Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Nahisi wanasikilizia upepo.........pia aliyeandika huu uzi aweke na video......
[HASHTAG]#kakobhe[/HASHTAG]
 
Kakobe analeta uchochezi na huu ujinga anaoufanya haupaswi kuvumiliwa
Mnachopaswa kufanya ni kujibu hoja zake kwa fact. Kuita uchochezi bila fact yoyote haisaidii. Mwisho wa siku kwanini hamkubali mawazo tofauti? Mwanadamu hakuna mkamilifu hivyo ukisemwa acha kutafuta sababu za kujitetea, jiangalie kama kinachosemwa ni kweli chukua hatua. Kama sio kweli songa mbele kila mtu ana mdomo wake anayo haki ya kuongea. Mbona JK aliweza hili sana tu, mtu akiongea ili mradi havunji sheria hakuna shida.
 
kakobe huyu huyu alieshtakiwa na wachungaji wake kwa kujimilikisha sadaka za kanisa?
Ndio huyu huyu si unakumbuka na ile kashfa yake ya kumuuzia kimada wake nyumba za kanisa na ile skendo yake ya kununua kivuko kibovu cha kanisa!
 
Askofu Zakaria Kakobe leo akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, amenukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.
Amina Baba Askofu Kakobe.Umesema kweli

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu" amenukuliwa akisema Kakobe.
 
Unajua Askofu kakobe anajijua uaskofu aliupataje kitapeli Askofu wa kiukweli angekuwa na uhusiano nzuri na Askofu wa Magufuli ambaye ni kardinali lengo akiwa na jambo angeenda kuongea na Askofu wa Magufuli Pengo na kumnongoneza kitu akamnongoneze muumini wake Magufuli .ninachokiona kuna maaskofu immature Ndani ya katoliki ,Lutheran,akina gwajima ,kakobe nk ambao hawajui majukumu ya uaskofu ni yepi na ukiwa na jbo na muumini wa kanisa lingine lisilo lako unatakiwa ufanyaje.shame on them all
Humjui kakobe ndugu kwa uliyoyaongea
 
Kakobe is right.
Uncle ni muoga kama kunguru, ndio maana anaonyesha tabia za kidikteta na kutovumilia kukosolewa.
 
Mbaya ni kupanda daradara harafu hujui uendako wacha watumishi wa mungu wanyooshe maelezo tujue safari yetu ndani ya hii daradara
 
HUYU NI ASKOFU DUME,atakuwa ameoa huyu,wale wenye kulembua macho HAWAWEZI kukemea uovu,na akitokea mwana baraza akakemea,utaona wanakimbilia kukanusha.
Big up KAKOBE.
 
December 25, 2017
Dar -es-Salaam, Tanzania

Askofu wa Kanisa la FBGF (Full Bible Gospel Fellowship ) HOME - fgbfchurch.org makao yake Makuu jijini Dar-es-Salaam, Bishop Zachary Kakobe aomba Mh.John Joseph Magufuli atubu, sikiliza ombi hilo live:

c.c Goliath Mfalamagoha Crimea Mods Francis12 bampani
 
Yehodaya upo sahihi Mkuu lakini kwa mtu kama Kakobe haitaji kumtafuta nani ampelekee ujumbe Mh. ilitakiwa yeye mwenyewe afuate taratibu za kumuona Magufuri kuliko kuongea sehemu za ibada mambo ya siasa hata kama ni ushauri mzuri kwa mazingira aliyoyatoa inaleta chuki baina yao...
we nyoko kabisa,aache kuhubiri mema afanye kazi ya kutafuta watu?
Yeye ametoa mahubiri wala hajamjeruhi mtu.
 
Back
Top Bottom