Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Hali ya sintofahamu imeendelea kutawala kuhusu alipo Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship (BGBF) Zachary Kakobe.
Ikiwa ni miezi michache imepita tangu Frank Zachary Kakobe ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa Askofu Kakobe kutoa taarifa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari kuwa hafahamu alipo Baba yake kwa muda wa miaka miwili huku akidai kuwa jitihada za kumuona zimegonga mwamba.
Pamoja na Frank kutoa kauli kadhaa kuhusu Kakobe inadaiwa kuwa kuna hofu na tayari mjadala unazidi kufukuta chini kwa chini kwa baadhi ya Wanafamilia, ambapo baadhi ya ndugu wa familia ya Kakobe wanadai kuwa hawajamuona kwa miaka takribani miwili hadi mitatu kufikia Oktoba 2023.
Mmoja kati ya Wanafamilia ambaye anadai alizoea kukutana na Askofu Kakobe wakati alipokuwa akija Dar es Salaam kutokea Mkoani Kilimanjaro anapozaliwa Askofu huyo, alisema ni zaidi ya miaka mitatu sasa imepita yeye pamoja na baadhi ya Wanafamilia hawafahamu alipo Askofu huyo.
Mwanafamilia huyo amesema kuwa wanapofuatilia kufahamu wapi alipo majibu yanayotolewa ni kuwa “Kakobe anaandika vitabu 200 vya dini”.
Ananukuliwa akiseam "Ni miaka mitatu sasa imepita hatujamuona, mimi nilipokuwa nakuja Dar es Salaam nilikuwa naonana naye lakini kwa sasa ni miaka mitatu imepita kila ukifuatilia wapi alipo unaambiwa yupo mzima anaandika vitabu jambo ambalo naamini si kweli."
Frank Zachary ambaye alianza kutoa taarifa ya awali anadai licha ya jitihada kadhaa za kumtafuta Baba yake kupitia Vyombo vya Habari lakini juhudi zote hizo ziligonga mwamba.
"Mpaka sasa sijui halipo baba yangu nimefanya kila jitihada hata kwenda nyumbani kwake lakini kuna ugumu kuingia, najiuliza Baba yetu yuko wapi."
Ameongeza "Siku nilipotoa taarifa kwenye Vyombo vya Habari nilipokea simu za watu wengi wakinitaka ninyamaze na kudai Baba yupo anaandika vitabu, wengine wakasema ningewaambia kabla ya kusema, lakini kumbuka kwamba nimeshafatilia nimeenda mpaka nyumbani kwa Mzee majibu ninayopata ni yaleyale ya vitabu, sasa najiuliza kuna siri gani hata kama anatunga vitabu ndio asionekane au waseme wapi anapotungia vitabu."
Aidha, Mtu mmoja ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Askofu Kakobe alipoulizwa kuhusu wapi alipo Askofu huyo alidai yupo anatunga vitabu na kuwa taarifa nyingine tofauti na hizo ni uzushi huku akisema kuwa majukumu mengine ya kanisa lake amewaachia watu wa karibu waendelee kutoa huduma ikiwa yeye anaendelea na utunzi wa vitabu.
"Yupo ni mzima hana shida yoyote alikuwa na kazi ya kutunga vitabu takribani 200 amejikita kwenye suala hilo mengine akawa amewaachia wengine watu wake wa karibu.
“Wengi wamekuwa wakitoa taarifa zisizo sahihi hayuko wapi sijui kaenda wapi, kumbe anaendelea vizuri.''
Hata hivyo baadhi ya watu wa karibu kwenye kanisa lake wanakiri kuwa hawajamuona muda mrefu na kuwa sababu ambayo imekuwa ikielezwa kwao ni kwamba yupo anatunga vitabu.
Maelezo yaliyotolewa na Frank Kakobe alidai kuwa sintofahamu kwake ilianza baada ya kutumiwa picha ya Baba yake akiwa anaonekana katika hali ambayo anadai akuizoea.
"Nilitumiwa picha ya Mzee wangu nikabakia kushika tama na kutoa machozi huku nikijiuliza lini Mzee ameanza kufuga ndevu maana katika maisha yake nilivyomzoea hakupenda kabisa ndevu lakini kwenye picha ile ndevu zilikuwa zimejaa mpaka mashavuni.
“Hofu yangu ilianzia hapo kuongezeka na nikaongeza kasi ya kumtafuta lakini bado sijabahatika kumuona au kujua alipo," anasema Frank Kakobe.