tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,850
- 18,260
Wakati akihubiri kwenye kanisa lake la FGBF, Mwenge jijini Dar es Salaam, Askofu Zakary Kakobe amesikika akisema kuwa Tanzania ni mpango wa shetani ndio maana kila mara hoja ya kuitaka Tanganyika inaibuka. Hebu msikilize wewe mwenyewe:
MAONI YANGU
Askofu Kakobe ni miongoni mwa viongozi wa dini ninaowakubali sana hapa nchini. Hana unafiki na uchawa kama walivyo akina Geodavie, Kuhani Mussa na wengine, hasa linapokuja suala la kutetea maslahi mapana ya taifa na ustawi wa wananchi.
Marehemu Karume aliwahi kusema kuwa ikiwa koti linakubana ni vizuri ulivue na kulitupilia mbali. Kwa hali ilivyo sasa, naona koti la muungano tayari limebana. Hakuna faida zozote za muungano kwa watanganyika. Wazaznzibar ndio wananufaika zaidi na muungano huu. Wameona haitoshi wameamua kuuza bandari ya Tanganyika kwa waarabu. Wakati sasa umefika tuamue kunyoa hizi nywele chafu zilizojaa chawa kwa manufaa yetu na ya vizazi vijavyo.