ya Maziwa na Asali. Daima sisi Watanzania wanyonge tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli siku zote, nyakati zote.

Naona wameamua kumjibu kakobe.

Source

Breaking news swahili.
Kakobe atakalia chupa soon, JPM sio Kikwete wala Mkapa
 
Leta takwimu hapa. Hakuna hata mmoja kati ya hao uliotaja alishinda. Hizi ni hadithi za vijiweni Watz. Kwa nini mnaonesha dalili zisizo na staha za kumchukia Dr. Magufuli. Huyu ndiye aina ya Rais Tz na Africa inamuhitaji kwa sasa. Mumezoea 'madili' mpaka makanisani tena bila aibu wala uoga kwa 'Jina la Yesu kristo?!
 
Bwana mdogo nae Amechoka sasa mana Kick zilikuwa kibao walau aonekane apewe u RC ila dizaini kama JPM kamvalia miwani ya mbao
 
Kakobe kakusudia Kuchota Michango ya Sadaka ya Team Ufipa next week maana Jamaa wiki ijayo watahamia huko wote kutoa kwa Gwajima
7e0591237f04730cfb2bbf2cf4c1f9eb.jpg
 
TATIZO LAKO UNAMCHUKULIA RAIS KAMA MUNGU WAKO NDO MANA UNAONA KAKOBE AMEFANYA KOSA. KAONDOE UJNGA HUO SHULE
 
Askofu Zakaria Kakobe leo akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, amenukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu" amenukuliwa akisema Kakobe.
Kakobe utapotea, vuta subira mtafuta janga hula mwenyewe
 
Maana tulikuona ukienda resi kwa mhe Halima Mdee eti kamsema vibaya rais Magufuli? Kisa alitaka Magufuli awekewe breki ukamtia ndani masaa 48.

Bishop Kakobe hajamung'unya maneno wala kupepesa macho. Amesema Magufuli akatubu maana anavunja sheria kwa kuendesha nchi kama vile ni ya chama kimoja. Na kama vipi atumie wabunge wake wa ccm walio wengi kubadilisha katiba, ili iseme nchi hii ni ya chama kimoja.

Mhe. Happi hayajakuuma maneno haya? Mtukufu akatubu?? Unakubali?
Wewe ni mpuuzi mtumishi wa Mungu halindwi na Mabunduki, au mizinga bali mkono wa Mungu uliotukuka hutanda pande zote asidhurike, yule siyo mwanasiasa anasema kweli na ndiyo itamweka huru, pia kwa nabii wa Mungu kudhuriwa na wapuuzi hasa wanasiasa ni ushuhuda wa kufa kwa ajili ya Mungu.
 
Zakharia Kakobe ni Mrundi ambae Wazazi wale walihamia Kigoma kwa Njia haramu Miaka ya 1960 Uhamiaji wafuatilie tumechoka kuishi na Wahamiaji Haramu

Pili Huyu Ana kesi ya kukutwa na fuvu la Binadamu Kanisani kwake Mwenge wakati wa Jk lakin kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji wakati wa Kikwete aliachiwa huru bila ya kuhojiwa ipasavyo, Jeshi la Polisi chini ya Jemedari Simon Sirro ifufue huu upelelezi

Kakobe anatafuta kick Kama ya Gwajima kwa kuwa anajua Next Sunday Team Ufipa yote itahamia kwa Kakobe kusikiliza 'Mahubiri' baada ya Gwajima kupoa
Kwahiyo hapo ndo umejibu hoja au?, mbona tofauti? Mbona huyo kakobe kazungumza kwa ufasaha tu kwamba mkuu wa nchi asikasirishwe na maneno, tena kwa nia njema tu. Amemtolea mfano kuna mkuu wa dunia watu humsema vibaya kila siku lakni hajali vipi wewe mkuu wa nchi? Hapo kuna ubaya gani? Kakobe labda ameona raisi anapoteza muda kujibizana na misemo ya msimu, kama vyuma vimekaza , au ule wa nyufa, au kusema eneo lako lina njaa, ni kupoeza muda kukimbizana na misemo hii, kwani hata waseme vp haitaleta athari yeyote ktk mlaka yake. Au hata kwa nchi. Ukiwa mtu mzima yakupasa kuwa na kifua sio unakurupuka tu. Hamna baya hapo mi nadhani kakobe anampenda na anamtakia mema zaidi raisi kuliko hata wewe.
 
Mleta hoja ni mchochezi na alistahili akae lupango masaa 48+ kwa kumfundisha mkuu wa wilaya kazi! Na hata akifanya ulivyomtuma itasaidia nini ilihali dunia nzima imeshasikia? Sio kila mahali na wakati sheeia au kanuni ile inaweza kutumika kwani haijaathiri amani wala utendaji wa yeyote. Acha uchochezi wa kitoto!
 
Back
Top Bottom