Askofu Zachary Kakobe yupo wapi? Mwaka wa pili haonekani Uraiani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
ASKOFU wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (BGBF), Zachary Kakobe yupo wapi?

Ni mwaka wa pili sasa haonekani Kanisani. Hata Mke wake anaweza kuja Kanisani mara Moja kwa mwezi.

Je, kuna aliyemuona Askofu huyu huko mliko au kukutana naye?

Na wanaosambaza habari eti kapoteza kumbukumbu, naomba hizo habari msinipe mimi kwani nyie sio wasemaji wa Familia au Kanisa.

Kama anaumwa augue pole ila Kakobe ni Baba yetu wa Kiroho na tunamtegemea kwa Huduma.

Kanisa au Familia ijitokeze iseme yupo wapi ili kuondoa minong'ono isiyo furahisha. Baba yetu yupo wapi?
Bishop_Zachary_Kakobe.jpg

Kakobe anachunga kanisa Kubwa sana Dar-Es-Salaam, ambalo ni kanisa mama na amewafundisha yeye mwenyewe na kuwatuma kwenye mashamba ya Bwana zaidi ya wachungaji 700.

Jumapili, tarehe 7 Machi, 1993; aliwatawadha kundi la kwanza la wachungaji 28 (Wachungaji 19 na Wachungaji Wasaidizi 9); na kuwapa mamlaka ya kufungua makanisa tanzu ya kwanza 19 (au makanisa mtoto), katika makao makuu ya mikoa yote 19 iliyokuwepo Tanzania bara enzi hizo;

Na Februari 2000, Kakobe tayari alikuwa ameshaanzisha zaidi ya Makanisa tanzu 400 (au Makanisa mtoo) yaliyo tapakaa mikoa na wilaya yote ya Tanzania bara.
20230324_174530.jpg

Mara ya mwisho mimi kumuona alikuwa na Hayati Magufuli katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es salaam
 
ASKOFU wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (BGBF), Zachary Kakobe yupo wapi?

Ni mwaka wa pili sasa haonekani Kanisani. Hata Mke wake anaweza kuja Kanisani mara Moja kwa mwezi.

Je, kuna aliyemuona Askofu huyu huko mliko au kukutana naye?
View attachment 2563984
Bado anaomboleza msiba wa nduli magufuli akiwa kanisan kwake mawasiliano barabara ya kawe maana kipindi cha awamu ya tano aligeuka mpiga zumari kama masukuma gang na wale nguruwe wa uvccm.
 
ASKOFU wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (BGBF), Zachary Kakobe yupo wapi?

Ni mwaka wa pili sasa haonekani Kanisani. Hata Mke wake anaweza kuja Kanisani mara Moja kwa mwezi.

Je, kuna aliyemuona Askofu huyu huko mliko au kukutana naye?
View attachment 2563984
Kakobe anachunga kanisa Kubwa sana Dar-Es-Salaam, ambalo ni kanisa mama na amewafundisha yeye mwenyewe na kuwatuma kwenye mashamba ya Bwana zaidi ya wachungaji 700.

Jumapili, tarehe 7 Machi, 1993; aliwatawadha kundi la kwanza la wachungaji 28 (Wachungaji 19 na Wachungaji Wasaidizi 9); na kuwapa mamlaka ya kufungua makanisa tanzu ya kwanza 19 (au makanisa mtoto), katika makao makuu ya mikoa yote 19 iliyokuwepo Tanzania bara enzi hizo; na Februari 2000, Kakobe tayari Kakobe alikuwa amesha anzisha zaidi ya Makanisa tanzu 400 (au Makanisa mtoo) yaliyo tapakaa mikoa na wilaya zote za Tanzania bara.
Lengo lilisha timia, amezipiga za wajinga, amepumzika. Hana haja ya kupayuka tena mana alikuwa anjua kuwa anawadanganya wajinga! Nasikia ana jengo matata kwake hata New York halipo :D :D :D :D

Sasa zinapigwa na Mwamposa, wajinga bado wengi na wanazidi kuzaliwa!
 
Kuna Uzi Fulani uliletwa humu JF mtoto wake wa Kiume nae anamtafuta,hajaonana nae miaka mingi sana na ameandika barua zaidi ya 300 na kuzifikisha Kanisani ila majibu hajapata,ni mtu mzima kidogo,sasa unaweza kuona ilivyo kazi kujua alipo.
 
Safi sana acha apge Hela alizovuna Kwa wajinga,Sasa hvi ni wakati WA mwingine kuvuna
 
Ningekuwa na kipaji cha kupiga makelele kwa sauti ya kukoroma, muda huu na mimi ningekuwa nakula hela tu za wale wenzangu na mimi wanao amini kila kitu wanacho ambiwa.
 
Bado anaomboleza msiba wa nduli magufuli akiwa kanisan kwake mawasiliano barabara ya kawe maana kipindi cha awamu ya tano aligeuka mpiga zumari kama masukuma gang na wale nguruwe wa uvccm.
ukabila haufai , acha lugha za kikabila , kutumia ukabila ni ishara ya umaskin wa hoja
 
Kuna jengo moja maeneo ya mbezi beach niliambiwa ni la kwake, aisee ni bonge la hekalu hadi nikashangaa baba mchungaji aka. mtumishi wa bwana kujikita kujenga ufalme duniani badala ya mbinguni.
 
Kuna Uzi Fulani uliletwa humu JF mtoto wake wa Kiume nae anamtafuta,hajaonana nae miaka mingi sana na ameandika barua zaidi ya 300 na kuzifikisha Kanisani ila majibu hajapata,ni mtu mzima kidogo,sasa unaweza kuona ilivyo kazi kujua alipo.
huyo mtoto wake ni wa mtaani, kabla hajaoa na kabla hajaokoka, enzi hizo kakobe alikuwa kwenye bendi za mziki wa kienyeji huko hajaingia kwenye injili kabisa, na inasemekana hadi miaka ya 2000 alikuwa anasali pale kwake na watu walimjua kamani mtoto wa kakobe, ila alianza tabia za kijinga akafukuzwa, mlevi wa ajabu. mtu kama ameshafika miaka 18 akaleta ujinga, huyo ni mtu mzima, fukuzia mbali kabisa huko. mfano, hivi wewe mtoto wako akiwa shoga, utaendelea kuishi naye au kumsapoti? si unamkana kabisa na kumfuta?
 
Back
Top Bottom